1 Wakorintho 14 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version

1 Wakorintho 14:1-40

Karama Za Unabii Na Lugha

114:1 1Kor 16:14; 12:31; Efe 4:11Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii. 214:2 Mk 16:17; 1Kor 13:2Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho. 314:3 Rum 14:19; 1Kor 14:31; 14:4, 5, 12Lakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji. 414:4 Mk 16:17; 1Kor 13:2Anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa. 514:5 Hes 11:29; 1Kor 1:3Ningependa kila mmoja wenu anene kwa lugha lakini ningependa zaidi nyote mtoe unabii. Kwa kuwa yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha, isipokuwa atafsiri, ili kanisa lipate kujengwa.

614:6 Efe 1:17; 2Kor 8:7; Rum 6:17Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho? 7Hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti, kama vile filimbi au kinubi, mtu atajuaje ni wimbo gani unaoimbwa kusipokuwa na tofauti ya upigaji? 814:8 Hes 10:9; Yer 4:19Tena kama tarumbeta haitoi sauti inayoeleweka, ni nani atakayejiandaa kwa ajili ya vita? 9Vivyo hivyo na ninyi, kama mkinena maneno yasiyoeleweka katika akili, mtu atajuaje mnalosema? Kwa maana mtakuwa mnasema hewani tu. 10Bila shaka ziko sauti nyingi ulimwenguni, wala hakuna isiyo na maana. 1114:11 Mwa 11:7Basi kama sielewi maana ya hiyo sauti, nitakuwa mgeni kwa yule msemaji, naye atakuwa mgeni kwangu. 1214:12 1Kor 12:1Vivyo hivyo na ninyi. Kwa kuwa mnatamani kuwa na karama za rohoni, jitahidini kuzidi sana katika karama kwa ajili ya kulijenga kanisa.

1314:13 1Kor 14:2Kwa sababu hii, yeye anenaye kwa lugha na aombe kwamba apate kutafsiri kile anachonena. 1414:14 1Kor 14:2Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu inaomba, lakini akili yangu haina matunda. 1514:15 Efe 5:19; Kol 3:16Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho, na pia nitaomba kwa akili yangu. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia. 1614:16 Kum 27:15-26; 1Nya 16:36; Neh 8:6; Za 106:48; Ufu 5:14; 7:12; Mt 14:19; 1Kor 11:24Ikiwa unabariki kwa roho, mtu mwingine atakayejikuta miongoni mwa hao wasiojua, atawezaje kusema “Amen” katika kushukuru kwako, wakati haelewi unachosema? 1714:17 1Kor 14:3Mnaweza kuwa mnatoa shukrani kweli, sawa, lakini huyo mtu mwingine hajengeki.

18Namshukuru Mungu kwamba mimi nanena kwa lugha kuliko ninyi nyote. 1914:19 1Kor 14:6Lakini ndani ya kanisa ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno 10,000 kwa lugha.

2014:20 1Kor 3:11; Efe 4:14; Ebr 5:12-13; 1Pet 2:2; Yer 4:22; Mt 10:16; Rum 16:19Ndugu zangu, msiwe kama watoto katika kufikiri kwenu, afadhali kuhusu uovu mwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri kwenu, mwe watu wazima. 2114:21 Yn 10:34; Kum 28:49; Isa 28:11-12Katika Sheria imeandikwa kwamba:

“Kupitia kwa watu wenye lugha ngʼeni

na kupitia midomo ya wageni,

nitasema na watu hawa,

lakini hata hivyo hawatanisikiliza,”

asema Bwana.

2214:22 1Kor 14:1Basi kunena kwa lugha ni ishara, si kwa watu waaminio, bali kwa wasioamini, wakati unabii si kwa ajili ya wasioamini, bali kwa ajili ya waaminio. 2314:23 Mdo 2:13Kwa hiyo kama kanisa lote likikutana na kila mmoja akanena kwa lugha, kisha wakaingia wageni wasioelewa wasioamini, je, hawatasema kwamba wote mna wazimu? 2414:24 Mdo 4:13Lakini kama mtu asiyeamini au asiyeelewa akiingia wakati kila mtu anatoa unabii, ataaminishwa na watu wote kuwa yeye ni mwenye dhambi na kuhukumiwa na wote, 2514:25 Rum 2:16; Zek 8:23; Isa 45:14nazo siri za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akikiri, “Kweli Mungu yuko katikati yenu!”

Kumwabudu Mungu Kwa Utaratibu

2614:26 Kum 7:1; 1Kor 12:7-10; Efe 5:19; Rum 14:19Basi tuseme nini ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana wimbo, au neno la mafundisho, au ufunuo, lugha mpya au atatafsiri. Mambo yote yatendeke kwa ajili ya kulijenga kanisa. 27Kama mtu yeyote akinena kwa lugha, basi waseme watu wawili au watatu si zaidi, mmoja baada ya mwingine na lazima awepo mtu wa kutafsiri. 28Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya kanisani na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu.

2914:29 1Kor 13:2; 12:10Manabii wawili au watatu wanene na wengine wapime yale yasemwayo. 3014:30 1The 5:19, 20Kama mtu yeyote aliyeketi karibu, akipata ufunuo, basi yule wa kwanza na anyamaze. 31Kwa maana wote mnaweza kutoa unabii, mmoja baada ya mwingine, ili kila mtu apate kufundishwa na kutiwa moyo. 3214:32 1Yn 4:1Roho za manabii huwatii manabii. 3314:33 Rum 15:33; 1Kor 7:17; 10:32; Mdo 9:13Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani.

