1 Wafalme 15 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

1 Wafalme 15:1-34

Abiya Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 13:1–14:1)

1Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda, 215:2 2Nya 11:20naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.15:2 Yaani Absalomu, maana yake Baba wa amani.

315:3 1Fal 8:61Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana Mungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa. 415:4 2Sam 21:17Pamoja na hayo, kwa ajili ya Daudi, Bwana Mungu wake akampa taa katika Yerusalemu kwa kumwinua mwana atawale badala yake na kwa kuifanya Yerusalemu kuwa imara. 515:5 2Sam 11:2-27Kwa kuwa Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana na hakushindwa kushika maagizo yote ya Bwana siku zote za uhai wake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.

615:6 1Fal 12:21; 2Nya 16:9Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu wakati wote wa maisha ya Abiya. 7Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Abiya na yote aliyofanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu. 8Naye Abiya akalala na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake.

Asa Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 15:16–16:6)

9Katika mwaka wa ishirini wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akawa mfalme wa Yuda, 10naye akatawala katika Yerusalemu miaka arobaini na mmoja. Bibi yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.

1115:11 1Fal 9:4Asa akatenda yaliyo mema machoni mwa Bwana, kama alivyokuwa ametenda Daudi baba yake. 1215:12 1Fal 14:24Akawafukuza mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu kutoka nchi na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza. 13Hata akamwondoa bibi yake Maaka kwenye wadhifa wake kama mama malkia, kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni. 1415:14 2Nya 14:5; 1Fal 8:61Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote. 1515:15 2Sam 8:11Akaleta ndani ya Hekalu la Bwana fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.

1615:16 1Fal 12:21Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zote za utawala wao. 1715:17 Yos 18:25Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.

1815:18 Yoe 3:5; Yer 49:27Kisha Asa akachukua fedha yote na dhahabu iliyokuwa imeachwa katika hazina za Hekalu la Bwana na za jumba lake mwenyewe la kifalme. Akawakabidhi maafisa wake na kuwatuma kwa Ben-Hadadi mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Aramu,15:18 Yaani Shamu (ambayo leo ni Syria). aliyekuwa akitawala Dameski. 19“Akasema na pawepo mkataba kati yangu na wewe, kama ulivyokuwepo kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekuletea zawadi ya fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniondokee mimi.”

20Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Akaishinda miji ya Iyoni, Dani, Abel-Beth-Maaka na Kinerethi yote, pamoja na Naftali. 21Wakati Baasha aliposikia hili, akaacha kuijenga Rama na akaenda kuishi Tirsa. 2215:22 Yos 18:24; 2Fal 23:8Kisha Mfalme Asa akatoa amri kwa Yuda yote, pasipo kumbagua hata mmoja, kubeba mawe na mbao kutoka Rama, ambazo Baasha alikuwa akitumia huko. Mfalme Asa akazitumia kujengea Geba iliyoko Benyamini na Mispa pia.

23Kwa matukio yote ya utawala wa Asa, mafanikio yake yote, yote aliyofanya na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Katika uzee wake, hata hivyo, alipata ugonjwa wa miguu. 2415:24 Mt 1:8Kisha Asa akalala pamoja na baba zake na kuzikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Naye Yehoshafati mwanawe akawa mfalme baada yake.

Nadabu Mfalme Wa Israeli

25Nadabu mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Asa wa Yuda, naye akatawala Israeli kwa miaka miwili. 2615:26 1Fal 12:30; Kum 4:25Akafanya maovu machoni pa Bwana, akienenda katika njia za baba yake na katika dhambi yake, ambayo alisababisha Israeli kuifanya.

2715:27 1Fal 14:14; Yos 19:44Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akafanya shauri baya dhidi yake, naye akamuua huko Gibethoni, mji wa Wafilisti, wakati Nadabu na Israeli yote walipokuwa wameuzingira. 28Baasha akamuua Nadabu katika mwaka wa tatu wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, naye Baasha akaingia mahali pake kuwa mfalme.

29Mara tu alipoanza kutawala, aliua jamaa yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu yeyote aliyekuwa hai, bali aliwaangamiza wote, kulingana na neno la Bwana lililotolewa kupitia kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni, 30kwa sababu ya dhambi alizokuwa amezitenda Yeroboamu na kusababisha Israeli kuzitenda, tena kwa sababu alimkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli.

