1 Samweli 25 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 25:1-44

Daudi, Nabali Na Abigaili

125:1 1Sam 28:3; Law 10:6; Hes 20:29; Kum 34:8; Mwa 21:2; 1Sam 7:17; 2Nya 33:20Basi Samweli akafa, nao Israeli wote wakakusanyika na kumwombolezea; wakamzika nyumbani kwake huko Rama.

Kisha Daudi akateremka kwenye Jangwa la Maoni. 225:2 Yos 15:55; 2Sam 19:32; Mwa 31:19; 1Sam 23:24; Mwa 38:13; 2Sam 13:23Mtu mmoja huko Maoni, aliyekuwa na makao huko Karmeli, alikuwa tajiri sana. Alikuwa na mbuzi elfu moja na kondoo elfu tatu, aliokuwa akiwakata manyoya huko Karmeli. 325:3 Mit 31:10; Yos 14:13; 15:13; Rut 4:11; Mit 14:1; 24:3, 4; Isa 32:5, 7Jina la mtu huyo lilikuwa Nabali, naye mkewe aliitwa Abigaili. Alikuwa mwanamke mwenye busara na mzuri wa sura, lakini mumewe, ambaye alikuwa wa ukoo wa Kalebu, alikuwa mwenye hasira na mchoyo katika utendaji wake.

425:4 Mwa 38:13; 2Sam 13:23Daudi alipokuwa huko jangwani, akasikia kuwa Nabali alikuwa anakata kondoo manyoya. 525:5 1Sam 18:28; Lk 10:5Basi akatuma vijana kumi na kuwaambia, “Pandeni kwa Nabali huko Karmeli, mkamsalimie kwa jina langu. 625:6 Za 122:7; Mt 10:12; 1Nya 12:18Mwambieni: ‘Amani iwe kwako! Amani iwe kwako pamoja na wa nyumbani mwako! Pia amani iwe pamoja na vyote ulivyo navyo!

7“ ‘Nasikia kuwa huu ni wakati wa kukata kondoo manyoya. Wachunga mifugo wako walipokuwa pamoja nasi, hatukuwatendea mabaya na wakati wote waliokuwa huko Karmeli hakuna chochote chao kilipotea. 825:8 Neh 8:10; Es 9:19Waulize watumishi wako nao watakuambia. Kwa hiyo uwatendee wema vijana wangu, kwani tumekuja wakati wa furaha. Tafadhali wape watumishi wako na mwanao Daudi chochote kitakachokuja mkononi mwako kwa ajili yao.’ ”

9Watu wa Daudi walipofika wakampa Nabali ujumbe huu kwa jina la Daudi. Kisha wakangojea.

1025:10 Amu 9:28; Za 73:7, 8; 123:3, 4Nabali akawajibu watumishi wa Daudi, “Huyu Daudi ni nani? Huyu mwana wa Yese ni nani? Watumishi wengi wanakimbia kutoka kwa bwana zao siku hizi. 1125:11 Amu 8:6Kwa nini nichukue mkate wangu, maji yangu na nyama niliyochinja kwa ajili ya wakata manyoya wangu, na kuwapa watu ambao hakuna anayejua wanakotoka?”

12Watu wa Daudi wakageuka na kurudi. Walipofika, wakaarifu kila neno. 1325:13 1Sam 22:2; 21:10; 23:13; 30:24; Hes 31:27Daudi akawaambia watu wake, “Jifungeni panga zenu!” Basi wakajifunga panga zao, naye Daudi akajifunga upanga wake. Watu kama mia nne hivi wakapanda pamoja na Daudi, na watu mia mbili wakabaki na vifaa.

1425:14 1Sam 13:10Mmoja wa watumishi akamwambia Abigaili, mkewe Nabali: “Daudi alituma wajumbe kutoka jangwani kumpa bwana wetu salamu zake, lakini akawavurumishia matukano. 15Hata hivyo watu hawa walikuwa wema sana kwetu. Hawakututendea mabaya, na wakati wote tulipokuwa nje huko mashambani karibu nao, hatukupotewa na kitu chochote. 1625:16 Kut 14:22; Ay 1:10; Za 139:5; Zek 2:5Usiku na mchana walikuwa ukuta wakituzunguka wakati wote tulipokuwa tukichunga kondoo zetu karibu nao. 1725:17 Kum 13:13; 1Sam 20:7Sasa fikiri juu ya jambo hili na uone unaweza kufanya nini, kwa sababu maafa yanakaribia juu ya bwana wetu na nyumba yake yote. Yeye ni mtu mwovu kiasi kwamba hakuna mtu awezaye kuzungumza naye.”

