2 Nyakati 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 15:1-19

Asa Afanya Matengenezo

115:1 Hes 24:4; Amu 3:10; 2Nya 24:20; 2Sam 23:2; 2Nya 20:14; 2Pet 1:21Roho wa Bwana akamjia Azaria mwana wa Odedi. 215:2 Yak 4:8; 2Nya 20:17; Kum 31:17; 1Nya 28:9; Ebr 12:25; 2Nya 33:12-13; Yer 29:13; Mt 7:7; 2Nya 12:1-3; Rum 11:1-2Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. Bwana yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Kama mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini kama mkimwacha yeye, naye atawaacha ninyi. 315:3 Law 10:11; Mao 2:9; Amo 8:11; Hos 3:4Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria. 415:4 Kum 4:29Lakini katika taabu yao walimrudia Bwana, Mungu wa Israeli na kumtafuta, naye akaonekana kwao. 515:5 Amu 19:20; Zek 8:10; Amu 5:6Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa yeyote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa. 615:6 Mt 24:7; Isa 19:2; Mk 13:8Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina. 715:7 1Sam 24:19; Mit 14:14; Rut 2:12; Za 58:11; Mt 5:12-46; Lk 6:35; Kol 3:24Lakini kwa habari yenu ninyi, kuweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu.”

815:8 2Nya 13:19; 8:12; 1Fal 8:64Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya Bwana iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la Bwana.

915:9 2Nya 11:16-17Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni waliokuwa wanaishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba Bwana Mungu wake alikuwa pamoja naye.

10Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa. 1115:11 2Nya 14:13-15Wakati huo wakamtolea Bwana dhabihu za ngʼombe 700, kondoo na mbuzi 7,000 kutoka zile nyara walizoteka. 1215:12 2Fal 11:17; 2Nya 23:16; Neh 10:29; 1Nya 16:11; 2Fal 23:3; 2Nya 34:31Wakafanya agano kumtafuta Bwana, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote. 1315:13 Kut 22:20; Kum 13:9-16Wale wote ambao hawangemtafuta Bwana, Mungu wa Israeli wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke. 14Wakamwapia Bwana kwa sauti kuu, kwa kupiga kelele, tarumbeta na kwa mabaragumu. 1515:15 Kum 4:29; 1Nya 22:9; 2Nya 14:7Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo Bwana akawastarehesha pande zote.

1615:16 Kut 34:13; 2Nya 14:2-5; 1Fal 15:2, 10Mfalme Asa akamwondolea Maaka mama yake wadhifa wake kama mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo, akaivunjavunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni. 1715:17 2Fal 12:3; 1Fal 3:2-4; Kum 12:7; 1Fal 15:14; 2Nya 14:3-5Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika Israeli, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote. 18Akaleta ndani ya Hekalu la Mungu fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.

19Hapakuwepo vita tena mpaka mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa.