1 Wakorintho 9 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Wakorintho 9:1-27

Haki Za Mtume

19:1 1Kor 1:1; 2Kor 12:12; 1Kor 15:8; 3:6; 4:15Je, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana? 29:2 2Kor 3:2-3; 1Kor 12:12Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni mhuri wa utume wangu katika Bwana.

3Huu ndio utetezi wangu kwa hao wanaokaa kunihukumu. 49:4 Mdo 18:3; Lk 10:8; 1Kor 9:14Je, hatuna haki ya kula na kunywa? 59:5 1Kor 7:7-8; Mt 12:46; 1Kor 1:12Je, hatuna haki ya kusafiri na mke anayeamini, kama wanavyofanya mitume wengine na ndugu zake Bwana na Kefa?9:5 Yaani Petro. 69:6 Mdo 4:36; 2The 3:8, 9Au ni mimi na Barnaba tu inatubidi kufanya kazi ili tuweze kupata mahitaji yetu?

79:7 2Tim 2:3-4; Kum 20:6; Mit 27:18; 1Kor 3:6-8Ni askari yupi aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye shamba la mizabibu na asile matunda yake? Ni nani achungaye kundi na asipate maziwa yake. 8Je, nasema mambo haya katika mtazamo wa kibinadamu tu? Je, sheria haisemi vivyo hivyo? 99:9 Kum 25:4; 1Tim 5:18; Kum 22:1-4; Mit 12:10Kwa maana imeandikwa katika Sheria ya Mose: “Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka.” Je, Mungu hapa anahusika na ngʼombe? 109:10 Rum 4:23-24; Mit 11:25; 2Tim 2:6Je, Mungu hasemi haya hasa kwa ajili yetu? Hakika yameandikwa kwa ajili yetu, kwa sababu mtu anapolima na mpuraji akapura nafaka, wote wanapaswa kufanya hivyo wakiwa na tumaini la kushiriki mavuno. 119:11 Rum 15:27; Gal 6:6Je, ikiwa sisi tulipanda mbegu ya kiroho miongoni mwenu, itakuwa ni jambo kubwa iwapo tutavuna vitu vya mwili kutoka kwenu? 129:12 Mdo 18:3; 2Kor 6:3; 11:7-12Kama wengine wana haki ya kupata msaada kutoka kwenu, isingepasa tuwe na haki hiyo hata zaidi?

Lakini sisi hatukutumia haki hii. Kinyume chake, tunavumilia kila kitu ili tusije tukazuia Injili ya Kristo. 139:13 Law 6:16-26; Kum 18:1Je, hamjui kwamba, watu wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni, nao wale wahudumiao madhabahuni hushiriki kile kitolewacho madhabahuni? 149:14 1Tim 5:18; Mt 10:10; Lk 10:7; Gal 6:6; 1Tim 5:17Vivyo hivyo, Bwana ameamuru kwamba wale wanaohubiri Injili wapate riziki yao kutokana na Injili.

159:15 Mdo 18:3; 2Kor 11:9-10Lakini sijatumia hata mojawapo ya haki hizi. Nami siandiki haya nikitumaini kwamba mtanifanyia mambo hayo. Heri nife kuliko mtu yeyote kuninyima huku kujisifu kwangu. 169:16 Rum 1:14; Mdo 9:15; 26:15-18Lakini ninapohubiri Injili siwezi kujisifu maana ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipoihubiri Injili! 179:17 1Kor 3:8-14; 4:1; Gal 2:7; Kol 1:25Nikihubiri kwa hiari, ninayo thawabu. Lakini kama si kwa hiari, basi ninachofanya ni kutekeleza tu uwakili niliowekewa. 189:18 2Kor 11:7; 12:13; 1Kor 10:33; 2Kor 4:5; 1Kor 7:31Basi je, thawabu yangu ni nini? Thawabu yangu ni hii: Ya kwamba katika kuhubiri Injili niitoe bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.

199:19 2Kor 4:5; Gal 5:13; Mt 18:15; 1Pet 3:1Ingawa mimi ni huru, wala si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya kuwa mtumwa wa kila mtu, ili niweze kuwavuta wengi kadri iwezekanavyo. 209:20 Mdo 16:3; 21:20-26; Rum 11:14; 2:12Kwa Wayahudi, nilikuwa kama Myahudi, ili niwapate Wayahudi. Kwa watu wale walio chini ya sheria, nilikuwa kama aliye chini ya sheria (ingawa mimi siko chini ya sheria), ili niweze kuwapata wale walio chini ya sheria. 219:21 Rum 2:12-14; Gal 6:2Kwa watu wasio na sheria nilikuwa kama asiye na sheria (ingawa siko huru mbali na sheria ya Mungu, bali niko chini ya sheria ya Kristo), ili niweze kuwapata wale wasio na sheria. 229:22 Rum 14:1; 1Kor 2:3; 10:33; Rum 11:14Kwa walio dhaifu nilikuwa dhaifu, ili niweze kuwapata walio dhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yoyote niweze kuwaokoa baadhi yao. 23Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nipate kushiriki baraka zake.

249:24 Flp 3:14; Kol 2:18; Gal 2:2; 5:7; Flp 2:16; 2Tim 4:7; Ebr 12:1Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa jinsi ambavyo mtapata tuzo.

259:25 2Tim 2:5; 4:8; Yak 1:12; 1Pet 5:4; Ufu 2:10; 3:11Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji isiyodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji idumuyo milele. 269:26 1Tim 6:12; 2Kor 2:5; 1Kor 9:24Kwa hiyo mimi sikimbii kama mtu akimbiaye bila lengo, sipigani kama mtu anayepiga hewa, 279:27 Rum 8:12; 8:13; Kol 3:5; Rum 6:18-19; Yer 6:30; 2Kor 13:5, 6; Lk 10:7la, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha ili nikiisha kuwahubiria wengine, mimi nisiwe mtu wa kukataliwa.