1825:18 Law 23:14; 1Sam 17:17; 1Nya 12:40; Mwa 42:26; 2Sam 16:1; Isa 30:6Abigaili akafanya haraka, akachukua mikate mia mbili, viriba viwili vya divai, kondoo watano waliochinjwa vipimo vitano vya bisi, vishada mia moja vya zabibu kavu, mikate mia mbili ya tini, akavipakia juu ya punda. 1925:19 Mwa 32:20; 1Sam 25:36Kisha akawaambia watumishi wake, “Tangulieni; mimi nitakuja nyuma yenu.” Lakini hakumwambia Nabali mumewe.

20Ikawa alipokuwa amepanda punda wake kwenye bonde la mlima, tazama, Daudi na watu wake wakawa wanateremka kumwelekea, naye akakutana nao. 2125:21 Za 109:5; 1Sam 19:4; Mwa 44:4; Za 35:12; Mit 17:13; Yer 18:20; 1Pet 2:20; 3:17Daudi alikuwa amesema, “Ilikuwa ni kazi bure kuchunga kwangu kote mali za huyu mtu huko jangwani hivi kwamba hakuna chochote chake kilichopotea. Yeye amenilipa baya kwa ajili ya wema. 2225:22 Rut 1:17; 1Fal 14:10; 21:21; 2Fal 9:8; 1Sam 20:13Bwana na amshughulikie Daudi, tena kwa ukali, ikiwa kesho asubuhi nitambakizia mwanaume hata mmoja aliye hai miongoni mwa watu wake wote!”

2325:23 Mwa 19:1; 1Sam 20:41; Yos 15:18; Amu 1:14Abigaili alipomwona Daudi, akashuka haraka kwenye punda wake, akainama kifudifudi uso wake mpaka nchi mbele ya Daudi. 2425:24 2Sam 14:9Akamwangukia miguuni pake na kusema: “Bwana wangu, kosa hili na liwe juu yangu mwenyewe. Tafadhali mruhusu mtumishi wako aseme nawe. Sikia kile mtumishi wako atakachosema. 2525:25 Mit 17:12; 12:16; 14:16; 20:3; Isa 32:5Bwana wangu na asimjali huyo mtu mwovu Nabali. Yeye anafanana na jina lake; jina lake ni Mpumbavu, nao upumbavu huenda pamoja naye. Lakini kwangu mimi, mtumishi wako, sikuwaona hao watu waliotumwa na bwana wangu.

2625:26 Ebr 10:30; 2Sam 18:32; 2Fal 2:2; Mwa 20:6; Rum 12:19; 2Sam 18:32“Basi sasa, kwa kuwa Bwana amekuzuia, wewe bwana wangu, kutokumwaga damu na kutolipiza kisasi kwa mikono yako mwenyewe, hakika kama Bwana aishivyo na kama uishivyo, maadui zako na wote wanaokusudia kumdhuru bwana wangu wawe kama Nabali. 2725:27 Mwa 33:11; 1Sam 30:26Nayo zawadi hii ambayo mtumishi wako amemletea bwana wangu, wapewe watu wanaofuatana nawe. 2825:28 2Sam 14:9; 7:11, 26; 1Sam 18:17; 24:11; 1Fal 9:5; 1Nya 17:16Tafadhali samehe kosa la mtumishi wako, kwa kuwa Bwana kwa hakika ataifanya imara nyumba ya ufalme kwa bwana wangu, kwa sababu anapigana vita vya Bwana. 2925:29 1Sam 20:1; Yer 10:18; 22:26; 1Sam 17:50; 2Sam 4:8; Za 66:9; Mit 10:29, 30; Mdo 17:28Hata ingawa yuko mtu anayekufuatia kuuondoa uhai wako, usiruhusu baya lolote kuonekana kwako siku zote za maisha yako, uhai wa bwana wangu utafungwa salama kwenye furushi la walio hai na Bwana Mungu wako. Lakini uhai wa adui zako atavurumishwa kama vile jiwe kutoka kwenye kombeo. 3025:30 1Sam 12:12; 13:14Bwana atakapokuwa ameshamtendea bwana wangu kila kitu chema alichoahidi kumhusu yeye na kumweka kuwa kiongozi wa Israeli, 3125:31 Mwa 40:14; 2Sam 3:10bwana wangu hatakuwa na dhamiri inayolemewa na mzigo kwa kumwaga damu kusiko na sababu, au kujilipizia kisasi yeye mwenyewe. Bwana atakapomletea bwana wangu mafanikio, umkumbuke mtumishi wako.”

