1 Wathesalonike 5 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Wathesalonike 5:1-28

Kuweni Tayari Kwa Siku Ya Bwana

15:1 Mdo 1:7; 1The 4:9Basi, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira hatuna haja ya kuwaandikia, 25:2 1Kor 1:8; 2Pet 3:10kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajapo usiku. 35:3 Yer 6:14; Yn 16:21, 22; Mt 24:39; Lk 21:34, 35Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka.

45:4 Mdo 26:18; 1Yn 2:8Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi. 55:5 Rum 13:12; Efe 5:9Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku. 65:6 Rum 13:11Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine walalavyo, bali tukeshe na kuwa na kiasi. 75:7 Lk 21:34, 36; Rum 13:13; 1Kor 15:34Kwa kuwa wote walalao hulala usiku na wale walewao hulewa usiku. 85:8 Isa 59:17; Efe 6:14, 16, 17Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo. 95:9 2The 2:13-14Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. 105:10 2Kor 5:15Yeye alikufa kwa ajili yetu ili hata kama tuko macho au tumelala, tupate kuishi pamoja naye. 115:11 1The 4:18Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.

Maagizo Ya Mwisho, Salamu Na Kuwatakia Heri

125:12 1Tim 5:17; Ebr 13:17Sasa tunawaomba, ndugu, waheshimuni wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu, wale ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana na ambao wanawaonya. 135:13 Mk 9:50; 2The 3:6-11; Rum 14:1Waheshimuni sana katika upendo kwa ajili ya kazi zao. Ishini kwa amani ninyi kwa ninyi. 145:14 2The 3:11, 12; Ebr 12:12; Rum 4:1; 15:1Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote. 155:15 1Pet 3:9; Gal 6:10; Efe 4:32Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

165:16 2Kor 6:10; Flp 4:4Furahini siku zote; 175:17 Lk 18:1; 21:36; Rum 12:12; Efe 6:18; Kol 4:12ombeni bila kukoma; 185:18 Efe 5:20; Kol 3:17shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.

195:19 Efe 4:30Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu; 205:20 1Kor 14:1-40msiyadharau maneno ya unabii. 215:21 1Kor 14:29; 1Yn 4:1Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema. 225:22 1The 4:12Jiepusheni na uovu wa kila namna.

235:23 Rum 15:33; Ebr 4:12; 1The 3:13; 2:19Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. 245:24 Rum 8:28; 1Kor 1:9; Hes 23:19; Flp 1:6Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo.

255:25 Kol 4:3; 2The 3:1; Ebr 13:18; Efe 6:9Ndugu, tuombeeni. 26Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu. 27Nawaagizeni mbele za Bwana mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii.

28Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. Amen.