1 Samweli 16 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 16:1-23

Samweli Anamtia Daudi Mafuta

116:1 1Sam 8:6; 15:35; 13:14; 10:1; Rut 4:17; 2Sam 5:2; 7:8; 1Fal 8:16; 1Nya 12:23; Za 78:70; Mdo 13:22; 1Sam 9; 16Bwana akamwambia Samweli, “Utamlilia Sauli mpaka lini, maadamu nimemkataa asiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli? Jaza pembe yako mafuta, ushike njia uende; ninakutuma kwa Yese huko Bethlehemu. Nimemchagua mmoja wa wanawe kuwa mfalme.”

216:2 1Sam 20:29Lakini Samweli akasema, “Nitakwendaje? Sauli atasikia juu ya jambo hili na ataniua.”

Bwana akamwambia, “Chukua mtamba wa ngʼombe na useme, ‘Nimekuja kumtolea Bwana dhabihu.’ 316:3 Kut 4:15; Kum 17:15; 1Sam 9:16Mwalike Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakalofanya. Utamtia mafuta kwa ajili yangu yule nitakayekuonyesha.”

416:4 Mwa 48:7; Lk 2:4; 1Sam 21:1; 1Fal 2; 13; 2Fal 9:17; 2Sam 6:9; 1Fal 17:18; Hos 6:5; 11:10; Lk 18:11Samweli akafanya kile Bwana alichosema. Alipofika Bethlehemu, wazee wa mji wakatetemeka walipomlaki. Wakauliza, “Je, umekuja kwa amani?”

516:5 Kut 19:10, 22Samweli akajibu, “Ndiyo, kwa amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu. Jiwekeni wakfu na mje kwenye dhabihu pamoja nami.” Ndipo akamweka Yese wakfu pamoja na wanawe na kuwaalika kwenye dhabihu.

616:6 1Sam 17:13; 1Nya 2:13; 1Fal 12:26Walipofika, Samweli akamwona Eliabu, naye akafikiri, “Hakika mpakwa mafuta wa Bwana anasimama hapa mbele za Bwana.”

716:7 Za 147:10; 1Sam 2:3; 2Sam 7:20; Za 44:21; 139:23; Ufu 2:23; Isa 55:8; 55:8; 2Kor 10:7; 1Fal 8:39; 1Nya 29:8; Yer 11:20; 17:10Lakini Bwana akamwambia Samweli, “Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. Bwana hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini Bwana hutazama moyoni.”

816:8 1Sam 17:13Kisha Yese akamwita Abinadabu na kumpitisha mbele ya Samweli. Lakini Samweli akasema, “Hata huyu Bwana hakumchagua.” 916:9 1Sam 17:13; 2Sam 13:3; 21:21Kisha Yese akampitisha Shama, lakini Samweli akasema, “Wala huyu Bwana hakumchagua.” 10Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, “Bwana hajawachagua hawa.” 1116:11 1Sam 17:12; Mwa 37:2; 2Sam 7:8; Za 78:70Hivyo akamuuliza Yese, “Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?”

Yese akajibu, “Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo.”

Samweli akasema, “Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike.”

1216:12 1Sam 9:17; Mwa 39:6; 1Sam 17:42; Wim 5:10Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.

Ndipo Bwana akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.”

1316:13 1Sam 2:35; 2Sam 22:51; 1Sam 18; 12; 11:6; Hes 27:18; Amu 11:29; 1Sam 6:9-10Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Bwana akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama.

Daudi Katika Utumishi Kwa Sauli

1416:14 Amu 16:20; 9:23; 1Sam 18; 10; 2Sam 7:15; 1Sam 19:9; Isa 19:14; Za 51:11Basi Roho wa Bwana alikuwa ameondoka kwa Sauli, nayo roho mbaya ikaachiwa nafasi na Bwana ili imtese.

15Watumishi wa Sauli wakamwambia, “Angalia, roho mbaya imeachiwa nafasi na Bwana nayo inakutesa. 1616:16 1Sam 10:5-6; 2Nya 29:26-27; 2Fal 3:15; Za 49:4Basi bwana wetu na aamuru watumishi wake walioko hapa kutafuta mtu ambaye anaweza kupiga kinubi. Atakipiga kinubi wakati roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ikujiapo, nawe utajisikia vizuri.”

17Basi Sauli akawaambia watumishi wake, “Mtafuteni mtu apigaye kinubi vizuri mkamlete kwangu.”

1816:18 Rut 4:17; 2Sam 17:8; Mwa 39:2; 1Sam 17:37; 20:13; 1Nya 22:11; Mt 1:23Mmoja wa watumishi wake akajibu, “Nimemwona mwana wa Yese Mbethlehemu ambaye anajua kupiga kinubi. Yeye ni mtu hodari na shujaa wa vita. Ni mwenye busara katika kunena, mtu mzuri wa umbo. Bwana yu pamoja naye.”

1916:19 1Sam 17:15Ndipo Sauli akatuma wajumbe kwa Yese na kumwambia, “Nitumie mwanao Daudi, ambaye anachunga kondoo.” 2016:20 Mwa 32:13; 1Sam 10:4; Mit 18:16Kwa hiyo Yese akamchukua punda aliyepakizwa mikate, kiriba cha divai na mwana-mbuzi, na kuvipeleka vitu hivyo kwa Sauli pamoja na Daudi mwanawe.

2116:21 Mwa 41:46; Mit 22:29; 1Fal 10:8; Mit 22:29Daudi akafika kwa Sauli na kuingia kwenye kazi yake. Sauli akampenda sana, naye Daudi akawa mmoja wa wabeba silaha wake. 22Basi Sauli akatuma ujumbe kwa Yese, akisema, “Mruhusu Daudi abaki katika utumishi wangu, kwa kuwa ninapendezwa naye.”

2316:23 Amu 9:23Kila mara roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ilipomjia Sauli, Daudi alichukua kinubi chake na kupiga. Ndipo Sauli angetulizwa na kujisikia vizuri, nayo ile roho mbaya ingemwacha.