1 Timotheo 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Timotheo 4:1-16

Maagizo Kwa Timotheo

14:1 Mdo 8:29; 2Tim 3:1; 1The 2:3Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. 24:2 Efe 4:19Mafundisho kama hayo huja kupitia kwa waongo ambao ni wanafiki, hali dhamiri zao zikiungua kwa kuchomwa moto. 34:3 Ebr 13:4; Kol 2:16; Mwa 1:29; Rum 14:6Wao huwakataza watu wasioe na kuwaagiza wajiepushe na vyakula fulani, ambavyo Mungu aliviumba ili vipokewe kwa shukrani na wale wanaoamini na kuijua kweli. 44:4 Rum 14:14-18Kwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema, wala hakuna kitu chochote cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani, 54:5 Ebr 4:12kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.

Mtumishi Mwema Wa Yesu Kristo

64:6 1Tim 1:10Kama ukiwakumbusha ndugu mambo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, uliyelelewa katika kweli ya imani na yale mafundisho mazuri uliyoyafuata. 74:7 2Tim 2:16Usijishughulishe kamwe na hadithi za kipagani na masimulizi ya uongo ya wanawake wazee; badala yake, jizoeze kuwa mtauwa. 84:8 1Tim 6:6; Mit 22:4; Mt 6:33Kwa maana mazoezi ya mwili yana faida kwa sehemu, lakini utauwa una faida katika mambo yote, yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa na ya ule ujao.

94:9 1Tim 1:15Hili ni neno la kuaminiwa tena lastahili kukubaliwa kabisa, 104:10 1Kor 4:11, 12; 1Tim 6:17; Za 36:6(nasi kwa ajili ya hili tunajitaabisha na kujitahidi), kwamba tumeweka tumaini letu kwa Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi wa watu wote, hasa wale waaminio.

114:11 1Tim 5:7; 6:2Mambo haya yaagize na kuyafundisha. 124:12 Flp 3:17; 1The 1:7; 1Tim 1:14Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi. 134:13 1Tim 3:14; Lk 4:16; Mdo 13:14-16; Kol 4:16; 1The 5:27Fanya bidii kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja. 144:14 1Tim 1:18; Mdo 6:6; 2Tim 1:6Usiache kutumia kipawa kilicho ndani yako, ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee walikuwekea mikono.

15Uwe na bidii katika mambo haya; ujitolee kwa ajili ya mambo haya kikamilifu, ili kila mtu aone kuendelea kwako. 164:16 Rum 11:14; Mdo 20:28; Eze 33:9; 1Kor 9:22Jilinde sana nafsi yako na mafundisho yako. Dumu katika hayo, kwa maana kwa kufanya hivyo, utajiokoa wewe mwenyewe pamoja na wale wanaokusikia.