3225:32 Mwa 24:27; Kut 18:10; Lk 1:68; Ezr 7:27; Za 41:12, 13; 72:18; 2Kor 8:16Daudi akamwambia Abigaili, “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli aliyekutuma kunilaki leo. 33Ubarikiwe kwa uamuzi wako mzuri na kwa kunizuia nisimwage damu leo na kulipiza kisasi kwa mikono yangu. 34La sivyo, hakika kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye amenizuia nisiwadhuru, kama usingekuja haraka kunilaki, hakuna hata mwanaume mmoja wa Nabali angeachwa hai kufikia mapambazuko.”

3525:35 Mwa 19:21; 2Fal 5:19; 1Sam 20:42; 2Sam 15:9; Lk 7:50Ndipo Daudi akapokea kutoka mkononi mwake kile alichokuwa amemletea, naye akasema, “Nenda nyumbani kwako kwa amani; nimesikia maneno yako na kukujalia ombi lako.”

3625:36 Rut 3:7; Mit 20:1; Mhu 10:17; Isa 5:11, 22; 22:13; 28:7; 56:12; Hos 4; 11; 2Sam 13:23Abigaili alipokwenda kwa Nabali, alikuwa ndani ya nyumba yake akifanya karamu kama ile ya mfalme. Naye alikuwa ana furaha nyingi, akiwa amelewa sana. Kwa hiyo Abigaili hakumwambia mumewe kitu chochote mpaka asubuhi yake. 3725:37 Kut 15:16; Kum 28:28; Ay 15:21Basi asubuhi, Nabali alipokuwa amelevuka, mkewe akamwambia mambo yote, nao moyo wake ukazimia, akawa kama jiwe. 3825:38 Kum 32:35; 1Sam 24:12; 26:10; 2Sam 6:7; 12:15; Kut 12:29; 2Sam 6:7; Ay 12:10; Za 104:29; Mdo 12:23Baada ya siku kumi, Bwana akampiga Nabali, naye akafa.

3925:39 Mit 22:23; 2Sam 3:28, 29; 1Fal 2:44; Es 7:10; Za 7:16Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, akasema, “Ahimidiwe Bwana, ambaye amenitetea shauri langu dhidi ya Nabali kwa kuwa alinitendea kwa dharau. Amemzuia mtumishi wake asitende mabaya na Bwana ameuleta ubaya wa Nabali juu ya kichwa chake mwenyewe.”

Kisha Daudi akatuma ujumbe kwa Abigaili kumwomba awe mke wake. 40Watumishi wa Daudi wakaenda mpaka Karmeli na kumwambia Abigaili, wakisema, “Daudi ametutuma kwako kukuchukua uwe mkewe.”

4125:41 Rut 2:10, 13; Mit 15:33; 18:12Akainama chini uso wake mpaka ardhini, akasema, “Mjakazi wako yuko hapa, tayari kuwatumikia na kuwanawisha miguu watumishi wa bwana wangu.” 4225:42 2Sam 2:2; 3:3; 1Nya 3:1Abigaili akainuka kwa haraka, akapanda punda wake, akihudumiwa na wajakazi wake watano, akaenda pamoja na wajumbe wa Daudi, naye akawa mkewe. 4325:43 2Sam 3:2; 1Nya 3:1; 1Sam 30:5; 2Sam 2:2; Yos 15:56Pia Daudi alikuwa amemwoa Ahinoamu wa Yezreeli, wote wawili wakawa wake zake. 4425:44 2Sam 3:15; Isa 10:30Lakini Sauli alikuwa amemwoza Mikali binti yake, aliyekuwa mkewe Daudi, kwa Palti mwana wa Laishi, kutoka Galimu.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒母耳记上 25:1-44

大卫与亚比该

1撒母耳死了,以色列人都聚在一起哀悼他,把他安葬在拉玛他自己的坟地里。之后,大卫到了巴兰的旷野。 2玛云有个富翁拥有三千只绵羊和一千只山羊,他的产业在迦密。当时他正在迦密剪羊毛。 3他名叫拿八,是迦勒族人,妻子名叫亚比该,既聪慧又漂亮。拿八粗暴凶恶。 4大卫在旷野得知拿八正在剪羊毛, 5就派十个部下到迦密去见拿八,吩咐他们以他的名义向拿八问安, 6拿八说:“愿你和你全家平安,愿你一切顺利! 7我听说你正在剪羊毛。你的牧人与我们在迦密的时候,我们没有欺负过他们,他们没有丢过任何东西。 8你问问你的仆人就知道了。请你恩待我的部下,因为今天是好日子,求你随手赏一点东西给仆人们和晚辈我。”

