1 Samweli 30 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 30:1-31

Daudi Aangamiza Waamaleki

130:1 1Sam 27:6-8; 29:4, 11; 15:7; Kut 17:8-16; Hes 24:20; Kum 25:17, 19; 1Nya 4:43; Eze 25:15Daudi na watu wake wakafika Siklagi siku ya tatu. Basi Waamaleki walikuwa wamevamia Negebu na Siklagi. Wakawa wameshambulia mji wa Siklagi na kuuteketeza kwa moto, 230:2 Ay 38:11; Za 76:10; 89:9; Isa 27:8; Hab 3:2nao wakawa wamewachukua mateka wanawake pamoja na wote waliokuwamo humo, vijana na wazee. Hawakuua yeyote, bali waliwachukua wakaenda zao.

330:3 Mwa 31:26Daudi na watu wake walipofika Siklagi, wakakuta mji umeangamizwa kwa moto na wake zao pamoja na wana wao na binti zao wamechukuliwa mateka. 430:4 Mwa 27:38; Hes 14:1Hivyo Daudi na watu wake wakapiga yowe mpaka wakaishiwa na nguvu za kulia. 530:5 1Sam 25:43; 2Sam 2:2Wake wawili wa Daudi walikuwa wametekwa: yaani Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. 630:6 Kut 17:4; Yn 8:59; Za 27:14; Rut 1:13; Rum 4:20; Amu 18:25; 2Sam 17:8; Za 17:8; Yer 17:7, 17; Yoe 3:16; Rum 4:20Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana juu ya kumpiga kwa mawe. Kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni kwa sababu ya wanawe na binti zake. Lakini Daudi akajitia nguvu katika Bwana, Mungu wake.

730:7 1Sam 22:20; 2:28; 23:9Kisha Daudi akamwambia kuhani Abiathari mwana wa Ahimeleki, “Niletee kisibau.” Abiathari akamletea, 830:8 1Sam 23:2; Mwa 14:16; Kut 2:17naye Daudi akamuuliza Bwana, “Je, nifuatie kundi hili la wavamizi? Je, nitawapata?”

Bwana akajibu, “Wafuatie. Hakika utawapata na utafanikiwa kuwaokoa.”

930:9 1Sam 27:2Daudi pamoja na watu wake 600 wakafika kwenye Bonde la Besori, mahali ambapo wengine waliachwa nyuma, 10kwa kuwa watu 200 walikuwa wamechoka sana kuweza kuvuka hilo bonde. Lakini Daudi pamoja na watu 400 wakaendelea kufuatia.

1130:11 Za 11:2; Mit 3:5, 6Wakamkuta Mmisri katika shamba fulani, nao wakamleta kwa Daudi. Wakampa huyo Mmisri maji ya kunywa na chakula; 1230:12 Amu 15:19; 1Sam 14:27kipande cha andazi la tini na andazi la zabibu zilizokaushwa. Akala naye akapata nguvu, kwa kuwa hakuwa amekula chakula chochote wala kunywa maji kwa siku tatu usiku na mchana.

1330:13 1Sam 14:48Daudi akamuuliza, “Wewe ni wa nani, na umetoka wapi?”

Akajibu, “Mimi ni Mmisri, mtumwa wa Mwamaleki. Bwana wangu alinitelekeza nilipougua siku tatu zilizopita. 1430:14 2Sam 8:18; 15:18; 20:2, 23; 1Fal 1:38, 44; 1Nya 18:17; Sef 2:5; Yos 14:13; 15:13Tulivamia Negebu ya Wakerethi, na nchi ya Yuda, na Negebu ya Kalebu. Nasi tulichoma moto Siklagi.”

1530:15 Kum 23:15Daudi akamuuliza, “Je, unaweza kuniongoza kufikia kundi hili la uvamizi?”

Akajibu, “Niapie mbele ya Mungu kwamba hutaniua wala kunikabidhi mikononi mwa bwana wangu, nami nitakupeleka hadi waliko.”

