1 Yohana 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Yohana 4:1-21

Zijaribuni Hizo Roho

14:1 Mt 7:15; 1Kor 10:14; Yer 29:9; 1Kor 12:10; 2The 2:2; 1Yn 2:18Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni. 24:2 Yn 1:4; 1Yn 2:23; 1Kor 12:3Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. 34:3 1Yn 2:22; 2Yn 7; 1Yn 2:18Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.

44:4 Rum 8:31; 2Fal 6:16Watoto wapendwa, ninyi mmetokana na Mungu, nanyi mmewashinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu. 54:5 Yn 17:14, 16Wao wanatokana na ulimwengu na kwa hiyo hunena yaliyo ya ulimwengu, hivyo ulimwengu huwasikiliza. 64:6 Yn 8:47; 14:17Sisi twatokana na Mungu na yeyote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.

Mungu Ni Pendo

74:7 1Yn 3:11; 2:4Wapendwa, tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 84:8 1Yn 4:7, 16; 2:4; 3:6Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo. 94:9 Yn 3:16; 17; 1Yn 5:11Hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake. 104:10 Rum 5:8, 10; 1Yn 2:2Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu. 114:11 Yak 3:16; 1Yn 2:25; Yn 1:4; 1Yn 4:9Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana. 124:12 Yn 1:18; 1Tim 6:16Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.

134:13 1Yn 3:24; 2:3Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa sisi sehemu ya Roho wake. 144:14 Yn 15:27; Lk 2:10Nasi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanawe ili awe Mwokozi wa ulimwengu. 154:15 1Yn 5:5; Rum 10:9Kila akiriye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, basi Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu. 164:16 1Yn 4:8, 12, 13; 3:24Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu.

Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 174:17 1Yn 4:12; 2:5; Efe 3:12; Mt 10:15Kwa njia hii, pendo hukamilishwa miongoni mwetu ili tupate kuwa na ujasiri katika siku ya hukumu, kwa sababu kama alivyo ndivyo tulivyo sisi katika ulimwengu huu. 184:18 Rum 8:15; 1Yn 4:12Katika pendo hakuna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika pendo.

194:19 1Yn 4:10Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 204:20 1Yn 2:9; 3:17; Yn 1:18Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemuona? 21Naye ametupa amri hii: Yeyote anayempenda Mungu lazima pia ampende ndugu yake.