1 Samweli 5 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 5:1-12

Sanduku La Agano Huko Ashdodi Na Ekroni

15:1 1Sam 4:1; Yos 11:22; 13:3; 1Sam 7:12Baada ya Wafilisti kuteka Sanduku la Mungu, walilichukua kutoka Ebenezeri mpaka Ashdodi. 25:2 Amu 16:23; Isa 2:18; 19:1; 46:1Kisha wakaliingiza lile Sanduku ndani ya hekalu la Dagoni na kuliweka kando ya huyo Dagoni. 35:3 Isa 40:20; 41:7; Yer 10:4; Isa 46:7; Kut 12:12; 18:11; 1Nya 16:24-26; Za 95:3; 97:9; Isa 19:1; 46:1, 2, 7; Nah 1:14Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake. 45:4 Eze 6:6; Mik 1:7; Isa 40:18; Yer 50:2Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta huyo Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa navyo vimelala kizingitini, ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki. 55:5 Sef 1:9Ndiyo sababu mpaka leo makuhani wa Dagoni wala wengine waingiao katika hekalu la Dagoni huko Ashdodi hawakanyagi kizingiti.

65:6 Za 32:4; 78:66; Mdo 13:11; 2Sam 6:7; Kum 28:27; 1Sam 6:5Mkono wa Bwana ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi na vijiji jirani, akaleta uharibifu juu yao na kuwatesa kwa majipu. 7Watu wa Ashdodi walipoona kile kilichokuwa kikitokea, wakasema, “Sanduku la Mungu wa Israeli kamwe lisikae hapa pamoja na sisi, kwa sababu mkono wake ni mzito juu yetu na juu ya Dagoni mungu wetu.” 85:8 Amu 16:18; Yos 11:12Basi wakawaita watawala wote wa Wafilisti pamoja na kuwauliza, “Tutafanya nini na hili Sanduku la Mungu wa Israeli?”

Wakajibu, “Sanduku la Mungu wa Israeli na liende Gathi.” Basi wakalihamisha Sanduku la Mungu wa Israeli.

95:9 Kut 14:24; Kum 2:15Lakini baada ya kulihamisha, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi ya huo mji wa Gathi, akiuweka katika fadhaa kuu. Mungu akawatesa watu wa huo mji, vijana kwa wazee, kwa kuwaletea majipu. 105:10 Yos 13:3Basi wakapeleka Sanduku la Mungu Ekroni.

Wakati Sanduku la Mungu lilipokuwa linaingia Ekroni, watu wa Ekroni walilia wakisema “Wamelileta Sanduku la Mungu wa Israeli kwetu ili kutuua sisi na watu wetu.” 11Basi wakawaita watawala wote wa Wafilisti pamoja na kusema, “Liondoeni Sanduku la Mungu wa Israeli na lirudishwe mahali pake, la sivyo litatuua sisi na watu wetu.” Kwa kuwa kifo kilikuwa kimeujaza mji hofu; kwani mkono wa Mungu ulikuwa mzito sana juu yake. 125:12 1Sam 4:8; Kut 11:6; Mit 21:13; Isa 15:3; Yer 25:34; Amo 5:17; Yak 2:13Wale ambao hawakufa walipatwa na majipu, na kilio cha mji kilikwenda juu hadi mbinguni.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

撒母耳記上 5:1-12

約櫃在非利士人手中

1非利士人將擄來的上帝的約櫃從以便以謝抬到亞實突城, 2把它抬進大袞廟,放在大袞神像旁邊。 3第二天早上,亞實突人起來,發現大袞神像倒在耶和華的約櫃前,面伏於地,他們就把大袞神像扶起來,放回原處。 4次日早上起來,他們又發現大袞神像倒在耶和華的約櫃前,面伏於地,頭和雙手都在門檻處折斷了,只剩下軀幹。 5因此,大袞的祭司和所有進亞實突大袞廟的人,至今都不踏廟的門檻。 6耶和華出手重重地懲罰亞實突及附近村莊的居民,使他們恐懼,都患上毒瘡。 7亞實突人見此情形,就說:「以色列上帝的約櫃不能留在我們這裡,因為上帝重重地懲罰我們和我們的大袞神。」 8亞實突人派人召集非利士所有的首領,問他們:「我們如何處理以色列上帝的約櫃?」他們答道:「把它送到迦特去。」於是,眾人把以色列上帝的約櫃送到迦特9約櫃抵達迦特後,耶和華出手攻擊那城,使那裡的男女老少都患了毒瘡,全城驚恐不已。 10於是,他們把約櫃送往以革倫以革倫人看見上帝的約櫃到了,就驚叫道:「他們把以色列上帝的約櫃帶來,是要害死我們和我們的人民!」 11他們派人召集非利士的首領,說:「把以色列上帝的約櫃送回原處吧,免得它殺害我們和我們的人民。」因為上帝重重地懲罰他們,全城都籠罩在死亡的恐懼中。 12那些沒有死的人都飽受毒瘡的折磨,城中的哭喊聲上達於天。