1 Samweli 26 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 26:1-25

Daudi Amwacha Sauli Hai Tena

126:1 1Sam 23:19; Za 54; 1Sam 23:24Hao Wazifu wakamwendea Sauli huko Gibea na kusema, “Je, Daudi hakujificha katika kilima cha Hakila, kinachotazamana na Yeshimoni?”

226:2 1Sam 24:2; 13:2Hivyo Sauli akashuka kwenda katika Jangwa la Zifu, akiwa na watu wake 3,000 wa Israeli waliochaguliwa, kumsaka Daudi huko. 326:3 1Sam 12:19Sauli akapiga kambi yake kando ya barabara juu ya kilima cha Hakila kinachotazamana na Yeshimoni, lakini Daudi alikuwa anaishi huko jangwani. Alipoona kuwa Sauli amemfuata huko, 4Daudi akatuma wapelelezi na akapata habari kwa hakika kwamba Sauli alikuwa amewasili.

526:5 1Sam 17:55; 14:50Ndipo Daudi akaondoka, akaenda hadi mahali Sauli alikuwa amepiga kambi. Akaona mahali Sauli na Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi, walipokuwa wamelala. Sauli alikuwa amelala ndani ya kambi, jeshi likiwa limemzunguka.

626:6 Mwa 10:15; 2Sam 2:18; 10:10; 16:9; 18:2; 19:21; 23:18; 1Nya 11:20; 19:11; 2:16; Amu 7:10-11Basi Daudi akamuuliza Ahimeleki Mhiti, na Abishai mwana wa Seruya, nduguye Yoabu, akisema, “Ni nani atakayeshuka pamoja nami kambini kwa Sauli?”

Abishai akajibu, “Nitakwenda pamoja nawe.”

7Hivyo Daudi na Abishai wakaenda kwenye jeshi wakati wa usiku, tazama Sauli, alikuwa amelala ndani ya kambi na mkuki wake umekitwa ardhini karibu na kichwa chake. Abneri na askari walikuwa wamelala kumzunguka Sauli.

826:8 1Sam 24:18Abishai akamwambia Daudi, “Leo Mungu amemtia adui yako mikononi mwako. Sasa niruhusu nimchome mpaka ardhini kwa pigo moja la mkuki wangu; sitamchoma mara mbili.”

926:9 Mwa 26:11; 1Sam 9:16; 2Sam 1:14; 19:21; Mao 4:20; 1Sam 24:5Lakini Daudi akamwambia Abishai, “Usimwangamize! Ni nani awezaye kutia mkono juu ya mpakwa mafuta wa Bwana na asiwe na hatia?” 1026:10 Mwa 16:5; 1Sam 25:38; Rum 12:19; Za 37:13; 31:6; 2Sam 1:1; Za 94:1, 2, 23; Mit 20:22; Lk 18:7; Rum 12:19; Ebr 10:30; Ufu 18:8; Kum 31:14; Ay 7:1; 14:5Daudi akasema, “Hakika kama vile Bwana aishivyo, Bwana mwenyewe atampiga; au wakati wake utafika, naye atakufa, au atakwenda vitani na kuangamia. 1126:11 Law 19:8; 1Sam 24:6, 12; Mit 24:29; Rum 12:17, 19; Yak 5:5-11; 1Pet 3:9Lakini Mungu na apishie mbali nisije nikainua mkono juu ya mpakwa mafuta wa Bwana. Sasa chukua huo mkuki na hilo gudulia la maji vilivyo karibu na kichwa chake, tuondoke.”

1226:12 Amu 4:21; Mwa 2:21; Es 6:1; Isa 29:10Hivyo Daudi akachukua huo mkuki na hilo gudulia la maji vilivyokuwa karibu na kichwa cha Sauli, nao wakaondoka. Hakuna yeyote aliyeona au kufahamu habari hii, wala hakuna hata mmoja aliyeamka usingizini. Wote walikuwa wamelala, kwa sababu Bwana alikuwa amewatia kwenye usingizi mzito.

13Kisha Daudi akavuka upande mwingine na kusimama juu ya kilima mahali palipokuwa na nafasi pana kati yao. 14Daudi akalipigia kelele jeshi na Abneri mwana wa Neri, akisema, “Je, Abneri, hutanijibu?”

Abneri akajibu, “Nani wewe umwitaye mfalme?”

15Daudi akasema, “Wewe si ni mtu shujaa? Ni nani aliye kama wewe katika Israeli? Kwa nini basi hukumlinda mfalme bwana wako? Mtu mmoja alikuja kumwangamiza mfalme, bwana wako. 16Ulichokifanya si kizuri. Kwa hakika kama aishivyo Bwana, wewe na watu wako mnastahili kufa, kwa sababu hamkumlinda bwana wenu, mpakwa mafuta wa Bwana. Tazameni hapo mlipo. Uko wapi mkuki wa mfalme na gudulia la maji ambavyo vilikuwa karibu na kichwa chake?”

1726:17 1Sam 24:16Sauli akatambua sauti ya Daudi, na kusema, “Je, hiyo ni sauti yako, Daudi mwanangu?”

