1 Wakorintho 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Wakorintho 6:1-20

Kushtakiana Miongoni Mwa Waumini

16:1 Mt 18:7Kama mtu yeyote wa kwenu ana ugomvi na mwenzake, anathubutuje kuupeleka kwa wasiomcha Mungu ili kuamuliwa badala ya kuupeleka kwa watakatifu? 26:2 Mt 19:28; Lk 22:30; 1Kor 5:12Je, hamjui kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Nanyi kama mtauhukumu ulimwengu, je, hamwezi kuamua mambo madogo madogo? 36:3 1Kor 4:14; Mdo 1:15Hamjui kwamba tutawahukumu malaika? Je, si zaidi mambo ya maisha haya? 46:4 1Kor 5:12Kwa hiyo kama kuna ugomvi miongoni mwenu kuhusu mambo kama haya, chagueni kuwa waamuzi, watu ambao wanaonekana hata sio wa heshima katika kanisa. 56:5 1Kor 4:14; Mdo 1:15Nasema hivi ili mwone aibu. Je, inawezekana kuwa miongoni mwenu hakuna mtu mwenye hekima ya kutosha kuamua ugomvi kati ya waaminio? 66:6 Rum 7:1; 2Kor 6:14-15; 1Tim 5:8Badala yake ndugu mmoja anampeleka mwenzake mahakamani, tena mbele ya watu wasioamini!

76:7 Mt 5:39-40; 1The 5:15; 1Pet 3:9Huko kuwa na mashtaka miongoni mwenu ina maana kwamba tayari ni kushindwa kabisa. Kwa nini msikubali kutendewa mabaya? Kwa nini msikubali kunyangʼanywa? 86:8 1The 4:6; Kum 17:7; 19; 19; 21:21; 22:21, 24; 24:7Badala yake, ninyi wenyewe mwadanganya na kutenda mabaya, tena mwawatendea ndugu zenu.

96:9 Mt 25:34; Ay 13:9; 1Kor 15:33; Gal 6:7; Yak 1:16; Law 18:20; Kum 22:22; Law 18:22Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti, 106:10 1Tim 1:10; Ufu 21:8; 22:15wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyangʼanyi hawataurithi Ufalme wa Mungu. 116:11 Efe 2:2; Mdo 22:16; 1Kor 1:2; Rum 12:1Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.

Dhambi Za Zinaa

126:12 1Kor 10:23“Vitu vyote ni halali kwangu”: lakini si vitu vyote vyenye faida. “Vitu vyote ni halali kwangu”: lakini sitatawaliwa na kitu chochote. 136:13 Kol 2:22; Rum 12:1“Chakula ni cha tumbo, na tumbo ni la chakula”: lakini Mungu ataviangamiza vyote viwili. Mwili haukuumbwa kwa ajili ya zinaa bali kwa ajili ya Bwana na Bwana kwa ajili ya mwili. 146:14 Mdo 2:24; Rum 6:5; Efe 1:19-20; 1The 4:16Naye Mungu aliyemfufua Bwana kutoka kwa wafu atatufufua sisi pia kwa uweza wake. 156:15 Rum 12:5Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya Kristo mwenyewe? Je, nichukue viungo vya mwili wa Kristo na kuviunganisha na mwili wa kahaba? La hasha! 166:16 Mwa 2:24; Mt 19:5; Efe 5:31Hamjui kwamba aliyeungwa na kahaba anakuwa mwili mmoja naye? Kwa kuwa imenenwa, “Hao wawili watakuwa mwili mmoja.” 176:17 Yn 17:21-23; Rum 8:8-11; Gal 2:20Lakini mtu aliyeungwa na Bwana anakuwa roho moja naye.

186:18 1Kor 5:1; 2Kor 12:21; Gal 5:19; Efe 5:3; 1The 4:3-4; Ebr 13:4; Rum 6:12Ikimbieni zinaa. Dhambi zingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe. 196:19 Yn 2:21; Rum 14:7-8Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe, 206:20 Za 74:2; Mt 20:28; Mdo 20:28; 1Kor 7:23; Ufu 5:9; 14:4; Flp 1:20kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.