1 Samweli 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 15:1-35

Bwana Anamkataa Sauli Asiwe Mfalme

115:1 1Sam 9:16Samweli akamwambia Sauli, “Mimi ndiye ambaye Bwana alinituma nikutie mafuta uwe mfalme juu ya watu wake Israeli, basi sasa sikiliza ujumbe kutoka kwa Bwana. 215:2 Mwa 14:7; 1Sam 14:48; 2Sam 1; 8; Kut 17:8-14; Kum 25:17Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa kile walichowatendea Israeli walipowavizia wakati walipanda kutoka Misri. 315:3 Mwa 14:23; Yos 6:17; 1Sam 22:17; 22:19; 27:9; 28:8; Es 3:13; 9:5; Law 27:28; Kut 20:5; Isa 14:21; Mwa 3:17; Yos 7:24Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie; waue wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ngʼombe na kondoo, ngamia na punda.’ ”

415:4 Yos 15:24Ndipo Sauli akawaita watu na kuwapanga huko Telaimu, askari wa miguu 200,000 pamoja na watu 10,000 kutoka Yuda. 5Sauli akaenda katika mji wa Amaleki na kuwavizia bondeni. 615:6 Mwa 15:19; Hes 24:22; Amu 1:16; 1Sam 30:29; Mwa 18:25; 19:12; Mdo 2:40; Ufu 18:4; Kut 18:10; Hes 10:29Kisha akawaambia Wakeni, “Ondokeni, waacheni Waamaleki ili nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao, kwa kuwa ninyi mliwatendea mema Waisraeli wote wakati walipanda kutoka Misri.” Basi Wakeni wakaondoka, wakawaacha Waamaleki.

715:7 1Sam 14:48; Mwa 16:7; 25:17-18; Kut 15:22Ndipo Sauli akawashambulia Waamaleki toka Havila mpaka Shuri, hadi mashariki ya Misri. 815:8 Kut 17:8-16; Hes 24:7; Yos 8:23; 1Fal 20:34; Es 3:1; 1Sam 30:1Akamchukua Agagi, mfalme wa Waamaleki akiwa hai, nao watu wake wote akawaangamiza kabisa kwa upanga. 915:9 Mit 15:27; 1Tim 6:10Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi na kondoo na ngʼombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.

10Kisha neno la Bwana likamjia Samweli kusema: 1115:11 Mwa 6:6; Kut 32:14; Yos 22:16; Ay 21:14; 34:27; Za 28:5; Isa 5:12; 53:6; Yer 48:10; Eze 18:24; 1Sam 8:6; Yos 22:16; 1Fal 9:6; Za 36:3; Sef 1:6; Mt 24:13“Ninasikitika kwamba nimemfanya Sauli kuwa mfalme, kwa sababu ameacha kunifuata mimi na hakutimiza maagizo yangu.” Samweli akafadhaika, naye akamlilia Bwana usiku ule wote.

1215:12 Yos 15:55; Hes 32:42Asubuhi na mapema Samweli akaamka kwenda kukutana na Sauli, lakini akaambiwa, “Sauli amekwenda Karmeli. Huko amesimamisha mnara kwa heshima yake mwenyewe naye ameendelea na kuteremkia Gilgali.”

1315:13 Mwa 14:19; Amu 17:2; Rut 3:2; Lk 8:11Samweli alipomfikia, Sauli akamwambia, “Bwana akubariki! Nimetimiza yale Bwana aliniagiza.”

14Lakini Samweli akasema, “Nini basi huu mlio wa kondoo masikioni mwangu? Huu mlio wa ngʼombe ninaousikia ni kitu gani?”

1515:15 Mwa 3:12; Mit 28:13Sauli akajibu, “Askari wamewaleta kutoka kwa Waamaleki, waliwaacha wale kondoo na ngʼombe wazuri ili kuwatoa dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, lakini tuliwaangamiza kabisa wengine wote.”

16Samweli akamwambia Sauli, “Ngoja! Nami nitakuambia lile Bwana aliloniambia usiku huu.”

Sauli akajibu, “Niambie.”

1715:17 Kut 3:11; 1Sam 9:21Samweli akamwambia, “Ingawa zamani ulijiona mdogo machoni pako mwenyewe, Je, hukuwa kiongozi wa kabila za Israeli? Bwana alikutia mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli. 18Naye akakutuma kwa kazi maalum, akisema, ‘Nenda ukaangamize kabisa wale watu waovu, wale Waamaleki, upigane nao vita mpaka utakapowaangamiza kabisa.’ 1915:19 Mwa 14:23; 1Sam 14:32Kwa nini hukumtii Bwana? Kwa nini ulivamia nyara na kufanya uovu machoni pa Bwana?”

