1 Yohana 2 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Yohana 2:1-29

Kristo Mwombezi Wetu

12:1 1The 2:11; Ebr 7:25; 1Tim 2:5Watoto wangu wapendwa, nawaandikia haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba: ndiye Yesu Kristo, Mwenye Haki. 22:2 1Yn 4:10; Rum 3:25; Mt 1:21; Yn 3:17Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.

32:3 Yn 14:15; 1Yn 2:5; 3:24; 4:13; 5:2; 2:4Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake. 42:4 1Yn 1:6, 8; 2:3; Tit 1:16; 1Yn 3:6; 4:7, 8Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. 52:5 Yn 14:15, 21, 23; 1Yn 4:12Lakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake. 62:6 Mt 11:29; 2Pet 2:21Yeyote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Yesu alivyoenenda.

Amri Mpya

72:7 1Kor 10:14; 1Yn 2:24; 3:11, 23; 4:2Wapendwa, siwaandikii ninyi amri mpya bali ile ya zamani, ambayo mmekuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilosikia. 82:8 Yn 13:34; Ebr 10:25; Yn 1:9; Efe 5:8; 1The 5:5Lakini nawaandikia amri mpya, yaani, lile neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya kweli tayari inangʼaa.

92:9 1Yn 2:11; Law 19:17; 1Yn 3:10; 4:20, 21; 1:5Yeyote anayesema yumo nuruni lakini anamchukia ndugu yake bado yuko gizani. 102:10 1Yn 3:14; 2:11; Za 119:165; Rum 14:13, 15; Yn 11:9Yeye ampendaye ndugu yake anakaa nuruni, wala hakuna kitu chochote ndani yake cha kumkwaza. 112:11 Yn 11:9; 11:10; 12:35; 1Yn 1:6; Yn 12:35Lakini yeyote amchukiaye ndugu yake, yuko gizani na anaenenda gizani, wala hajui anakokwenda, kwa sababu giza limempofusha macho.

122:12 1Yn 2:9; 3:23Nawaandikia ninyi, watoto wadogo,

kwa sababu dhambi zenu

zimesamehewa kwa ajili ya Jina lake.

132:13 Mt 5:37; Yn 1:1; 16:33; 1Yn 2:14; 2:13Nawaandikia ninyi, akina baba,

kwa sababu mmemjua

yeye aliye tangu mwanzo.

Nawaandikia ninyi vijana

kwa sababu mmemshinda yule mwovu.

Nawaandikia ninyi watoto wadogo,

kwa sababu mmemjua Baba.

142:14 Efe 6:10; Yn 5:38; 1Yn 1:10Nawaandikia ninyi akina baba,

kwa sababu mmemjua

yeye aliye tangu mwanzo.

Nawaandikia ninyi vijana,

kwa sababu mna nguvu,

na neno la Mungu linakaa ndani yenu,

nanyi mmemshinda yule mwovu.

Msiupende Ulimwengu

152:15 Rum 12:2; Yak 4:4Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Kama mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake. 162:16 Efe 2:8; Mit 27:20Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu. 172:17 Ebr 12:27; Mt 12:50; 1Kor 7:31; Yak 1:10; 4:14; 1Pet 1:24Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.

Onyo Dhidi Ya Wapinga Kristo

182:18 1Yn 4:1; 2Yn 7Watoto wadogo, huu ni wakati wa mwisho! Kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo anakuja, hivyo basi wapinga Kristo wengi wamekwisha kuja. Kutokana na hili twajua kwamba huu ni wakati wa mwisho. 192:19 Mk 1:24; Yer 31:34Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa. Kwa maana kama wangelikuwa wa kwetu, wangelikaa pamoja nasi, lakini kutoka kwao kulionyesha kwamba hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kwetu.

202:20 1Yn 2:27; 2Kor 1:21; Mk 1:24; Yer 31:34; Mt 13:11; Yn 14:26Lakini ninyi mmetiwa mafuta na yeye Aliye Mtakatifu, nanyi nyote mnaijua kweli. 212:21 2Pet 1:12; Yud 5Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo utokao katika kweli. 222:22 1Yn 4:13; 2Yn 7Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo, yaani, yeye humkana Baba na Mwana. 232:23 Yn 14:7; 2Yn 9Hakuna yeyote amkanaye Mwana aliye na Baba. Yeyote anayemkubali Mwana anaye na Baba pia.

