1 Yohana 5 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

1 Yohana 5:1-21

Imani Katika Mwana Wa Mungu Huushinda Ulimwengu

15:1 Yn 3:15; 1Yn 2:22; 2:23; Yn 8:42Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo amezaliwa na Mungu, na yeyote ampendaye Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye. 25:2 1Yn 2:3; 3:14Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake. 35:3 Yn 14:15; Mt 11:30; 23:4Huku ndiko kumpenda Mungu, yaani, kuzitii amri zake. Nazo amri zake si nzito. 45:4 Yn 1:13; 16:33Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu. 55:5 1Yn 2:23Ni nani yule aushindaye ulimwengu? Ni yule tu aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Ushuhuda Kuhusu Mwana Wa Mungu

65:6 Yn 19:34; 14:17Huyu ndiye alikuja kwa maji na damu, yaani, Yesu Kristo. Hakuja kwa maji peke yake, bali kwa maji na damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. 75:7 Mt 18:16Kwa maana wako watatu washuhudiao[ mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho Mtakatifu. Hawa watatu ni umoja. 8Pia wako mashahidi watatu duniani]: Roho, Maji na Damu; hawa watatu wanakubaliana katika umoja. 95:9 Yn 5:34; Mt 3:16, 17; Yn 5:32, 37; 8:15, 18Kama tunaukubali ushuhuda wa wanadamu, basi ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi, kwa kuwa huu ndio ushuhuda wa Mungu kwamba amemshuhudia Mwanawe. 105:10 Rum 8:16; Gal 4:6; Yn 3:33; 1Yn 1:10Kila mtu amwaminiye Mwana wa Mungu anao huu ushuhuda moyoni mwake. Kila mtu asiyemwamini Mungu amemfanya yeye kuwa mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda Mungu alioutoa kuhusu Mwanawe. 115:11 Mt 25:46; Yn 1:4Huu ndio ushuhuda: kwamba Mungu ametupa uzima wa milele, nao huo uzima umo katika Mwanawe. 125:12 Yn 3:15, 16, 36Aliye naye Mwana wa Mungu anao uzima, yeye asiye na Mwana wa Mungu hana uzima.

Maneno Ya Mwisho

135:13 Yn 3:23; 1Yn 5:11; Mt 25:46Nawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu ili mpate kujua ya kuwa mnao uzima wa milele. 145:14 Efe 3:12; 1Yn 3:21; Mt 7:7Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 155:15 1Yn 5:18, 20; 1Fal 3:12Nasi kama tunajua atusikia, lolote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba.

165:16 Yak 5:15; Kut 23:21; Ebr 6:4-6; 10:26; Yer 7:16; 14:11Kama mtu akimwona ndugu yake akitenda dhambi isiyo ya mauti, inampasa aombe, naye Mungu atampa uzima mtu huyo. Ninamaanisha wale ambao dhambi yao si ya mauti. Iko dhambi ya mauti, sisemi kwamba utaomba kwa ajili ya hiyo. 175:17 1Yn 3:4; 5:16; 2:1Jambo lolote lisilo la haki ni dhambi, lakini iko dhambi isiyo ya mauti.

185:18 Yn 1:13; Mt 5:37; 14:30Tunajua ya kuwa yeye aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, bali aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hawezi kumdhuru. 195:19 1Yn 4:6; Yn 12:31; 14:30; 17:15Sisi twajua kuwa tu watoto wa Mungu na ya kwamba ulimwengu wote uko chini ya utawala wa yule mwovu. 205:20 1Yn 5:5; Lk 24:45; Yn 17:3; 1Yn 5:11; Mt 25:46Nasi pia twajua ya kwamba Mwana wa Mungu amekuja, naye ametupa sisi ufahamu ili tupate kumjua yeye aliye Kweli. Nasi tumo ndani yake yeye aliye Kweli, yaani, ndani ya Yesu Kristo Mwanawe. Yeye ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele.

215:21 1Yn 2:1; 1Kor 10:14; 1The 1:9Watoto wapendwa, jilindeni nafsi zenu kutokana na sanamu. Amen.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

约翰一书 5:1-21

胜过世界的人

1凡信耶稣是基督的人,都是从上帝生的。凡爱生他之上帝的,也必爱上帝所生的。 2当我们爱上帝,遵行祂的命令时,便知道自己也爱祂的儿女。 3因为我们遵行上帝的命令就是爱上帝。其实,祂的命令并不难遵守, 4因为凡从上帝生的人都能胜过世界,使我们得胜的是我们的信心。 5谁能胜过世界呢?不就是那些信耶稣是上帝儿子的人吗?

上帝的见证

6耶稣基督是借着水和血来的。祂不是单借着水来的,而是借着水和血来的,并且有圣灵为祂做见证,因为圣灵就是真理。 7这样,做见证的共有三样: 8圣灵、水和血。这三者是一致的。 9我们既然接受人的见证,就更该接受上帝的见证,因为这是上帝为祂儿子做的见证。 10信上帝儿子的人里面有这见证,不信上帝的人把上帝当作了说谎的,因为他不信上帝为祂儿子做的见证。 11这见证就是:上帝已经把永生赐给我们,这生命在祂儿子里面。 12人有上帝的儿子,就有这生命;没有上帝的儿子,就没有这生命。

永恒的生命

13我把这些话写给你们这些信上帝儿子之名的人,是要你们知道自己有永生。 14我们若按着上帝的旨意祈求,祂必垂听,这是我们对祂的信心。 15我们既然知道上帝垂听我们一切的祈求,就知道我们必能得到所求的。

16人若看见信徒犯了不至于死的罪,就当为他祷告,上帝必将生命赐给他,就是那些犯了不至于死之罪的人。有的罪会导致死亡,我并不是说你们要为这样的罪祷告。 17一切不义的事都是罪,但有的罪不会导致死亡。

18我们知道凡从上帝生的不会继续犯罪,因为上帝的儿子保护他,那恶者无法害他。 19我们知道自己属于上帝,全世界都在那恶者手中。

20我们知道上帝的儿子已经来了,并且赐给了我们悟性,使我们能认识真神。我们在真神里面,就是在祂儿子耶稣基督里面。祂是真神,也是永生。

21孩子们啊,你们要远离偶像!