1 Wafalme 18 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

1 Wafalme 18:1-46

Eliya Na Obadia

118:1 Lk 4:25; Kum 28:12Baada ya muda mrefu, katika mwaka wa tatu, neno la Bwana likamjia Eliya kusema, “Nenda ukajionyeshe kwa Ahabu na mimi nitanyesha mvua juu ya nchi.” 218:2 Law 26:26Kwa hiyo Eliya akaenda kujionyesha kwa Ahabu.

Wakati huu njaa ilikuwa kali sana katika Samaria, 318:3 1Fal 16:9; Neh 7:2naye Ahabu alikuwa amemwita Obadia ambaye alikuwa msimamizi wa jumba lake la kifalme. (Obadia alimcha Bwana sana. 418:4 1Fal 21:23; Yer 26:24Wakati Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa Bwana, Obadia alikuwa amewachukua manabii mia moja na kuwaficha katika mapango mawili, hamsini kwenye kila moja na akawa akiwapa chakula na maji.) 518:5 Yer 14:3; Mwa 47:4Ahabu alikuwa amemwambia Obadia, “Nenda katika nchi yote kwenye vijito vyote na mabonde. Huenda tunaweza kupata majani ya kuwalisha farasi na nyumbu wapate kuishi ili tusilazimike kuwaua hata mmoja wa wanyama wetu.” 6Kwa hiyo wakagawanya nchi waliyokusudia kutafuta majani, Ahabu akaenda upande mmoja na Obadia upande mwingine.

718:7 2Fal 1:8; Zek 13:4Wakati Obadia alipokuwa akitembea njiani, Eliya akakutana naye. Obadia akamtambua, akamsujudia hadi nchi na kusema, “Je, hivi kweli ni wewe, bwana wangu Eliya?”

8Eliya akamjibu, “Ndiyo, nenda ukamwambie bwana wako Ahabu, ‘Eliya yuko hapa.’ ”

9Obadia akamuuliza, “Ni kosa gani nimefanya, hata ukaamua kumkabidhi mtumishi wako mkononi mwa Ahabu ili aniue? 1018:10 1Fal 17:3Hakika kama Bwana Mungu wako aishivyo, hakuna taifa hata moja au ufalme ambapo bwana wangu hajamtuma mtu kukutafuta. Kila wakati taifa au ufalme walipodai kwamba haupo huko, aliwafanya waape kwamba hawakuweza kukupata. 11Lakini sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kusema, ‘Eliya yuko hapa.’ 1218:12 2Fal 2:16; Eze 3:14; Mdo 8:39Sijui ni wapi Roho wa Bwana ataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Kama nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua. Hata hivyo mimi mtumishi wako nimemwabudu Bwana tangu ujana wangu. 13Je, hukusikia, bwana wangu, nilifanya nini wakati Yezebeli alipokuwa akiua manabii wa Bwana? Niliwaficha manabii wa Bwana mia moja katika mapango mawili, hamsini katika kila moja, nami nikawapatia chakula na maji. 14Nawe sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kumwambia, ‘Eliya yuko hapa.’ Yeye ataniua!”

15Eliya akasema, “Kama Bwana Mwenye Nguvu Zote aishivyo, yeye ninayemtumikia, hakika nitajionyesha kwa Ahabu leo.”

Eliya Juu Ya Mlima Karmeli

16Basi Obadia akaenda kukutana na Ahabu na kumwambia, naye Ahabu akaenda kukutana na Eliya. 1718:17 Yos 7:25; 1Fal 21:20Ahabu alipomwona Eliya, akamwambia, “Je, ni wewe, mtaabishaji wa Israeli?”

1818:18 1Fal 16:33Eliya akamjibu, “Mimi sijaitaabisha Israeli. Lakini wewe na jamaa ya baba yako ndio mnaofanya hivyo. Mmeziacha amri za Bwana na mkafuata Mabaali. 1918:19 2Fal 10:19; Yos 19:26Sasa waite watu kutoka Israeli yote tukutane nao juu ya Mlima Karmeli. Nawe uwalete hao manabii wa Baali mia nne na hamsini na hao manabii mia nne wa Ashera, walao chakula mezani mwa Yezebeli.”