242:24 2Yn 9Hakikisheni kwamba lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu. Kama lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 252:25 Mt 25:46; Yn 17:3; 1Yn 1:2; 5:11Hii ndiyo ahadi yake kwetu, yaani, uzima wa milele.

262:26 1Yn 3:7; 2Yn 7Nawaandikia mambo haya kuhusu wale watu ambao wanajaribu kuwapotosha. 272:27 1Yn 2:20; Yer 31:33, 34; Ebr 8:10, 11; Yn 14:26; 16:13Nanyi, upako mlioupata kutoka kwake unakaa ndani yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu yeyote kuwafundisha. Lakini kama vile upako wake unavyowafundisha kuhusu mambo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi kama ulivyowafundisha kaeni ndani yake.

Watoto Wa Mungu

282:28 Kol 3:4; 1Yn 3:2; Efe 3:12; 1The 2:19Sasa basi, watoto wapendwa, kaeni ndani yake, ili atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake wakati wa kuja kwake.

292:29 1Yn 3:7; Mdo 22:14; Yn 1:13Kama mkijua kuwa yeye ni mwenye haki, mwajua kwamba kila atendaye haki amezaliwa naye.

King James Version

1 John 2:1-29

1My little children, these things write I unto you, that ye sin not. And if any man sin, we have an advocate with the Father, Jesus Christ the righteous: 2And he is the propitiation for our sins: and not for ours only, but also for the sins of the whole world. 3And hereby we do know that we know him, if we keep his commandments. 4He that saith, I know him, and keepeth not his commandments, is a liar, and the truth is not in him. 5But whoso keepeth his word, in him verily is the love of God perfected: hereby know we that we are in him. 6He that saith he abideth in him ought himself also so to walk, even as he walked.

7Brethren, I write no new commandment unto you, but an old commandment which ye had from the beginning. The old commandment is the word which ye have heard from the beginning. 8Again, a new commandment I write unto you, which thing is true in him and in you: because the darkness is past, and the true light now shineth. 9He that saith he is in the light, and hateth his brother, is in darkness even until now. 10He that loveth his brother abideth in the light, and there is none occasion of stumbling in him. 11But he that hateth his brother is in darkness, and walketh in darkness, and knoweth not whither he goeth, because that darkness hath blinded his eyes. 12I write unto you, little children, because your sins are forgiven you for his name’s sake. 13I write unto you, fathers, because ye have known him that is from the beginning. I write unto you, young men, because ye have overcome the wicked one. I write unto you, little children, because ye have known the Father. 14I have written unto you, fathers, because ye have known him that is from the beginning. I have written unto you, young men, because ye are strong, and the word of God abideth in you, and ye have overcome the wicked one. 15Love not the world, neither the things that are in the world. If any man love the world, the love of the Father is not in him. 16For all that is in the world, the lust of the flesh, and the lust of the eyes, and the pride of life, is not of the Father, but is of the world. 17And the world passeth away, and the lust thereof: but he that doeth the will of God abideth for ever.

18Little children, it is the last time: and as ye have heard that antichrist shall come, even now are there many antichrists; whereby we know that it is the last time. 19They went out from us, but they were not of us; for if they had been of us, they would no doubt have continued with us: but they went out, that they might be made manifest that they were not all of us. 20But ye have an unction from the Holy One, and ye know all things. 21I have not written unto you because ye know not the truth, but because ye know it, and that no lie is of the truth. 22Who is a liar but he that denieth that Jesus is the Christ? He is antichrist, that denieth the Father and the Son. 23Whosoever denieth the Son, the same hath not the Father: (but) he that acknowledgeth the Son hath the Father also. 24Let that therefore abide in you, which ye have heard from the beginning. If that which ye have heard from the beginning shall remain in you, ye also shall continue in the Son, and in the Father. 25And this is the promise that he hath promised us, even eternal life. 26These things have I written unto you concerning them that seduce you. 27But the anointing which ye have received of him abideth in you, and ye need not that any man teach you: but as the same anointing teacheth you of all things, and is truth, and is no lie, and even as it hath taught you, ye shall abide in him. 28And now, little children, abide in him; that, when he shall appear, we may have confidence, and not be ashamed before him at his coming. 29If ye know that he is righteous, ye know that every one that doeth righteousness is born of him.