1 Samweli 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 23:1-29

Daudi Aokoa Keila

123:1 Yos 15:44; Hes 18:27; Amu 6:11Daudi alipoambiwa kuwa, “Tazama, Wafilisti wanapigana dhidi ya Keila nao wanapokonya nafaka katika sakafu za kupuria,” 223:2 1Sam 22; 10; 30:8; 2:1; 2Sam 5:19; Za 50:19; Hes 27:21; Amu 1:1; 1Sam 28:6; 30:8; 1Nya 10:14; 14:10; Za 32:8; 37:5; Mit 3:5, 6; Yer 10:23; Yak 1:5akauliza kwa Bwana, akisema, “Je, niende na kuwashambulia hawa Wafilisti?”

Bwana akamjibu, “Nenda, washambulie Wafilisti na uuokoe Keila.”

3Lakini watu wa Daudi wakamwambia, “Hapa Yuda kwenyewe tunaogopa. Si zaidi sana, kama tukienda Keila dhidi ya majeshi ya Wafilisti!”

423:4 1Sam 9:16; Yos 8:7; Amu 7:7Daudi akauliza kwa Bwana tena, naye Bwana akamjibu akamwambia, “Shuka uende Keila, kwa kuwa nitawatia Wafilisti mkononi mwako.” 5Basi Daudi na watu wake wakaenda Keila, wakapigana na Wafilisti na kutwaa wanyama wao wa kutosha. Daudi akawatia hasara kubwa Wafilisti na kuwaokoa watu wa Keila. 623:6 1Sam 22:20; 2:28; Ay 1:15-19(Basi Abiathari mwana wa Ahimeleki alikuwa ameleta kisibau alipokimbilia kwa Daudi huko Keila.)

Sauli Anamfuata Daudi

723:7 Kum 32:30; Za 31:21; Kut 15:9; 1Sam 24:4-6; 26:8, 9; Za 79:11Sauli akaambiwa kwamba Daudi alikuwa amekwenda Keila, naye akasema, “Mungu amemtia mkononi mwangu, kwa kuwa Daudi amejifunga mwenyewe kwa kuingia kwenye mji wenye malango na makomeo.” 8Naye Sauli akayaita majeshi yake yote yaende vitani, kuishukia Keila ili kumzingira Daudi na watu wake kwa jeshi.

923:9 1Sam 22:20; 2:28; 30:7Daudi alipojua kuwa Sauli alikuwa ana hila dhidi yake, akamwambia Abiathari kuhani, “Leta kile kisibau.” 1023:10 1Sam 22:19; 2Sam 20:20; Es 3:6; Za 44:22Daudi akasema, “Ee Bwana, Mungu wa Israeli, mtumishi wako amesikia kwa hakika kwamba Sauli anapanga kuja Keila na kuangamiza mji kwa ajili yangu. 11Je, watu wa Keila watanisalimisha kwake? Je, Sauli atateremka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, mwambie mtumishi wako.”

Naye Bwana akasema, “Ndiyo, atashuka.”

12Daudi akauliza tena, “Je watu wa Keila watanisalimisha mimi pamoja na watu wangu kwa Sauli?”

Naye Bwana akasema, “Ndiyo, watafanya hivyo.”

1323:13 1Sam 22:2; 25:13Basi Daudi na watu wake, wapatao 600, wakaondoka Keila wakawa wanakwenda sehemu moja hadi nyingine. Sauli alipoambiwa Daudi ametoroka kutoka Keila, hakwenda huko.

1423:14 Za 55:7; Yos 15:24; Za 54:3-4; 32:7; 11:1; Yos 15:55; 1Sam 27:1; Mit 1:16; 4:16; Kum 33:3; 1Sam 2:9; Za 32:7; 33:18; Mit 2:8; Rum 8:31; 2Tim 3:11; 4:17, 18Daudi akakaa katika ngome za jangwani na katika vilima vya Jangwa la Zifu. Siku baada ya siku Sauli aliendelea kumsaka, lakini Mungu hakumtia Daudi mikononi mwake.

1523:15 1Sam 20:1Daudi alipokuwa huko Horeshi katika Jangwa la Zifu, akajua kuwa Sauli alikuwa amekuja ili amuue. 1623:16 1Sam 30:6; Za 18:2; 27:14Naye Yonathani mwana wa Sauli akamwendea Daudi huko Horeshi na kumtia moyo kusimama imara katika imani yake kwa Mungu. 1723:17 1Sam 20:31; 24:20Akamwambia, “Usiogope, Daudi; baba yangu Sauli hatakutia mkononi mwake. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, nami nitakuwa wa pili wako. Hata baba yangu Sauli anajua hili.” 1823:18 1Sam 18:3; 2Sam 9:1; 21:7Wote wawili wakaweka agano mbele za Bwana. Kisha Yonathani akaenda zake nyumbani, lakini Daudi akabaki Horeshi.

1923:19 1Sam 26:1; Za 54; 1Sam 26:3Basi Wazifu wakakwea kwa Sauli huko Gibea na kusema, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu katika ngome huko Horeshi, katika kilima cha Hakila, kusini mwa Yeshimoni? 20Sasa, ee mfalme, uteremke wakati wowote unapoona vyema kufanya hivyo, sisi tutawajibika kumkabidhi kwa mfalme.”

2123:21 Rut 2:20; 2Sam 2:5; 1Sam 22:8Sauli akajibu, “Bwana awabariki kwa kunifikiria. 22Nendeni mkafanye maandalizi zaidi. Mkajue mahali ambapo Daudi huenda mara kwa mara na nani amepata kumwona huko. Wananiambia yeye ni mwerevu sana. 2323:23 Mwa 31:36Jueni kila mahali anapojificha mrudi na kunipa taarifa kamili. Kisha nitakwenda pamoja nanyi; kama atakuwa katika eneo hilo, nitamsaka miongoni mwa koo zote za Yuda.”

2423:24 Yos 15:55; 1Sam 26:1; 25:2Basi wakaondoka na kwenda mpaka Zifu wakimtangulia Sauli. Naye Daudi na watu wake walikuwa katika Jangwa la Maoni, katika Araba kusini mwa Yeshimoni. 25Sauli na watu wake wakaanza msako, naye Daudi alipoelezwa hili, akateremka mpaka mwambani na kukaa katika Jangwa la Maoni. Sauli aliposikia hili, akaenda katika Jangwa la Maoni akimfuata Daudi.

2623:26 Za 17:6; 1Sam 19:12; 20:38; 2Sam 15:14; Za 31:22; 2Nya 20:12; 2Kor 1:8Sauli alikuwa akienda upande mmoja wa mlima, naye Daudi na watu wake walikuwa upande mwingine wa mlima, wakiharakisha kumkimbia Sauli. Wakati Sauli na majeshi yake walipokaribia kumkamata Daudi na watu wake, 2723:27 Kum 32:36; 1Sam 14:6; 2Sam 22:1-51; 2Fal 19:9; Za 18:1-50; Isa 37:6-9; 59:1; Yer 15:20, 21mjumbe alikuja kwa Sauli, akisema, “Njoo haraka! Wafilisti wanaishambulia nchi.” 28Ndipo Sauli akarudi akaacha kumfuata Daudi na kwenda kukabiliana na Wafilisti. Ndiyo sababu wanaiita sehemu hii Sela-Hamalekothi.23:28 Sela-Hamalekothi maana yake Mwamba wa Kutengana. 2923:29 1Sam 24:22; Yos 15:62; 2Nya 20:2; Wim 1:14Naye Daudi akakwea kutoka huko na kuishi katika ngome za En-Gedi.