1 Samweli 31 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 31:1-13

Sauli Ajiua

(1 Nyakati 10:1-12)

131:1 1Sam 28:4; 1Nya 10:1-12; 1Sam 29:1; 1Nya 8:33Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika Mlima Gilboa. 231:2 1Sam 28:19; 18:1; 14:49; 1Nya 8:33Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua. 331:3 1Sam 28:4; 2Sam 1:6Mapigano yakawa makali sana kumzunguka Sauli, nao wapiga upinde wakampata na kumjeruhi vibaya.

431:4 Amu 9:54; Mwa 34:14; 1Sam 14:6; 2Sam 1:6, 10Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja wanichome na kunidhalilisha.”

Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia. 5Mchukua silaha wake alipoona Sauli amekufa, naye pia akaangukia upanga wake akafa pamoja naye. 631:6 1Sam 26:10; 12:25; 1Nya 10:6; Rum 6:23Basi Sauli, wanawe watatu, mbeba silaha wake na watu wake wote wakafa pamoja siku ile ile.

7Waisraeli waliokuwa kandokando ya bonde na wale waliokuwa ngʼambo ya Yordani walipoona kuwa jeshi la Waisraeli limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, wakaacha miji yao na kukimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.

831:8 2Sam 1:20Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe watatu wameanguka katika Mlima Gilboa. 931:9 1Sam 1:20; 4:4; Amu 16:24Wakamkata Sauli kichwa na kumvua silaha zake, nao wakatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari katika hekalu la sanamu zao na miongoni mwa watu wao. 1031:10 Amu 2:12-13; 1Sam 7:3; Yos 17:11; 2Sam 21:12; 1Sam 21:9; Amu 1:27Wakaweka silaha zake katika hekalu la Maashtorethi, na kukifunga kiwiliwili chake katika ukuta wa Beth-Shani.

1131:11 Amu 21:8; 1Sam 11:1Watu wa Yabeshi-Gileadi waliposikia yale Wafilisti walichomfanyia Sauli, 1231:12 Za 76:5; Mwa 38:24; Amo 6:10; 2Nya 16:14; 1Sam 11:1-11; 2Sam 2:4-7; Yer 34:5; Amo 6:10mashujaa wao wote wakaenda usiku hadi Beth-Shani. Wakauchukua mwili wa Sauli na miili ya wanawe kutoka kwenye ukuta wa Beth-Shani na kurudi hadi Yabeshi, mahali ambapo waliiteketeza kwa moto. 1331:13 2Sam 21:12-14; Mwa 21:33; 2Sam 3:35; 12:19-23; 1:12; Mwa 50:10; 1Sam 22:6; Mwa 50:10; Ay 2:13Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba.