1 Timotheo 2 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

1 Timotheo 2:1-15

Maagizo Kuhusu Kuabudu

12:1 Efe 6:18; Flp 4:6Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: 22:2 Ezr 6:10; Rum 13:1kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. 32:3 Mdo 20:1; 1Tim 5:4; Lk 1:42Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu, 42:4 Eze 18:23-32; 1Tim 4:10; 2Tim 2:25anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli. 52:5 Rum 10:12; Gal 3:20Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu, 62:6 1Kor 1:6; 1Tim 6:15aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wanadamu wote: jambo hili lilishuhudiwa kwa wakati wake ufaao. 72:7 2Tim 1:11; Mdo 9:15; Efe 3:7-8Nami kwa kusudi hili nimewekwa niwe mhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo wala sisemi uongo), mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli.

82:8 Za 24:4; Lk 24:50Nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono mitakatifu pasipo hasira wala kugombana.

92:9 1Pet 3:3Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, 102:10 1Tim 5:10; Mit 31:13bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.

112:11 1Kor 14:34; 1Pet 3:3, 4Mwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utiifu wote. 122:12 Efe 5:22; 1Kor 14:34; Mwa 3:16Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya. 132:13 Mwa 2:7, 22; 1Kor 11:8Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva. 142:14 Mwa 3:1-6, 13; 2Kor 11:3Wala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji. 152:15 1Tim 1:14Lakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

提摩太前書 2:1-15

要為他人禱告

1我勸你首先要為所有的人懇求、禱告、代求和感謝上帝。 2也要為所有的君王和掌權者禱告,使我們可以懷著虔誠、端正的心過和平安寧的生活。 3這樣做很美好,是蒙我們的救主上帝悅納的。 4因為祂願世人都得救,明白真理。 5上帝只有一位,在上帝和世人之間只有一位中保,就是降世為人的基督耶穌。 6祂捨命作所有人的贖價,這在所定的時候已顯明出來。 7為此,我被指派做傳道人和使徒,教導外族人認識信仰和真理。我說的是實話,並非謊言。

信徒的操守

8我願男人舉起聖潔的手隨處禱告,不發怒,不爭辯2·8 「爭辯」或譯「疑惑」。9我願女人衣著得體,樸素端莊,不靠髮型、珠寶金飾或名貴衣服來妝飾自己, 10要有善行,這樣才配稱為敬畏上帝的女人。 11女人應當安安靜靜地學習,完全順服。

12我不准女人教導或管轄男人,她們應當保持安靜。 13因為先造的是亞當,後造的是夏娃14並非亞當受騙,而是夏娃受騙陷入罪中。 15不過,女人如果持守信心和愛心,聖潔自律,就必在生育的事上得救。