1 Samweli 19 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 19:1-24

Sauli Ajaribu Kumuua Daudi

119:1 1Sam 18:1-9; Mit 27:4Sauli akamwambia mwanawe Yonathani na watumishi wake wote wamuue Daudi. Lakini Yonathani mwana wa Sauli alimpenda sana Daudi. 219:2 Mdo 23:16Yonathani akamwonya Daudi, akisema, “Baba yangu Sauli anatafuta nafasi ya kukuua. Ujilinde kesho asubuhi, nenda mahali pa siri na ukae huko. 319:3 1Sam 20:12Nitatoka na kukaa na baba yangu shambani mahali uliko. Nitazungumza naye juu yako, nami nitakueleza nitakachogundua.”

419:4 1Sam 20:32; 22:14; Mit 31:8-9; Yer 18:20; 1Sam 25:21; Mit 17:13; Mwa 42:22; 1Nya 6:22; Za 35:12; 109:5; Yer 18:20; 1Kor 8:12; 1Yn 3:15Yonathani akanena mema juu ya Daudi kwa Sauli baba yake na kumwambia, “Mfalme asitende mabaya kwa mtumishi wake Daudi; hajakukosea, aliyoyafanya yamekuwa ya faida sana kwako. 519:5 Amu 9:17; 1Sam 11:13; Mwa 31:36; Kum 19:10-13; 1Sam 17:49-50; 1Nya 11:14; Mt 27:4; Za 119:109; Mt 27:14Alihatarisha maisha yake alipomuua yule Mfilisti. Bwana akajipatia ushindi mkubwa kwa ajili ya Israeli wote, nawe uliuona na ukafurahi. Kwa nini basi utende mabaya kwa mtu asiye na hatia kama Daudi kwa kumuua bila sababu?”

6Sauli akamsikiliza Yonathani na kuapa hivi: “Hakika kama Bwana aishivyo, Daudi hatauawa.”

719:7 1Sam 16:21; 18:10Basi Yonathani akamwita Daudi na kumweleza mazungumzo yote. Akamleta kwa Sauli, naye Daudi akawa pamoja na Sauli kama kwanza.

8Vita vilitokea tena, naye Daudi akatoka na kupigana na Wafilisti. Akawapiga kwa nguvu nyingi hata wakakimbia mbele yake.

919:9 Amu 9:23; 1Sam 10:5; 16:14Lakini roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Bwana ikaja juu ya Sauli alipokuwa ameketi katika nyumba yake akiwa na mkuki mkononi mwake. Daudi alipokuwa anampigia kinubi, 1019:10 1Sam 18:11; Ay 5:2; Za 5:6; Mit 1:16; 29:10Sauli akajaribu kumchomea Daudi ukutani kwa huo mkuki wake, lakini Daudi akauhepa huo mkuki wa Sauli ukakita ukutani. Usiku ule ule Daudi akakimbia na kuokoka.

1119:11 Za 59; Amu 16:2Sauli akatuma watu nyumbani mwa Daudi wailinde hiyo nyumba na kumuua asubuhi. Lakini Mikali, mkewe Daudi, akamwonya akisema, “Kama hukukimbia kuokoa maisha yako usiku huu, kesho yake utauawa.” 1219:12 Yos 2:15; Mdo 9:25; 2Kor 11:33Basi Mikali akamteremsha Daudi kupitia dirishani, naye akakimbia na kuokoka. 1319:13 Mwa 31:19; Amu 17:5Kisha Mikali akachukua kinyago, akakilaza kitandani, akakifunika kwa vazi na kukiwekea singa za mbuzi kichwani.

1419:14 Kum 1:19; Yos 2:4Sauli alipotuma watu kumkamata Daudi, Mikali akasema, “Yeye ni mgonjwa.”

15Kisha Sauli akatuma watu tena kumwona Daudi naye akawaambia, “Mleteni kwangu juu ya kitanda chake ili nipate kumuua.” 16Lakini wale watu walipoingia, kumbe ni kinyago tu kilichokuwa kitandani na kwenye kichwa kulikuwepo na singa za mbuzi.

1719:17 2Sam 2:22Sauli akamwambia Mikali, “Kwa nini umenidanganya mimi hivi na kumwacha adui yangu aende zake ili apate kuokoka?”

Mikali akamwambia, “Yeye aliniambia, ‘Niache niende zangu. Kwa nini nikuue?’ ”

1819:18 1Sam 7:17; Mit 17:17; Mal 2:7Daudi alipokuwa amekimbia na kuokoka, alimwendea Samweli huko Rama na kumwambia yale yote Sauli alimfanyia. Ndipo Daudi na Samweli wakaenda Nayothi kukaa huko. 19Habari zikamfikia Sauli kusema: “Daudi yuko Nayothi huko Rama.” 2019:20 Hes 11:25-29; 1Sam 10:5; Yoe 2:28; Yn 7:32, 45; 1Kor 14:3, 24, 25Basi Sauli akatuma watu kumkamata Daudi, lakini walipoona kundi la manabii wakitoa unabii, wakiwa pamoja na Samweli akiwa amesimama hapo kama kiongozi wao, Roho wa Mungu akaja juu ya watu wa Sauli, nao pia wakatoa unabii. 21Sauli akaelezwa juu ya hilo, naye akapeleka watu wengine zaidi, nao wakatoa unabii pia. Sauli akatuma watu mara ya tatu, nao pia wakatoa unabii. 22Mwishowe, yeye mwenyewe akaondoka kwenda Rama na kwenda hadi kwenye kile kisima kikubwa kilichoko huko Seku. Naye akauliza, “Wako wapi Samweli na Daudi?”

Wakasema, “Wako Nayothi huko Rama.”

2319:23 1Sam 10:13; Mwa 31:24; Hes 23:5; 24:2; Mit 21:1; Dan 4:35; Mt 7:22; Yn 11:51; 1Kor 13:2Hivyo Sauli akaenda Nayothi huko Rama. Lakini Roho wa Mungu akaja juu yake hata yeye, akawa anatembea huku anatoa unabii hadi akafika Nayothi. 2419:24 2Sam 6:20; Isa 20:2; 1Sam 15:35; 10:11; Mik 1:8; Mdo 9:21Akavua majoho yake na pia akatoa unabii mbele ya Samweli. Akalala hali hiyo ule mchana kutwa na usiku kucha. Hii ndiyo sababu watu husema, “Je, Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?”