2018:20 2Fal 2:25; 4:25Ndipo Ahabu akatuma ujumbe katika Israeli yote na kuwakusanya manabii hao juu ya mlima Karmeli. 2118:21 Yos 24:15; 2Fal 17:41; Mt 6:24Eliya akasimama mbele ya watu na kusema, “Mtasitasita katika mawazo mawili hadi lini? Ikiwa Bwana ndiye Mungu, mfuateni yeye; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye.”

Lakini watu hawakusema kitu.

2218:22 1Fal 19:10; Yer 2:8Kisha Eliya akawaambia, “Ni mimi peke yangu nabii wa Bwana aliyebaki, lakini Baali ana manabii mia nne na hamsini. 23Leteni mafahali wawili. Wao na wajichagulie mmoja, wamkate vipande vipande na waweke juu ya kuni lakini wasiiwashie moto. Nitamwandaa huyo fahali mwingine na kumweka juu ya kuni lakini sitawasha moto. 2418:24 1Sam 7:8; Law 9:24Kisha mliitie jina la mungu wenu, nami nitaliitia jina la Bwana Mungu yule ambaye atajibu kwa moto, huyo ndiye Mungu.”

Kisha watu wote wakasema, “Hilo unalosema ni jema.”

25Eliya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni mmoja kati ya hawa mafahali na mwe wa kwanza kumwandaa, kwa kuwa ninyi mko wengi sana. Liitieni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto.” 2618:26 Za 115:4-5; 1Kor 8:4; 12:2Kwa hiyo wakamchukua yule fahali waliyepewa, nao wakamwandaa.

Kisha wakaliitia jina la Baali kutoka asubuhi hadi adhuhuri, wakapiga kelele, “Ee Baali, utujibu!” Lakini hapakuwa na jibu; hakuna aliyejibu. Nao wakacheza kuizunguka madhabahu waliyoijenga.

27Wakati wa adhuhuri, Eliya akaanza kuwadhihaki, akisema, “Pigeni kelele zaidi! Hakika yeye ni mungu! Labda amezama katika mawazo mazito, au ana shughuli nyingi, au amesafiri. Labda amelala usingizi mzito, naye ni lazima aamshwe.” 2818:28 Law 19:28Kwa hiyo wakapiga kelele zaidi na kama ilivyokuwa desturi yao wakajichanja wenyewe kwa visu na vyembe, mpaka damu ikachuruzika. 2918:29 Kut 29:41; 2Fal 19:12; Isa 16:12Adhuhuri ikapita, nao wakaendelea na utabiri wao wa kiwazimu mpaka wakati wa dhabihu ya jioni. Lakini hapakuwa na jibu, hakuna aliyejibu, hakuna aliyeangalia.

3018:30 1Fal 19:10Kisha Eliya akawaambia watu wote, “Sogeeni karibu nami.” Watu wote wakamkaribia, naye akakarabati madhabahu ya Bwana, ambayo ilikuwa imevunjwa. 3118:31 2Fal 17:34; Mwa 17:5Eliya akachukua mawe kumi na mawili, moja kwa ajili ya kila kabila la wana wa Yakobo, ambaye neno la Bwana lilimjia, likisema, “Jina lako litakuwa Israeli.” 3218:32 Kol 3:17; Kum 18:7Kwa mawe hayo, akajenga madhabahu katika jina la Bwana, na akachimba handaki kuizunguka, ukubwa wa kutosha vipimo viwili vya mbegu. 3318:33 Mwa 22:9Akapanga kuni, akamkata yule fahali vipande vipande na kuvipanga juu ya kuni. Kisha akawaambia, “Jazeni mapipa manne maji na kuyamwaga juu ya sadaka ya kuteketezwa na juu ya kuni.”

34Akawaambia, “Fanyeni hivyo tena.” Nao wakafanya hivyo tena.

Akaagiza, “Fanyeni kwa mara ya tatu.” Nao wakafanya hivyo kwa mara ya tatu. 35Maji yakatiririka kuizunguka madhabahu na hata kujaza lile handaki.

