1 Samweli 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 3:1-21

Bwana Amwita Samweli

13:1 1Sam 2:11; Za 74:9; Mao 2:9; Eze 7:26; Amo 8:11Kijana Samweli alihudumu mbele za Bwana chini ya Eli. Katika siku zile neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi.

23:2 1Sam 4:15; Mwa 27:1Usiku mmoja Eli, ambaye macho yake yalikuwa yamefifia sana kiasi kwamba aliona kwa shida sana, alikuwa amelala mahali pake pa kawaida. 33:3 Kut 25:31-38; Law 24:1-4; 1Sam 1:9; Kum 10:1-5; 1Fal 6:19; 8:1Taa ya Mungu bado ilikuwa haijazimika, na Samweli alikuwa amelala Hekaluni3:3 Hekaluni maana yake ndani ya Maskani ya Bwana. mwa Bwana, ambapo Sanduku la Mungu lilikuwako. 43:4 Mwa 22:1; Kut 3:4Kisha Bwana akamwita Samweli.

Samweli akajibu, “Mimi hapa.” 5Naye akakimbia kwa Eli na kumwambia, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”

Lakini Eli akasema, “Sikukuita; rudi ukalale.” Hivyo akaenda kulala.

6Bwana akaita tena, “Samweli!” Naye Samweli akaamka, kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”

Eli akasema, “Mwanangu, sikukuita, rudi ukalale.”

73:7 1Sam 2:12; Hes 12:6; Mdo 19:2; Amo 3:7Wakati huu Samweli alikuwa bado hajamjua Bwana. Neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.

8Bwana akamwita Samweli mara ya tatu, naye Samweli akaamka kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”

Ndipo Eli akatambua kuwa Bwana alikuwa akimwita kijana. 9Hivyo Eli akamwambia Samweli, “Nenda ukalale, na kama akikuita, sema, ‘Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.’ ” Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake.

103:10 Kut 3:4; Za 85:8; Mdo 9:6Bwana akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!”

Kisha Samweli akasema, “Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.”

113:11 2Fal 21:12; Ay 15:21; Yer 19:3Naye Bwana akamwambia Samweli: “Tazama, nipo karibu kufanya kitu katika Israeli ambacho kitafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia yawashe. 123:12 1Sam 2:27-36Wakati huo nitatimiza dhidi ya Eli kila kitu nilichonena dhidi ya jamaa yake, kuanzia mwanzo mpaka mwisho. 133:13 1Fal 1:6; 1Sam 2:12Kwa kuwa nilimwambia kwamba ningehukumu jamaa yake milele kwa sababu ya dhambi aliyoijua, wanawe kumkufuru Mungu, naye akashindwa kuwazuia. 143:14 1Sam 2:25; Law 15:30-31; Isa 22:14; Hes 12:6; Yer 7:16; Ebr 10:26-31Kwa hiyo, nikaapa kuhusu nyumba ya Eli, ‘Hatia ya nyumba ya Eli kamwe haitaweza kufidiwa kwa dhabihu au sadaka.’ ”

153:15 1Sam 3:2Samweli akalala mpaka asubuhi, kisha akafungua milango ya nyumba ya Bwana. Aliogopa kumwambia Eli yale maono, 16lakini Eli akamwita na kumwambia, “Samweli mwanangu.”

Samweli akamjibu, “Mimi hapa.”

173:17 1Fal 22:14; Yer 23:28; 38:14; 42:4; Rut 1:17; 1:17; Mt 26:63Eli akamuuliza, “Ni nini alichokuambia? Usinifiche. Bwana na ashughulike nawe, tena kwa ukali, kama utanificha chochote alichokuambia.” 183:18 Amu 10:15; 2:16; Mwa 18:25; 1Sam 16:10-12; Isa 39:8; 1Pet 5:6Kwa hiyo Samweli akamwambia kila kitu, bila kumficha chochote. Ndipo Eli akasema, “Yeye ni Bwana; na afanye lile lililo jema machoni pake!”

193:19 Mwa 21:22; Hes 14:43; Amu 13:24; 1Sam 9:6; Mwa 39:2Bwana alikuwa pamoja na Samweli alipokuwa akikua, na hakuacha hata moja ya maneno yake lianguke chini. 203:20 Amu 20:1; Kum 18:22; Eze 33:33; Amu 20:1Nao Israeli wote kuanzia Dani hadi Beer-Sheba wakatambua kuwa Samweli amethibitishwa kuwa nabii wa Bwana. 213:21 Mwa 12:7; Hes 12:6; Amo 3:7Bwana akaendelea kutokea huko Shilo, na huko kujidhihirisha kwa Samweli kwa njia ya neno lake.