1 Samweli 14 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 14:1-52

1Siku moja Yonathani mwana wa Sauli akamwambia kijana mbeba silaha wake, akasema, “Njoo, tuwavukie Wafilisti kwenye doria upande ule mwingine.” Lakini hakumwambia baba yake.

214:2 Amu 4:5; 1Sam 13:15; Kut 28:33; Isa 10:28Sauli alikuwa akikaa kwenye viunga vya Gibea chini ya mkomamanga huko Migroni. Alikuwa pamoja na watu kama 600, 314:3 Mwa 35:18; 1Sam 22:11; 1:3; Za 78:60; 1Sam 4:21; 2:28; 4:21; Kut 28:30; 1Sam 2:28; 22:18miongoni mwao alikuwepo Ahiya, ambaye alikuwa amevaa kisibau. Alikuwa mwana wa Ikabodi, nduguye Ahitubu mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa Bwana huko Shilo. Hakuna yeyote aliyekuwa na habari kwamba Yonathani alikuwa ameondoka.

414:4 1Sam 13:23Kila upande wa njia ambayo Yonathani alikusudia kupita ili kuvuka kufikia doria ya Wafilisti kulikuwepo na jabali; moja lilikuwa linaitwa Bosesi, na jingine Sene. 514:5 Yos 18:24Jabali moja lilisimama kaskazini kuelekea Mikmashi na jingine upande wa kusini kuelekea Geba.

614:6 Amu 14:3; 1Sam 17:26; 31:4; Yer 9:26; Eze 28:10; 1Sam 13:22; 1Fal 19:12; Mt 19:26; Ebr 11:34; Amu 7:4; Za 33:16; 1Sam 17:46-47Yonathani akamwambia kijana wake mbeba silaha, “Njoo, tuvukie doria ya wale jamaa wasiotahiriwa. Huenda Bwana atatenda kwa ajili yetu. Hakuna chochote kitakachoweza kumzuia Bwana kuokoa, kwamba ni kwa wingi au kwa uchache.”

7Mbeba silaha wake akamwambia, “Fanya yale yote uliyo nayo katika moyo wako. Songa mbele; moyo wangu na roho yangu viko pamoja nawe.”

8Yonathani akasema, “Basi njoo; tutavuka kuwaelekea hao watu na kuacha watuone. 9Kama wakituambia, ‘Subirini hapo mpaka tuje kwenu,’ tutakaa pale tulipo na hatutakwea kwao. 1014:10 Mwa 24:1, 14; Yos 2:24; Amu 6:36-37; 1Sam 10:7; 2Sam 5:24; Isa 7:11-14Lakini kama watasema, ‘Pandeni mje kwetu,’ tutakwea, kwa sababu hiyo itakuwa ishara yetu kwamba Bwana amewatia mikononi mwetu.”

1114:11 Mwa 14:13; 1Sam 13:6Basi wote wawili wakajionyesha kwa doria ya Wafilisti. Wafilisti wakasema, “Tazama! Waebrania wanatambaa toka mashimoni walimokuwa wamejificha.” 1214:12 Amu 8:16; 1Sam 17:46; 2Sam 5:24; 1Sam 17:43-44Watu wa kwenye doria wakawapigia kelele Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, “Njooni, pandeni kwetu nasi tutawakomesha.”

Basi Yonathani akamwambia mbeba silaha wake, “Panda nyuma yangu; Bwana amewatia mikononi mwa Israeli.”

13Yonathani akapanda juu, akitumia mikono yake na miguu, pamoja na mbeba silaha wake papo hapo nyuma yake. Wafilisti wakaanguka mbele ya Yonathani, naye mbeba silaha wake akamfuata akiwaua nyuma yake. 14Katika hilo shambulio la kwanza, Yonathani na mbeba silaha wake waliua kama watu ishirini kwenye eneo kama la nusu eka.

Israeli Wawafukuza Wafilisti

1514:15 Mwa 35:5; Kut 14:24; 19:16; 2Fal 7:5-7; 1Sam 13:17; Amu 7:21; Ay 18:11; Za 48:5-6Kisha fadhaa ikawapata jeshi lote, wale waliokuwa kambini na shambani, wale waliokuwa katika doria na makundi ya washambuliaji, nayo nchi ilitetemeka. Ilikuwa ni hofu ya ghafula iliyotumwa na Mungu.

1614:16 2Sam 18:24; 2Fal 9:17; Isa 52:8; Eze 33:2Wapelelezi wa Sauli huko Gibea ya Benyamini wakaona jeshi likitokomea pande zote. 17Ndipo Sauli akawaambia watu wale waliokuwa pamoja naye, “Kagueni jeshi mkaone ni nani ameondoka katikati yetu.” Walipokagua, akawa ni Yonathani na mbeba silaha wake ambao hawakuwepo.

1814:18 1Sam 30:7; Amu 18:5Sauli akamwambia Ahiya, “Leta Sanduku la Mungu.” (Wakati huo lilikuwa kwa Waisraeli.) 1914:19 Hes 27:21; Yos 9:14; Za 106:13Wakati Sauli alipokuwa akisema na kuhani, makelele katika kambi ya Wafilisti yakaongezeka zaidi na zaidi. Hivyo Sauli akamwambia kuhani, “Rudisha mkono wako.”