3618:36 Kut 29:39, 41; Yos 4:24; Hes 16:28Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea mbele na kuomba, akisema: “Ee Bwana, Mungu wa Abrahamu, na Isaki na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. 3718:37 Yos 4:24Unijibu mimi, Ee Bwana, nijibu mimi, ili watu hawa wajue kwamba wewe, Ee Bwana, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena.”

3818:38 Law 9:24; 1Nya 21:26; Ay 1:16Kisha moto wa Bwana ukashuka na kuiteketeza ile dhabihu, zile kuni, yale mawe, ule udongo, na pia kuramba yale maji yaliyokuwa ndani ya handaki.

3918:39 Law 9:24; Za 46:10Wakati watu wote walipoona hili, wakaanguka kifudifudi na kulia, “Bwana: yeye ndiye Mungu! Bwana: yeye ndiye Mungu!”

4018:40 Amu 4:7; Kut 22:20Kisha Eliya akawaamuru, “Wakamateni hao manabii wa Baali. Msimwache hata mmoja atoroke!” Wakawakamata, naye Eliya akawaleta mpaka Bonde la Kishoni na kuwachinja huko.

41Eliya akamwambia Ahabu, “Nenda, ukale na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa.” 4218:42 Yak 5:18; Isa 5:18Hivyo Ahabu akaondoka ili kula na kunywa. Lakini Eliya akapanda kileleni mwa Karmeli, akasujudu na akaweka kichwa chake katikati ya magoti yake.

43Akamwambia mtumishi wake, “Nenda ukatazame kuelekea bahari.” Akaenda na kutazama.

Akasema, “Hakuna kitu chochote huko.”

Mara saba Eliya akasema, “Nenda tena.”

4418:44 Yos 6:15; Lk 12:54Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, “Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini.”

Hivyo Eliya akasema, “Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Tandika gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ ”

4518:45 Ay 37:13; Hos 1:4Wakati ule ule anga likawa jeusi kwa mawingu, upepo ukainuka na mvua kubwa ikanyesha, naye Ahabu akaenda zake Yezreeli. 4618:46 Amu 3:10; 2Fal 4:29Nguvu za Bwana zikamjia Eliya, naye akajikaza viuno, akakimbia mbele ya Ahabu njia yote hadi maingilio ya Yezreeli.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

列王紀上 18:1-46

以利亞戰勝巴力的先知

1旱災持續了三年。一天,耶和華對以利亞說:「你去見亞哈。我要降雨在地上。」 2以利亞就去見亞哈。當時,撒瑪利亞正遭受嚴重饑荒。 3-4亞哈的宮廷總管俄巴底非常敬畏耶和華,耶洗別屠殺耶和華的眾先知時,他救了一百名先知,把他們分別藏在兩個山洞裡,每洞五十人,並供應他們飲食。亞哈召見俄巴底5對他說:「我們去各地的水泉和河谷,也許可以找到草救活騾馬,不致喪失牲畜。」 6於是,亞哈俄巴底分頭到不同地區尋找。

7俄巴底在路上遇見了以利亞俄巴底認出了他,就俯伏在地上說:「你是我主以利亞嗎?」 8以利亞回答說:「我就是,你去告訴你主人我在這裡。」 9俄巴底說:「僕人犯了什麼罪,你竟叫我去亞哈那裡送死? 10我憑你的上帝——永活的耶和華起誓,王派人到各邦各國尋找你,任何邦國若說你不在那裡,王就要他們起誓說真的找不到你。 11現在,你叫我去告訴我主人你在這裡, 12我離開你以後,不知道耶和華的靈會把你帶到哪裡。如果我去告訴亞哈,他來了卻找不到你,必定會殺我。但僕人自幼就敬畏耶和華。 13耶洗別屠殺耶和華的眾先知時,我把一百名先知分別藏在兩個山洞裡,每洞五十人,供應他們飲食。我主沒有聽說這事嗎? 14現在,你要我去告訴我主人你在這裡,這是讓我去送死。」 15以利亞說:「我事奉的是永活的萬軍之耶和華,我憑祂起誓,我今天必出現在亞哈面前。」