1630:16 Lk 12:19; Yos 22:830:16 Kut 32:6; 1Sam 25:36-38; 2Sam 13:28; Dan 5:1-4; Lk 12:19-20; 21:34; 1The 5:3; Ufu 11:10, 13Akamwongoza Daudi mpaka mahali walipokuwa, nao walikuwa wametawanyika eneo lote, wakila, wakinywa na wakifanya karamu kwa sababu ya nyara nyingi walizochukua kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka Yuda. 1730:17 1Sam 11:11; 2Sam 1:1; 15:3; 1:830:17 Ay 20:5Daudi akapigana nao kuanzia machweo ya jua hadi kesho yake jioni, na hakuna yeyote miongoni mwao aliyetoroka, isipokuwa vijana wanaume 400 waliopanda ngamia na kutoroka. 1830:18 Mwa 14:16; Za 34:9Daudi akarudisha kila kitu Waamaleki walikuwa wamechukua, pamoja na wake zake wawili. 19Hakuna chochote kilichopotea: kijana au mzee, mvulana au msichana, nyara au kitu kingine chochote walichokuwa wamechukua. Daudi akarudisha kila kitu. 20Akachukua makundi yote ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, nao watu wake wakawaswaga wanyama hao mbele ya wanyama wengine wa kufugwa, wakisema, “Hizi ni nyara za Daudi.”

2130:21 Amu 18:9Kisha Daudi akafika kwa wale watu 200 waliokuwa wamechoka sana kumfuata na ambao waliachwa nyuma kwenye Bonde la Besori. Wakatoka kwenda kumlaki Daudi na wale watu aliokuwa nao. Daudi na watu wake walipowakaribia, akawasalimu. 2230:22 Kum 13:13; Amu 19:22; 1Sam 22:2; 25:17; 1Fal 21:10Lakini watu wote waovu na wakorofi miongoni mwa wafuasi wa Daudi wakasema, “Kwa sababu hawakwenda pamoja nasi, hatutagawana nao nyara tulizorudisha. Lakini, kila mtu aweza kuchukua mkewe na watoto wake na kuondoka.”

23Daudi akajibu, “La hasha, ndugu zangu, kamwe hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho Bwana ametupatia. Yeye ametulinda na kuweka mikononi mwetu majeshi yale yaliyokuja kupigana dhidi yetu. 2430:24 Hes 31:27; Amu 5:30; Yos 22:8Ni nani atasikiliza yale mnayosema? Fungu la mtu aliyekaa na vyombo litakuwa sawa na la yule aliyekwenda vitani. Wote watashiriki sawa.” 25Daudi akafanya hili liwe amri na agizo kwa Israeli kutoka siku ile hata leo.

2630:26 Mwa 33:11Daudi alipofika Siklagi, akatuma baadhi ya nyara kwa wazee wa Yuda, waliokuwa rafiki zake, akasema, “Tazama, hapa kuna zawadi kwa ajili yenu kutoka nyara za adui za Bwana.”

2730:27 Yos 7:2; 10:40; 15:48; 19:8; Mwa 12:8; Yos 7:2; 10:40Akazituma kwa wale waliokuwa Betheli, Ramoth-Negebu na Yatiri; 2830:28 Hes 32:34; Yos 13:16; 1Nya 27:27; Yos 15:50kwa wale walioko Aroeri, Sifmothi, Eshtemoa 2930:29 1Sam 27:10; Amu 1:16; 1Sam 15:6na Rakali; kwa wale waliokuwa katika miji ya Wayerameeli na ya Wakeni; 3030:30 Hes 13:22; Yos 10:36; 14:13; 2Sam 2:1-4na kwa wale walioko Horma, Bori-Ashani, Athaki, 3130:31 Hes 13:22; Yos 10:36; 14:13; 2Sam 2:1-4na kwa wakazi wa Hebroni; na kwa wale waliokuwa mahali pengine pote ambako Daudi na watu wake walitembelea.