9大卫的部下就去把大卫的话告诉拿八,等候他的答复。 10拿八说:“大卫是谁?耶西的儿子是谁?这些日子有很多仆人逃离主人, 11我怎能把饼、水和为剪羊毛者预备的肉分给一群来历不明的人呢?” 12大卫的部下回去把拿八的话禀告大卫13大卫听了,就吩咐众人备刀,他自己也带了刀去拿八那里。大卫带了四百人去,留下二百人看守辎重。

14拿八的一个仆人告诉拿八的妻子亚比该说:“大卫从旷野派人来向我们主人问安,主人却辱骂他们。 15那些人对我们很好,从来不欺负我们。我们跟他们一起在田野的时候,从来没有丢过任何东西。 16我们在他们附近牧羊的时候,他们昼夜不断地保护我们。 17所以,请你赶快想个法子,不然主人和他全家恐怕都会大难临头。主人是个凶暴的人,没有人敢跟他说话。”

18亚比该连忙用驴驮上二百块饼、两皮袋酒、五只宰好了的羊、三十七升烤麦、一百块葡萄饼和二百块无花果饼, 19又吩咐仆人说:“你们先去吧!我随后就来。”她没有把这事告诉丈夫拿八20她骑着驴下山的时候,就看见大卫和他的部下迎面而来。 21大卫曾说:“我在旷野保护这人的羊群,使它们不致丢失,真是枉费功夫。他竟以怨报德。 22如果我让他家里一个男子活到明早,愿上帝重重地惩罚我!”

23亚比该看见大卫,连忙下驴俯伏下拜。 24她俯伏在大卫脚前说:“我主啊,我愿意承担一切罪过,请听婢女说。 25请不要理会拿八那个恶徒,他人如其名25:25 “拿八”意思是“愚蠢”。,是个名符其实的蠢人。当时婢女没有见到你派来的使者。 26我主啊,既然耶和华阻止你亲手杀人报仇,我就凭永活的耶和华和你的性命起誓,愿你的仇敌和伤害你的人都像拿八一样没有好下场。 27现在,请把婢女带来的礼物分给你的部下吧。 28请饶恕婢女的罪过,耶和华必使你的子孙世代做王,因为你是在为耶和华而战,愿你一生没有过错。 29你就是被人追杀,也会在你的上帝耶和华的保护下安然无恙。你敌人的性命却要像石头一样被耶和华用投石器抛出去。 30-31如果你现在没有杀人报仇,伤害无辜,到了耶和华照应许赐福给你、立你做以色列王的时候,你就不会心里不安了。我主啊,耶和华赐福给你的时候,求你不要忘了婢女。”

32大卫亚比该说:“以色列的上帝耶和华当受称颂!祂今天派你来见我。 33你很有见识,你今天拦阻我亲手杀人复仇,值得称赞。 34我凭阻止我杀你的以色列的上帝——永活的耶和华起誓,若不是你赶来迎接我,拿八家中不会有一个男子活到明天早上。” 35大卫接受了亚比该的礼物,对她说:“安心回家吧,我答应你的请求。”

36她回到家时,拿八正在大摆宴席,排场如御宴。她见拿八心情愉快,喝得酩酊大醉,就什么也没告诉他,等第二天早上再说。 37次日清晨,拿八酒醒以后,他妻子把发生的一切告诉他,他吓得昏死过去,身体僵硬如石。 38过了十天,耶和华击打拿八,他就死了。

39大卫听见拿八的死讯,就说:“赞美耶和华!拿八羞辱我,祂为我申了冤,又阻止仆人行恶。祂使拿八得到了报应。”后来,大卫差遣使者去向亚比该求婚。 40他的使者就启程到迦密去向亚比该传达大卫的心意。 41亚比该听了,立刻俯伏在地上说:“婢女愿意效劳,为我主的仆人洗脚。” 42她连忙骑上驴,带了五个侍女,跟随大卫的使者前去,做了大卫的妻子。 43大卫已经娶了耶斯列亚希暖,她们二人就同做大卫的妻子。 44扫罗已经把自己的女儿、大卫的妻子米甲嫁给了迦琳拉亿的儿子帕提