1 Wakorintho 12 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

1 Wakorintho 12:1-31

Karama Za Rohoni

112:1 Rum 1:11; 1Kor 1:7; 14:1, 37; Rum 11:25Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu. 212:2 Efe 2:2; Za 115:5; Yer 10:5; Hab 2:18-19Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au ingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena. 312:3 Rum 9:3; 1Kor 16:22; Yn 13:13; 4:2-3Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu.

412:4 Rum 12:4-8; Efe 4:11; Ebr 2:4Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 512:5 Rum 12:6; Efe 4:11Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. 612:6 Efe 4:6; Flp 2:13; Efe 1:23Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.

712:7 1Kor 14:12; Efe 4:12Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote. 812:8 1Kor 2:6; 2Kor 8:7Maana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo. 912:9 Mt 17:19-20; 1Kor 13:2; Mt 10:1Mtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya kwa huyo Roho mmoja. 1012:10 Gal 3:5; Efe 4:11; 1Yn 4:1; Mk 16:17Kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingine bado, tafsiri za lugha. 1112:11 1Kor 11:4; Rum 12:3; Efe 4:7; 1Kor 7:7Haya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo.

Mwili Mmoja, Wenye Viungo Vingi

1212:12 Rum 12:5; 1Kor 11:27Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo. 1312:13 Efe 2:18; Gal 3:28; Kol 3:11; Yn 7:37-38Kwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

1412:14 1Kor 12:12, 20Basi mwili si kiungo kimoja, bali ni viungo vingi. 15Kama mguu ungesema, “Kwa kuwa mimi si mkono basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya huo mguu usiwe sehemu ya mwili. 16Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili. 17Kama mwili wote ungelikuwa jicho, kusikia kungekuwa wapi? Au kama mwili wote ungelikuwa sikio, kunusa kungekuwa wapi? 1812:18 1Kor 12:28; 12:11Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda. 19Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? 20Kama ulivyo, una viungo vingi, lakini mwili ni mmoja.

21Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sina haja nawe!” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sina haja na ninyi!” 22Lakini badala yake, vile viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa dhaifu, ndivyo ambavyo ni vya muhimu sana. 23Navyo vile viungo tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee; 24wakati vile viungo vyenye uzuri havihitaji utunzaji wa pekee. Lakini Mungu ameviweka pamoja viungo vya mwili na akavipa heshima zaidi vile vilivyopungukiwa, 25ili pasiwe na mafarakano katika mwili, bali viungo vyote vihudumiane kwa usawa kila kimoja na mwenzake. 26Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia pamoja nacho, kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.

2712:27 Efe 1:23; 4:12; Kol 1:18, 24; Rum 12:5Sasa ninyi ni mwili wa Kristo na kila mmoja wenu ni sehemu ya huo mwili. 2812:28 1Kor 10:32; Efe 4:11; Mk 16:17; Rum 12:6-8Mungu ameweka katika kanisa, kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za kusaidiana, karama za uongozi, aina mbalimbali za lugha. 29Je, wote ni mitume? Je, wote ni manabii? Je, wote ni walimu? Je, wote wanatenda miujiza? 3012:30 1Kor 12:10Je, wote wana karama ya kuponya? Je, wote hunena kwa lugha mpya? Je, wote wanatafsiri? 3112:31 1Kor 14:1, 39Basi tamanini sana karama zilizo kuu.

Nami nitawaonyesha njia iliyo bora zaidi.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

哥林多前书 12:1-31

圣灵的恩赐

1弟兄姊妹,谈到圣灵的恩赐,我不希望你们无知。 2你们知道,自己在信主前曾受到迷惑和引诱去拜不会说话的偶像。 3因此我希望你们知道,一个被上帝的灵感动的人绝不会说“耶稣该受咒诅”;若不是受了圣灵的感动,没有人会说“耶稣是主”。

4恩赐各有不同,但圣灵是同一位。 5事奉各有不同,但主是同一位。 6工作各有不同,但上帝是同一位,祂在众人当中成就万事。 7圣灵给各人不同的恩赐为要使众人得益处。 8这人从圣灵领受智慧的话,那人从圣灵领受知识; 9圣灵赐这人信心,赐那人医病的恩赐; 10圣灵使这人能行神迹,使那人能做先知讲道;使这人能辨别诸灵,使那人能说方言12:10 “方言”或译“语言”。,又使另一人能翻译方言。 11这一切都是同一位圣灵所赐的,是祂按自己的旨意分别赐给各人的。

同属一个身体

12这如同一个身体有许多肢体,肢体虽多,仍同属一个身体。基督的身体也是这样。 13不论是犹太人或希腊人,是奴隶或自由人,我们都领受了同一位圣灵的洗礼,归入了同一个身体,同饮一位圣灵。

14人的身体并非只有一个肢体,而是由许多肢体组成的。 15如果脚说:“我不是手,所以我不属于身体”,难道它就因此不属于身体吗? 16如果耳朵说:“我不是眼睛,所以我不属于身体,”难道它就因此不属于身体吗? 17如果整个身体是一只眼睛,哪里有听觉呢?如果整个身体是一只耳朵,哪里有嗅觉呢?

18其实,上帝按自己的旨意将各个肢体安置在身体上了。 19全身如果只有一个肢体,还会是身体吗? 20如今肢体虽多,但身体只有一个。 21眼睛不能对手说:“我不需要你。”头也不能对脚说:“我不需要你。”

22相反,看起来不太重要的肢体其实是不可或缺的。 23我们认为身体上不体面的肢体,越要加以美化;不雅观的肢体,越要精心呵护。 24我们身上体面的肢体用不着美化。上帝把身体的各肢体安排在一起,使那些不体面的肢体更体面, 25这样身体各肢体才可以彼此相顾,不会分门别类。 26如果一个肢体感到痛苦,全身也一同受苦。如果一个肢体得到荣耀,全身也一同喜乐。

27你们就是基督的身体,并且各自都是身体的肢体。 28上帝在教会中设立的第一是使徒,第二是先知,第三是教师,其次是行神迹的,然后是有医病恩赐的,帮助别人的,管理事务的,说各种方言的。 29岂是都做使徒吗?都做先知吗?都做教师吗?都行神迹吗? 30都有医病的恩赐吗?都会说方言吗?都会翻译方言吗? 31你们应该热心追求更大的恩赐。

现在,我要将一条奇妙无比的道路指示你们!