2 Nyakati 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 13:1-22

Abiya Mfalme Wa Yuda

(1 Wafalme 15:1-8)

1Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu, Abiya akawa mfalme wa Yuda, 213:2 2Nya 11:20; 1Fal 15:6naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka, binti Urieli wa Gibea.

Basi kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu. 3Abiya aliingia vitani na jeshi la watu 400,000 wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu 800,000 wenye uwezo.

413:4 Yos 18:22; 1Nya 11:1Abiya akasimama juu ya Mlima Semaraimu, katika nchi ya vilima ya Efraimu, naye akasema, “Yeroboamu na Israeli yote, nisikilizeni mimi! 513:5 2Sam 7:13; 1Nya 17:12; Law 2:13; Hes 18:19; Amu 11:21-24; Eze 43:24; 1Sam 16:13; Za 89:20; Lk 1:31-33Hamfahamu kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi na wazao wake ufalme juu ya Israeli milele kwa Agano la chumvi? 613:6 1Fal 11:26; 12:20; 2Nya 10:19Hata hivyo Yeroboamu mwana wa Nebati afisa wa Solomoni mwana wa Daudi, aliasi dhidi ya bwana wake. 713:7 Amu 9:4; Za 26:4; Mdo 17:5; Mit 12:11Baadhi ya watu wasiofaa kitu, wabaya kabisa walimkusanyikia na kumpinga Rehoboamu mwana wa Solomoni alipokuwa kijana mdogo asiyekuwa na uamuzi, asiye na nguvu za kuweza kupingana nao.

813:8 Za 68:25; 1Nya 25:10-24; 2Nya 29:2513:8 Kut 32:4; 1Fal 12:28; Hos 8:6“Hata sasa unapanga kupingana na ufalme wa Bwana ambao uko mikononi mwa wazao wa Daudi. Kweli ninyi ni jeshi kubwa nanyi mnazo ndama za dhahabu Yeroboamu alizozitengeneza kuwa miungu yenu. 913:9 2Nya 11:14-15; Kut 29:35-36; Gal 4:8; Yer 2:11Lakini je, hamkuwafukuza makuhani wa Bwana, wana wa Aroni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Yeyote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo dume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu.

10“Lakini kwetu sisi, Bwana ndiye Mungu wetu, wala hatujamwacha. Makuhani wanaomtumikia Bwana ni wana wa Aroni, nao Walawi wakiwasaidia. 1113:11 Kut 29:39; 2Nya 2:4; Law 24:2-6; 1Nya 9:24; Kut 27:20-21Kila asubuhi na jioni wao hutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa Bwana. Wao huweka mikate juu ya meza safi kwa taratibu za kiibada na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Sisi tunazishika kanuni za Bwana Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu. 1213:12 Hes 10:8-9; Amu 2:15; Mdo 5:39; Kum 20:4; Yos 5:4; Za 20:7; Ay 15:25-26; Mdo 9:4-5Mungu yu pamoja nasi, yeye ndiye kiongozi wetu. Makuhani wake wakiwa na tarumbeta zao watapiga baragumu ya vita dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane dhidi ya Bwana, Mungu wa baba zenu, kwa maana hamtashinda.”

1313:13 2Nya 20:22; Yos 8:9Basi Yeroboamu alikuwa ametuma jeshi kuzunguka nyuma ya Yuda ili kwamba akiwa mbele ya Yuda, jeshi liwavizie kwa nyuma. 1413:14 1Nya 5:20; 2Nya 18:31Basi Yuda wakageuka na kuona kwamba wanashambuliwa mbele na nyuma. Ndipo wakamlilia Bwana. Makuhani wakapiga tarumbeta zao, 1513:15 2Nya 14:12; Hes 32:4nao watu wa Yuda wakapaza sauti ya kilio cha vita. Katika kupiga kelele za vita, Mungu akawafukuza Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Mfalme Abiya na Yuda. 1613:16 2Nya 16:8Waisraeli wakakimbia mbele ya Yuda, naye Mungu akawatia Israeli mikononi mwao. 17Abiya na watu wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi 500,000 miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli. 1813:18 1Nya 5:20; Za 22:5; Amu 8:28; 2Fal 18:5; 2Nya 16:8-9; 20:20Watu wa Israeli walitiishwa katika tukio lile, nao watu wa Yuda wakawa washindi kwa sababu walimtegemea Bwana, Mungu wa baba zao.

1913:19 Yos 15:9; Yn 11:54Abiya akamfuatia Yeroboamu na kuteka miji ya Betheli, Yeshana na Efroni kutoka kwake, pamoja na vijiji vinavyoizunguka miji hiyo. 2013:20 1Sam 25:38; Eze 24:16; Mdo 12:23; 1Sam 26:10; 1Fal 14:20Yeroboamu hakupata nguvu tena wakati wa utawala wa Abiya. Naye Bwana akampiga Yeroboamu akafa.

21Lakini Abiya akapata nguvu. Alioa wanawake kumi na wanne na alikuwa na wana ishirini na wawili na binti kumi na sita.

2213:22 2Nya 9:29; 12:15Matukio mengine ya utawala wa Abiya, pamoja na mambo aliyofanya na aliyosema, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.