16於是,俄巴底去稟告亞哈亞哈就來找以利亞17見到以利亞後,就說:「給以色列帶來災禍的就是你嗎?」 18以利亞回答說:「給以色列帶來災禍的不是我,而是你和你父親家,因為你們拋棄耶和華的誡命,去隨從巴力19現在,你快派人去召集所有的以色列人到迦密山來見我,把四百五十名巴力的先知和耶洗別所供養的四百名亞舍拉的先知也帶來。」

20亞哈便派人把以色列人和那些先知招聚到迦密山。 21以利亞走到眾人面前說:「你們三心二意要到什麼時候呢?如果耶和華是上帝,你們當跟從祂;如果巴力是上帝,你們就跟從他吧!」他們都默不作聲。 22以利亞繼續對眾人說:「耶和華的先知現在只剩下我一人,巴力的先知卻有四百五十人。 23請給我們牽兩頭公牛來,巴力的先知可以選一頭,切成塊放在柴上,但不要點火;我會把另一頭公牛預備好,放在柴上,也不點火。 24然後,你們求告你們神明的名字,我求告耶和華的名,那聽禱告降下火來的就是上帝。」眾人非常贊同他的主意。 25以利亞巴力的先知說:「你們人數眾多,可先選一頭公牛預備好,然後呼求你們的神明,但不可點火。」 26他們取了公牛預備好,然後從早上到正午不斷地呼求巴力的名:「巴力啊,求你應允我們!」可是毫無動靜。他們又繞著自己築的祭壇跳個不停。

27中午時分,以利亞譏諷他們說:「喊大聲點吧,它肯定是神明!也許它在沉思冥想,也許太忙了,也許出遊了,也許睡著了,需要人叫醒它!」 28於是,他們更加大聲呼求,並按自己的風俗用刀槍自割自刺,直到身體流血。 29過了中午,他們仍不斷地狂呼亂叫,直到獻晚祭的時候,仍然毫無動靜,沒有半點反應。

30以利亞把眾人召集到自己跟前,他重修已遭毀壞的耶和華的祭壇, 31拿了十二塊石頭分別代表雅各子孫的十二支派。耶和華曾經對雅各說:「你的名字要叫以色列。」 32以利亞就奉耶和華的名用那些石頭築了一座祭壇,又在壇的周圍挖了一條能盛十五升穀種的溝, 33然後在壇上擺好柴,把公牛切成塊放在柴上,對眾人說:「你們去打四桶水倒在祭物和柴上。」他們照做了。 34以利亞吩咐他們再倒一次,他們又倒了一次。以利亞又吩咐他們倒第三次,他們就倒了第三次。 35水流到壇的四周,溝裡也灌滿了。

36到了獻晚祭的時候,以利亞先知走到壇前禱告:「亞伯拉罕以撒以色列的上帝耶和華啊,求你今天讓這些人知道你是以色列的上帝,我是你的僕人,我是按你的命令做這一切事。 37耶和華啊,求你應允我,應允我,好讓眾人知道你耶和華是上帝,你要使他們回心轉意。」 38於是,耶和華降火燒盡了祭物、木柴、石頭、塵土,甚至燒乾了溝裡的水。 39眾人看見這情景,都俯伏在地高呼:「耶和華是上帝!耶和華是上帝!」 40以利亞對他們說:「抓住巴力的先知,別放走一個人!」眾人就抓住他們,以利亞把他們帶到基順河邊,在那裡殺了他們。

上帝降雨

41以利亞亞哈說:「你去吃喝吧,因為已傳來大雨聲。」 42亞哈就去吃喝。以利亞上到迦密山頂,跪在地上,臉伏在雙膝之間。 43他吩咐僕人:「你去向海的方向觀看。」僕人就去觀看,然後說:「什麼也沒有。」以利亞又讓他去觀看,前後共七次。 44第七次,僕人說:「我看見一朵手掌那麼大的雲從海裡升起來了。」以利亞便吩咐他:「你去告訴亞哈,叫他套車下山,免得被雨阻擋。」 45霎時間,天上烏雲密佈,狂風大作,下起大雨。亞哈坐著馬車回耶斯列46耶和華的手按在以利亞身上,他就束上腰帶,飛奔回城,在亞哈之前到達耶斯列的城門。