1 Wafalme 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Wafalme 10:1-29

Malkia Wa Sheba Amtembelea Solomoni

(2 Nyakati 9:1-12)

110:1 2Nya 20:9; Dan 9:20Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Solomoni na uhusiano wake na jina la Bwana, akaja kumjaribu kwa maswali magumu. 210:2 Ezr 9:2; Kut 34:13; Neh 13:27; Kum 30:8-10Alifika Yerusalemu akiwa na msafara mkubwa sana: pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani; alikuja kwa Solomoni na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake. 310:3 2Fal 11:17; 2Nya 34:31; Kut 34:16; Kum 7:2-3; Ezr 9:4; Za 119:53, 120; Isa 66:2Solomoni akamjibu maswali yake yote, hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwa mfalme asiweze kumwelezea. 410:4 1Nya 28:10; Isa 35:3-4Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Solomoni na jumba la kifalme alilokuwa amejenga, 510:5 Neh 5:12; 13:25chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika hekalu la Bwana, alipatwa na mshangao.

610:6 Kum 9:18; Yn 3:7; Za 102:4Akamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli. 7Lakini sikuamini mambo haya hadi nilipokuja na kuona kwa macho yangu mwenyewe. Naam, sikuambiwa hata nusu yake; katika hekima na mali umezidi sana ile taarifa niliyoisikia. 810:8 Law 27:28; Yos 6:19Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wasimamao mbele yako daima na kusikia hekima yako! 910:9 1Sam 12:18; Ezr 1:5Ahimidiwe Bwana Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe na kukuweka juu ya kiti cha ufalme cha Israeli. Kwa sababu ya upendo wake Bwana wa milele ajili ya Israeli, amekufanya mfalme, ili kudumisha haki na uadilifu.”

10Naye akampa mfalme talanta 12010:10 Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5. za dhahabu, kiasi kikubwa sana cha vikolezi na vito vya thamani. Haikuwahi kamwe kuletwa tena vikolezi vingi hivyo kuletwa kama vile malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Solomoni.

1110:11 Kum 24:1; Mit 28:13; Mal 2:10-16; Yer 3:13; Isa 1:16-17; Rum 12:2(Meli za Hiramu zilileta dhahabu kutoka Ofiri; tena kutoka huko zilileta shehena kubwa ya miti ya msandali na vito vya thamani. 1210:12 Yos 6:5Mfalme akatumia miti ya msandali kuwa nguzo ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa au kuonekana humo tangu siku ile.)

13Mfalme Solomoni akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, kando na vile mfalme alivyokuwa amempa kwa ukarimu wake wa kifalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake.

Fahari Ya Solomoni

(2 Nyakati 9:13-28)

1410:14 Kum 16:18; Hes 25:4; 2Nya 30:8; 2Fal 23:26; 2Nya 28:11-13; 29:10; 30:8; Za 78:38; Isa 12:1Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,10:14 Talanta 666 za dhahabu ni sawa na tani 25. 1510:15 Neh 11:16mbali na mapato kutoka kwa wafanyabiashara na wachuuzi, na kutoka kwa wafalme wote wa Kiarabu na watawala wa nchi.

16Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa; kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 60010:16 Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 3.5. 17Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu10:17 Mane tatu za dhahabu ni sawa na kilo 1.7. za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.

1810:18 Ezr 5:2; 2:2; Amu 3:6; Zek 6:1Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi. 1910:19 2Fal 10:15; Law 5:15; 6:4-6; 1Nya 29:24; 2Nya 30:8; Gal 2:9; Mit 22:26Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na egemeo la nyuma lilikuwa la mviringo kwa juu. Pande zote za kiti kulikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono. 2010:20 1Nya 24:14Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wowote. 2110:21 1Nya 24:8Vikombe vyote vya Mfalme Solomoni vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo siku za Solomoni. 2210:22 1Nya 9:12Mfalme alikuwa na meli nyingi za biashara10:22 Au: za Tarshishi (ona pia 1Fal 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 2:16; 60:9). baharini zilizokuwa zikiandamana na meli za Hiramu. Kwa mara moja kila miaka mitatu zilirudi, zikiwa zimebeba dhahabu, fedha, pembe za ndovu na nyani wakubwa na wadogo.

2310:23 Neh 8:7; 9:4Mfalme Solomoni alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia. 2410:24 Neh 3:1; 12:10Dunia yote ikatafuta kukutana na Solomoni ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake. 2510:25 Ezr 3:2; 8:3; Neh 7:13Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja alileta zawadi: vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezi, farasi na nyumbu.

2610:26 Kum 17:16Solomoni akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari na mengine akawa nayo huko Yerusalemu. 2710:27 Ay 27:16; 1Nya 27:28Mfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani. 28Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue.10:28 Yaani Kilikia ilioko Syria. Wafanyabiashara wa mfalme waliwanunua kutoka Kue. 2910:29 Hes 13:29Waliagiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha10:29 Shekeli 600 za fedha ni sawa na kilo 7. na farasi kwa shekeli 150.10:29 Shekeli 150 za fedha ni sawa na kilo 1.7. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.10:29 Waaramu hapa ina maana ya Washamu.