1 Yohana 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Yohana 1:1-10

Neno La Uzima

11:1 Yn 1:2; 2Pet 1:16; Yn 20:27Tunawajulisha lile lililokuwepo tangu mwanzo, lile tulilosikia, ambalo tumeliona kwa macho yetu, ambalo tumelitazama na kuligusa kwa mikono yetu, kuhusu Neno la uzima. 21:2 Yn 14:6; 1Pet 1:20Uzima huo ulidhihirishwa; nasi tumeuona na kuushuhudia, nasi twawatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa pamoja na Baba, nao ukadhihirishwa kwetu. 31:3 1Kor 1:9; 1Yn 1:1; Mdo 4:20; Yn 17:21; 1Yn 2:24Twawatangazia lile tuliloliona na kulisikia, ili nanyi mwe na ushirika nasi. Na ushirika wetu hasa ni pamoja na Baba na Mwanawe, Yesu Kristo. 4Tunaandika mambo haya ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.

Kutembea Nuruni

51:5 1Yn 3:11; 2Yn 12Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote. 61:6 Efe 5:8; 1Yn 4:20Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli. 71:7 Ufu 7:14; Ebr 9:14; Ufu 1:5Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

81:8 Yer 2:35; Yn 8:44Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. 91:9 Mit 28; 13; Za 32:5; 51:2; Mit 28:13; 1Yn 1:7; Mik 7:18-20; Ebr 10:22Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote. 101:10 1Yn 5:10; Yn 5:38; 1Yn 1:8; 5:10; Yn 5:38; 2:15Kama tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo na neno lake halimo ndani yetu.