1 Wakorintho 16 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wakorintho 16:1-24

Changizo Kwa Ajili Ya Watakatifu

116:1 Mdo 24:17; 9:13; 16:6Basi kuhusu changizo kwa ajili ya watakatifu: Kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia, fanyeni vivyo hivyo. 216:2 Mdo 20:7; 2Kor 9:4-5Siku ya kwanza ya kila juma, kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha, kulingana na mapato yake na fedha hizo aziweke akiba, ili nitakapokuja pasiwe na lazima ya kufanya mchango. 316:3 2Kor 3:1; 8:18-19Kwa hiyo nitakapowasili, nitawapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili kuwatuma wapeleke zawadi zenu huko Yerusalemu. 416:4 2Kor 8:4, 19Kama ikionekana ni vyema na mimi niende, basi hao watu watafuatana nami.

Mahitaji Binafsi

516:5 1Kor 4:19; Mdo 16:9Baada ya kupitia Makedonia nitakuja kwenu, maana ninakusudia kupitia Makedonia. 616:6 Rum 15:24; Tit 3:13Huenda nitakaa nanyi kwa muda, au hata kukaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili mweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendapo. 716:7 Mdo 18:21Kwa maana sitaki niwaone sasa na kupita tu; natarajia kuwa nanyi kwa muda wa kutosha, kama Bwana akipenda. 816:8 Mdo 18:19; 2:1Lakini nitakaa Efeso mpaka wakati wa Pentekoste, 916:9 Mdo 14:27; 2Kor 2:12; Kol 4:3; Ufu 3:8; Mdo 19:9kwa maana mlango mkubwa umefunguliwa kwangu kufanya kazi yenye matunda, nako huko kuna adui wengi wanaonipinga.

1016:10 Mdo 16:1; 19:22; Rum 16:21; Flp 2:20, 22; 1The 3:2Ikiwa Timotheo atakuja kwenu, hakikisheni kwamba hana hofu yoyote akiwa nanyi, kwa sababu anafanya kazi ya Bwana, kama mimi nifanyavyo. 1116:11 1Tim 4:12; 2Kor 1:16; 3Yn 6; Mdo 19:9Basi asiwepo mtu atakayekataa kumpokea. Msafirisheni kwa amani ili aweze kunijia tena. Namtarajia pamoja na ndugu.

1216:12 Mdo 18:24; 1Kor 1:12Basi kwa habari za ndugu yetu Apolo, nimemsihi kwa bidii aje kwenu pamoja na hao ndugu. Ingawa alikuwa hapendi kabisa kuja sasa, lakini atakuja apatapo nafasi.

Maneno Ya Mwisho

1316:13 1Kor 1:8; 2Kor 1:21; Gal 5:1; Flp 1:27; 1The 3:8; Tit 1:9; Efe 6:10Kesheni, simameni imara katika imani, fanyeni kiume, kuweni mashujaa kuweni hodari. 1416:14 1Kor 14:1Fanyeni kila kitu katika upendo.

1516:15 1Kor 1:6; Rum 16:5; Mdo 18; 12; 24; 17; 9:13Ninyi mnajua kwamba watu wa nyumbani mwa Stefana ndio waliokuwa wa kwanza kuamini katika Akaya, nao wamejitoa kwa ajili ya kuwahudumia watakatifu. Ndugu nawasihi, 1616:16 1The 5:12; Ebr 13:17mjitie katika kuwahudumia watu kama hawa na kila mmoja aingiaye kwenye kazi na kuifanya kwa bidii. 1716:17 2Kor 11:9; Flp 2:30Nilifurahi wakati Stefana, Fortunato na Akaiko walipofika, kwa sababu wamenipatia yale niliyopungukiwa kutoka kwenu. 1816:18 Rum 15:32; Flp 1:7; 2:29Kwa kuwa waliiburudisha roho yangu na zenu pia. Watu kama hawa wanastahili kutambuliwa.

Salamu Za Mwisho

1916:19 Mdo 2:9; 18:2; Rum 16:5Makanisa ya Asia yanawasalimu. Akila na Prisila,16:19 Prisila kwa Kiyunani ni Priska, hivyo tafsiri nyingine zimemuita Priska. pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao wanawasalimu sana katika Bwana. 2016:20 Rum 16:16; 2Kor 13:12; 1Pet 5:14Ndugu wote walioko hapa wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.

2116:21 Gal 6:11; Kol 4:18; 2The 3:17Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe.

2216:22 Efe 6:24; Rum 9:3; Ufu 22:20Kama mtu yeyote hampendi Bwana Yesu Kristo, na alaaniwe. Bwana wetu, njoo.16:22 Kwa Kiaramu ni Marana tha.

2316:23 Rum 16:20Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.

24Upendo wangu uwe nanyi nyote katika Kristo Yesu. Amen.