2015:20 1Sam 28:18Sauli akasema, “Lakini nilimtii Bwana. Nilikamilisha ile kazi ambayo Bwana alinituma. Niliwaangamiza Waamaleki kabisa na kumleta Agagi mfalme wao. 21Askari walichukua kondoo na ngʼombe kutoka kwenye nyara, zile ambazo ni nzuri sana zimewekwa wakfu kwa Mungu, ili zitolewe dhabihu kwa Bwana Mungu wako huko Gilgali.”

2215:22 Za 40:6-8; 51:16; Mit 21:3; Isa 1:11-15; Yer 7:22; Hos 6:6; Amo 5:25; Mik 6:6-8; Mk 12:33; Mt 12:7; Ebr 10:6; Kut 19:5; Mhu 5:1; Yer 7:23; Hos 6:6; Mt 5:24; 9:13Lakini Samweli akajibu:

“Je, Bwana anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu

kama vile kuitii sauti ya Bwana?

Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu,

nako kusikia ni bora

kuliko mafuta ya kondoo dume.

2315:23 Kum 18:10; 1Sam 13:13Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi,

nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu.

Kwa sababu umelikataa neno la Bwana,

naye amekukataa wewe

kuendelea kuwa mfalme.”

2415:24 Kut 9:27; Hes 22:24; Za 51:4; 1Sam 13:13; Mit 29:25; Isa 51:12-13; Yer 42:11; 2Sam 12:13; Mt 27:4; Ay 31:34; Mit 29:25; Ufu 21:8Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Nimetenda dhambi. Nimevunja amri ya Bwana na maagizo yako. Niliwaogopa watu na kwa hiyo nikafanya walivyotaka. 2515:25 Kut 10:17Sasa ninakusihi usamehe dhambi yangu, nawe urudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu Bwana.”

2615:26 Hes 15:31; 1Sam 13:14; 1Fal 14:10Lakini Samweli akamwambia, “Sitarudi pamoja nawe. Umelikataa neno la Bwana, naye Bwana amekukataa wewe, usiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli!”

2715:27 1Sam 28:14; 1Fal 11:11; 14:8; 2Fal 17:21Samweli alipogeuka ili aondoke, Sauli akangʼangʼania pindo la joho lake, nalo likararuka. 2815:28 1Sam 28:17; 13:14; 2Sam 6:21; 7:15; 1Fal 11:31Samweli akamwambia, “Bwana ameurarua ufalme wa Israeli kutoka kwako leo, naye ameutia kwa mmoja wa majirani zako, aliye bora kuliko wewe. 2915:29 Tit 1:2; Hes 23:19; Ebr 7:21; 1Nya 29:11; Eze 24:14Yeye aliye Utukufu wa Israeli hasemi uongo wala hana kigeugeu; kwa kuwa yeye si mwanadamu, hata abadili nia yake.”

3015:30 Hes 22:34; Isa 29:13; Yn 12:43; 12:41-43; Rum 2:28-29Sauli akajibu, “Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali niheshimu mbele ya wazee wa watu wangu na mbele ya Israeli; rudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu Bwana Mungu wako.” 31Hivyo Samweli akarudi pamoja na Sauli, naye Sauli akamwabudu Bwana.

32Ndipo Samweli akasema, “Niletee Agagi mfalme wa Waamaleki.”

Agagi akaja kwake kwa ujasiri, akifikiri, “Hakika uchungu wa mauti umepita.”

3315:33 Es 9:7-10; Yer 18:21; Mwa 9:6; Kut 17:11; Amu 1:7; Yak 2:13; 1Fal 18:40Lakini Samweli akasema,

“Kama upanga wako ulivyofanya wanawake

kufiwa na watoto wao,

ndivyo mama yako atakavyokuwa

hana mtoto miongoni mwa wanawake.”

Naye Samweli akamuua Agagi mbele za Bwana huko Gilgali.

3415:34 1Sam 7:17; Amu 19:14; 1Sam 10:5; 11:4Kisha Samweli akaenda Rama, lakini Sauli akapanda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli. 3515:35 1Sam 19:24; 16:1; Mwa 6:6Hadi siku Samweli alipofariki hakwenda kumwona Sauli tena, ingawa Samweli alimwombolezea. Naye Bwana alihuzunika kwamba alimfanya Sauli kuwa mfalme juu ya Israeli.