Kama ilivyo katika makusanyiko yote ya watakatifu, 3414:34 1Kor 11:5, 13; Efe 5:22; 1Tim 2:11-12wanawake wanapaswa kuwa kimya kanisani. Hawaruhusiwi kusema, bali wanyenyekee kama sheria isemavyo. 3514:35 1Tim 2:11-12; Mwa 3:16Kama wakitaka kuuliza kuhusu jambo lolote, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza kanisani.

3614:36 Ebr 4:12Je, neno la Mungu lilianzia kwenu? Au ni ninyi tu ambao neno la Mungu limewafikia? 3714:37 Mdo 11:27; 1Kor 13:2; 2Kor 10:7; 1Kor 2:15; 1Yn 4:6Kama mtu yeyote akidhani kwamba yeye ni nabii, au ana karama za rohoni, basi na akubali kwamba haya ninayoandika ni maagizo kutoka kwa Bwana. 38Kama mtu akipuuza jambo hili yeye mwenyewe atapuuzwa.

3914:39 1Kor 12:31; Efe 4:11Kwa hiyo ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii na msikataze watu kusema kwa lugha. 4014:40 Kol 2:5Lakini kila kitu kitendeke kwa heshima na kwa utaratibu.

New International Version

1 Corinthians 14:1-40

Intelligibility in Worship

1Follow the way of love and eagerly desire gifts of the Spirit, especially prophecy. 2For anyone who speaks in a tongue14:2 Or in another language; also in verses 4, 13, 14, 19, 26 and 27 does not speak to people but to God. Indeed, no one understands them; they utter mysteries by the Spirit. 3But the one who prophesies speaks to people for their strengthening, encouraging and comfort. 4Anyone who speaks in a tongue edifies themselves, but the one who prophesies edifies the church. 5I would like every one of you to speak in tongues,14:5 Or in other languages; also in verses 6, 18, 22, 23 and 39 but I would rather have you prophesy. The one who prophesies is greater than the one who speaks in tongues,14:5 Or in other languages; also in verses 6, 18, 22, 23 and 39 unless someone interprets, so that the church may be edified.

6Now, brothers and sisters, if I come to you and speak in tongues, what good will I be to you, unless I bring you some revelation or knowledge or prophecy or word of instruction? 7Even in the case of lifeless things that make sounds, such as the pipe or harp, how will anyone know what tune is being played unless there is a distinction in the notes? 8Again, if the trumpet does not sound a clear call, who will get ready for battle? 9So it is with you. Unless you speak intelligible words with your tongue, how will anyone know what you are saying? You will just be speaking into the air. 10Undoubtedly there are all sorts of languages in the world, yet none of them is without meaning. 11If then I do not grasp the meaning of what someone is saying, I am a foreigner to the speaker, and the speaker is a foreigner to me. 12So it is with you. Since you are eager for gifts of the Spirit, try to excel in those that build up the church.

13For this reason the one who speaks in a tongue should pray that they may interpret what they say. 14For if I pray in a tongue, my spirit prays, but my mind is unfruitful. 15So what shall I do? I will pray with my spirit, but I will also pray with my understanding; I will sing with my spirit, but I will also sing with my understanding. 16Otherwise when you are praising God in the Spirit, how can someone else, who is now put in the position of an inquirer,14:16 The Greek word for inquirer is a technical term for someone not fully initiated into a religion; also in verses 23 and 24. say “Amen” to your thanksgiving, since they do not know what you are saying? 17You are giving thanks well enough, but no one else is edified.

18I thank God that I speak in tongues more than all of you. 19But in the church I would rather speak five intelligible words to instruct others than ten thousand words in a tongue.

20Brothers and sisters, stop thinking like children. In regard to evil be infants, but in your thinking be adults. 21In the Law it is written:

“With other tongues

and through the lips of foreigners

I will speak to this people,

but even then they will not listen to me,

says the Lord.”14:21 Isaiah 28:11,12

22Tongues, then, are a sign, not for believers but for unbelievers; prophecy, however, is not for unbelievers but for believers. 23So if the whole church comes together and everyone speaks in tongues, and inquirers or unbelievers come in, will they not say that you are out of your mind? 24But if an unbeliever or an inquirer comes in while everyone is prophesying, they are convicted of sin and are brought under judgment by all, 25as the secrets of their hearts are laid bare. So they will fall down and worship God, exclaiming, “God is really among you!”

Good Order in Worship

26What then shall we say, brothers and sisters? When you come together, each of you has a hymn, or a word of instruction, a revelation, a tongue or an interpretation. Everything must be done so that the church may be built up. 27If anyone speaks in a tongue, two—or at the most three—should speak, one at a time, and someone must interpret. 28If there is no interpreter, the speaker should keep quiet in the church and speak to himself and to God.

29Two or three prophets should speak, and the others should weigh carefully what is said. 30And if a revelation comes to someone who is sitting down, the first speaker should stop. 31For you can all prophesy in turn so that everyone may be instructed and encouraged. 32The spirits of prophets are subject to the control of prophets. 33For God is not a God of disorder but of peace—as in all the congregations of the Lord’s people.

34Women14:33,34 Or peace. As in all the congregations of the Lord’s people, 34 women should remain silent in the churches. They are not allowed to speak, but must be in submission, as the law says. 35If they want to inquire about something, they should ask their own husbands at home; for it is disgraceful for a woman to speak in the church.14:34,35 In a few manuscripts these verses come after verse 40.

36Or did the word of God originate with you? Or are you the only people it has reached? 37If anyone thinks they are a prophet or otherwise gifted by the Spirit, let them acknowledge that what I am writing to you is the Lord’s command. 38But if anyone ignores this, they will themselves be ignored.14:38 Some manuscripts But anyone who is ignorant of this will be ignorant

39Therefore, my brothers and sisters, be eager to prophesy, and do not forbid speaking in tongues. 40But everything should be done in a fitting and orderly way.