31Kwa matukio mengine ya utawala wa Nadabu na yote aliyofanya, je hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 32Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli wakati wote wa utawala wao.

Baasha Mfalme Wa Israeli

33Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya akawa mfalme wa Israeli yote huko Tirsa, naye akatawala kwa miaka ishirini na minne. 34Akatenda maovu machoni pa Bwana, akienenda katika njia za Yeroboamu na dhambi yake, ambayo alikuwa amesababisha Israeli kuitenda.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

列王纪上 15:1-34

亚比央做犹大王

1尼八的儿子耶罗波安王执政第十八年,亚比央登基做犹大王。 2他在耶路撒冷执政三年,母亲是押沙龙的女儿玛迦

3亚比央和他父亲一样作恶多端,没有像他祖先大卫一样忠于他的上帝耶和华。 4但他的上帝耶和华因为大卫的缘故,仍然让他儿子在耶路撒冷继位,使耶路撒冷坚立。 5除了乌利亚事件以外,大卫一生都做耶和华视为正的事,没有违背耶和华的任何命令。

6罗波安耶罗波安之间常有战事,一直延续到亚比央王朝。 7亚比央耶罗波安之间也常有战事。亚比央其他的事及一切所为都记在《犹大列王史》上。 8亚比央与祖先同眠后,葬在大卫城,他儿子亚撒继位。

亚撒做犹大王

9耶罗波安以色列王第二十年,亚撒登基做犹大王, 10他在耶路撒冷执政四十一年。他祖母是押沙龙的女儿玛迦11亚撒效法他祖先大卫,做耶和华视为正的事。 12他从国中驱逐了男庙妓,清除了他祖先制造的一切偶像。 13亚撒还废除了他祖母玛迦的太后之位,因为她造了可憎的亚舍拉神像。亚撒把她的神像砍倒,放在汲沦溪烧掉。 14他虽然没有清除丘坛,但一生忠于耶和华。 15他把自己和父亲奉献的金银及器皿都带到耶和华的殿里。

16亚撒以色列巴沙执政期间,双方常常交战。 17以色列巴沙上来攻打犹大,并修筑拉玛,不许任何人进出犹大亚撒的地界。 18于是,亚撒把耶和华殿里和王宫库房里剩余的金银交给臣仆,派他们送给大马士革亚兰王,即他伯利们的儿子、希旬的孙子便·哈达,说: 19“我们之间应立盟约,像我们的父辈间立约一样,现在奉上金银为礼,请你取消与以色列巴沙的盟约。这样,他就会从我境内退兵。” 20便·哈达接受了亚撒王的提议,派将领攻打以色列的城邑,攻占了以云亚伯·伯·玛迦基尼烈全境和拿弗他利全境。 21巴沙闻讯,就停止修筑拉玛,退回得撒去了。 22亚撒王号令全体犹大人出动,任何人不得有误,将巴沙修筑拉玛的石头和木材搬走,用它们修建便雅悯迦巴米斯巴23亚撒其他的事,包括他的功业和兴建城邑的事迹都记在《犹大列王史》上。亚撒年老的时候,患了脚疾。 24他与祖先同眠后,葬在大卫城他的祖坟里。他儿子约沙法继位。

拿答做以色列王

25亚撒犹大王第二年,耶罗波安的儿子拿答登基做以色列王,执政两年。 26拿答行耶和华视为恶的事,像他父亲一样作恶多端,使以色列人陷入罪中。 27-28亚撒犹大王第三年,拿答以色列军围攻非利士基比顿城时,以萨迦支派亚希雅的儿子巴沙叛变,杀了拿答,篡位称王。 29巴沙一做王,立刻诛杀耶罗波安全家,不留一个活口,应验了耶和华借祂仆人示罗亚希雅所说的话。 30这是因为耶罗波安犯罪,并使以色列人陷入罪中,惹以色列的上帝耶和华发怒。 31拿答其他的事及一切所为都记在《以色列列王史》上。 32亚撒以色列巴沙执政期间,双方常常交战。

巴沙做以色列王

33犹大亚撒执政第三年,亚希雅的儿子巴沙得撒登基做以色列王,执政二十四年。 34他做耶和华视为恶的事,步耶罗波安的后尘,使以色列人陷入罪中。