Daudi akajibu, “Naam, hiyo ndiyo, bwana wangu mfalme.” 1826:18 Ay 13:23; Yer 37:18; 1Sam 24:9, 11; Za 7:3Pia akaongeza, “Kwa nini bwana wangu anamfuatia mtumishi wake? Nimefanya nini, nalo kosa langu ni lipi nililolifanya niwe na hatia? 1926:19 1Sam 24:9; 2Sam 16:11; Kum 20:16; 2Sam 14:16; 20:19; 21:3; Kum 4:28; 11:28; Za 120:5; Kut 15:17; Kum 4:20; 9:26; Za 106:4, 5; Isa 19:25Sasa mfalme bwana wangu na asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama Bwana amekuchochea dhidi yangu, basi yeye na aipokee sadaka yangu. Lakini hata hivyo, kama ni wanadamu waliofanya hivyo, walaaniwe mbele za Bwana! Wao sasa wamenifukuza kutoka sehemu yangu katika urithi wa Bwana wangu wakisema, ‘Nenda ukatumikie miungu mingine.’ 2026:20 1Sam 24:11; 24:14; Yer 4:29; 16:16; Amo 9:3Basi usiache damu yangu imwagike kwenye ardhi mbali na uso wa Bwana. Mfalme wa Israeli ametoka kutafuta kiroboto, kama vile mtu awindavyo kware katika milima.”

2126:21 Kut 9:27; Za 72:14; 1Sam 15:24; 24:17; Hes 22:34; 1Sam 15:24; 24:17; Mt 27:4Ndipo Sauli akasema, “Nimetenda dhambi. Rudi, Daudi mwanangu. Kwa kuwa uliyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani leo, sitajaribu kukudhuru tena. Hakika nimetenda kama mpumbavu na nimekosa sana.”

22Daudi akajibu, “Mkuki wa mfalme uko hapa. Mmoja wa vijana wako na avuke kuuchukua. 2326:23 Mwa 16:5; Rut 2:21; Za 62:12; 2Sam 22:21-25; Za 18:20-24; 1Sam 24:18; Mhu 8:12; Isa 3:10-11Bwana humlipa kila mtu kwa ajili ya haki yake na uaminifu wake. Bwana alikutia katika mikono yangu leo, lakini sikuinua mkono wangu juu ya mpakwa mafuta wa Bwana. 2426:24 Za 54:7Kwa hakika kama vile maisha yako yalivyokuwa ya thamani kwangu leo, vivyo hivyo maisha yangu na yawe na thamani kwa Bwana na kuniokoa kutoka taabu zote.”

2526:25 Rut 2:12Ndipo Sauli akamwambia Daudi, “Mwanangu Daudi na ubarikiwe; utafanya mambo makubwa na hakika utashinda.”

Basi Daudi akaenda zake, naye Sauli akarudi nyumbani.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒母耳记上 26:1-25

大卫再次放过扫罗

1西弗人到基比亚扫罗,说:“大卫正躲在旷野附近的哈基拉山中。” 2扫罗就带领三千以色列精兵到西弗的旷野去追捕大卫3他们在旷野附近路边的哈基拉山上扎营。大卫在旷野听说扫罗追来了, 4就派人去打探消息,得知扫罗的追兵果然已到。 5大卫来到扫罗的营地,看见了他和他的元帅尼珥的儿子押尼珥睡觉的地方,他睡在军营中间,其他人围绕着他扎营。 6大卫亚希米勒洗鲁雅的儿子约押的兄弟亚比筛:“谁愿意跟我到扫罗的营里?”亚比筛答道:“我愿意。” 7大卫亚比筛就趁夜间走进扫罗的军营,发现扫罗正在熟睡,他的矛插在地上,靠近他的头,押尼珥和其他人睡在他周围。 8亚比筛大卫说:“现在上帝把你的敌人交在你手中了,让我一矛把他钉在地上,决不用刺第二下。” 9大卫却说:“不要杀他,谁杀害耶和华所膏立的王,都难逃罪责。 10我凭永活的耶和华起誓,耶和华必亲手击杀他。他要么寿终而死,要么命丧沙场。 11我在耶和华面前绝不敢出手伤害祂所膏立的王。我们拿走他旁边的矛和水瓶吧。” 12大卫拿上扫罗的矛和水瓶便同亚比筛离开了,没有人看见,没有人知道,他们都在沉睡,没有人醒来,因为耶和华使他们都熟睡了。

13大卫爬上营地对面的山坡,远远地站在山顶上,与他们相距很远。 14他呼喊扫罗的士兵和尼珥的儿子押尼珥:“押尼珥,你回答我!”押尼珥问道:“你是谁,竟敢在王面前喊叫?” 15大卫说:“你不是勇士吗?在以色列有谁比得上你呢?有人来刺杀你的王你的主,你为何没有保护他呢? 16你失职了。我凭永活的耶和华起誓,你们都该死。因为你们没有保护你们的主——耶和华所膏立的王。你看看王头旁的矛和水瓶在哪里?”

17扫罗听出是大卫的声音,就说:“我儿大卫!是你吗?”大卫答道:“我主我王啊,是我。 18我主为什么又要追杀仆人呢?我做错了什么,犯了什么罪? 19我主我王,请听仆人说,如果是耶和华使你与我作对,愿祂悦纳我献上的祭物;如果这是出于人的主意,愿他们在耶和华面前受咒诅。因为他们赶我离开耶和华所赐的产业,叫我去供奉其他神明。 20求你不要让我死在远离耶和华的异乡!以色列王为何要像在山上猎杀鹧鸪一样追捕一只跳蚤呢?”

21扫罗说:“我犯罪了。我儿大卫,你回来吧,我不会再伤害你,因为你今日保存了我的性命。我真是糊涂,犯了大错。” 22大卫答道:“王的矛在这里,请派一个人来拿回去吧。 23耶和华奖赏公义、信实的人。今天耶和华把你交在我手中,但我不愿下手伤害耶和华所膏立的王。 24我今天保存了你的性命,愿耶和华也保存我的性命,救我脱离一切患难。” 25扫罗大卫说:“我儿大卫,愿你蒙福。你一定能建功立业,战胜仇敌。”于是,大卫起身离开,扫罗也回家去了。