1 Wakorintho 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Wakorintho 13:1-13

Karama Ya Upendo

113:1 Mk 16:17; 1Kor 13:8Hata kama nitasema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolialia au toazi livumalo. 213:2 Efe 4:11; Mdo 11:27; 1Kor 14:2; 2Kor 8:7; 1Kor 12:9; Mt 17:20; 21:21Ningekuwa na karama ya unabii na kujua siri zote na maarifa yote, hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. 313:3 Lk 19:8; Mdo 2:45; Dan 3:28Kama nikitoa mali yote niliyo nayo na kama nikijitolea mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.

413:4 1The 5:14; 1Kor 5:2Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi. 513:5 1Kor 10:24; Mt 5:22; Ay 14:16-17; Mit 10:12; 7:19; 1Pet 4:8Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya. 613:6 2The 2:12; 2Yn 4; 1:3-4Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli. 713:7 1Kor 13:8, 13; Mit 10:12; 1Kor 9:12; Rum 15:1Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.

813:8 1Kor 13:2; 1Pet 4:8Upendo haushindwi kamwe. Lakini ukiwepo unabii, utakoma; zikiwepo lugha, zitakoma; yakiwepo maarifa, yatapita. 913:9 1Kor 8:2Kwa maana tunafahamu kwa sehemu na tunatoa unabii kwa sehemu. 1013:10 Flp 3:12Lakini ukamilifu ukija, yale yasiyo kamili hutoweka. 1113:11 Za 131:2Nilipokuwa mtoto, nilisema kama mtoto, niliwaza kama mtoto, nilifikiri kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto. 1213:12 Ay 26:14; 36:26; Mwa 32:30; Ay 19:26; 1Yn 3:2; 1Kor 8:2; 8:3; Gal 4:9Kwa maana sasa tunaona taswira kama kwa kioo, lakini wakati huo tutaona wazi. Sasa nafahamu kwa sehemu, wakati huo nitafahamu kikamilifu, kama vile mimi ninavyofahamika kikamilifu.

1313:13 Rum 5:2-5; Gal 5:5-6; Efe 4:25; Kol 1:4-5; 1The 1:3; Ebr 6:10-12; Mt 22:37-40; 1Kor 16:14; Gal 5:6; 1Yn 4:7-12, 16Basi sasa, yanadumu mambo haya matatu: Imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu miongoni mwa haya matatu ni upendo.