2014:20 Amu 7:22; Eze 38:21; Zek 14:13; 2Nya 20:23Kisha Sauli na watu wake wote wakakusanyika na kwenda vitani. Wakawakuta Wafilisti wakiwa wamechanganyikiwa kabisa, wakitiana panga kila mmoja na wenzake. 2114:21 1Sam 29:4Wale Waebrania ambao walishakuwa pamoja na Wafilisti, na waliokuwa wamepanda pamoja nao katika kambi zao, wakaenda upande wa Waisraeli waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani. 2214:22 1Sam 13:6; Isa 9:19-21Waisraeli wote waliokuwa wamejificha katika nchi ya milima ya Efraimu waliposikia kuwa Wafilisti wamekimbia, wakajiunga vitani na kuwafuata kwa bidii. 2314:23 Kut 14:30; Yos 7; 2; 1Sam 13:5; Za 44:6-7; Isa 63:9; Za 17:7Hivyo Bwana akawaokoa Waisraeli siku ile, navyo vita vilienea hadi kupita Beth-Aveni.

Yonathani Ala Asali

2414:24 Yos 6:26; Law 27:29; Hes 21:2; Kum 27:15-26; Amu 11:30; 21:1-5; Mit 11:9Basi watu wa Israeli walikuwa katika dhiki siku ile, kwa sababu Sauli alikuwa amewafunga watu kwa kiapo, akisema, “Alaaniwe mtu yeyote ambaye atakula chakula kabla ya jioni, kabla sijalipiza kisasi juu ya adui zangu!” Kwa hiyo hakuna mtu yeyote katika jeshi aliyeonja chakula.

2514:25 Kum 9:28; Mt 3:5; Kut 3:8; Hes 13:27Jeshi lote liliingia mwituni, na huko kulikuwepo na asali ardhini. 26Walipoingia mwituni, wakaona asali ikitiririka, hata hivyo hakuna mtu yeyote aliyetia mkono wake kinywani, kwa sababu waliogopa kiapo. 2714:27 Za 19:10; Mit 16:24; 24:13Lakini Yonathani alikuwa hajasikia kuwa baba yake alikuwa amewafunga watu kwa kiapo, hivyo akainyoosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake na kuichovya katika sega la asali. Akainua mkono wake na kuutia kinywani mwake, nayo macho yake yakawa maangavu. 28Kisha mmoja wa askari wake akamwambia, “Baba yako alilifunga jeshi kwa kiapo kikali, akisema, ‘Alaaniwe mtu yeyote alaye chakula leo!’ Ndiyo sababu watu wanalegea.”

2914:29 Yos 7:25; 1Fal 18:18Yonathani akasema, “Baba yangu ameitaabisha nchi. Ona jinsi nilivyopata nguvu mpya nilipoonja asali hii kidogo. 30Ingekuwa bora zaidi mara ngapi kama watu wangalikula leo baadhi ya nyara walizoteka kutoka kwa adui zao. Je, mauaji ya Wafilisti yasingekuwa makubwa zaidi?”

3114:31 Yos 10:12Siku ile baada ya Waisraeli kuwaua Wafilisti kutoka Mikmashi mpaka Aiyaloni, walikuwa wamechoka. 3214:32 1Sam 15:19; Es 9:10; Mwa 9:4; Law 3:17; Kum 12:16Watu wakarukia zile nyara, wakichukua kondoo, ngʼombe na ndama, wakawachinja hapo juu ya nchi na kuwala, pamoja na damu. 3314:33 Mwa 9:4Kisha mtu mmoja akamwambia Sauli, “Tazama, watu wanatenda dhambi dhidi ya Bwana kwa kula nyama yenye damu.”

Akasema, “Mmevunja uaminifu. Livingirisheni jiwe kubwa hapa mara moja.” 3414:34 Law 19:26Kisha Sauli akasema, “Nendeni miongoni mwa watu, mwaambie, ‘Kila mmoja wenu aniletee ngʼombe wake na kondoo, mwachinjie hapa na mle. Msitende dhambi dhidi ya Bwana kwa kula nyama ikiwa na damu ndani yake.’ ”

Hivyo kila mmoja akaleta ngʼombe wake jioni ile na kumchinja hapo. 3514:35 1Sam 7:17; Amu 21:4; 2Sam 24:25Ndipo Sauli akamjengea Bwana madhabahu, na ndiyo ilivyokuwa mara yake ya kwanza kujenga madhabahu.

3614:36 Mwa 25:22; Amu 18:5; Mal 2:7; Yak 4:8Sauli akasema, “Tuteremke tufuatie Wafilisti usiku na kuwateka nyara mpaka mapambazuko, nasi tusiache hata mmoja wao hai.”

Wakajibu, “Fanya lolote lile uonalo jema zaidi kwako.”

Lakini kuhani akasema, “Tuulize kwa Mungu mahali hapa.”

3714:37 1Sam 28:6, 15; 2Sam 22:42; Za 18:41Basi Sauli akamuuliza Mungu, akisema, “Je, niteremke kuwafuatia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwa Israeli?” Lakini Mungu hakumjibu siku ile.

3814:38 Yos 7:11; 1Sam 10:19Kwa hiyo Sauli akasema, “Njooni hapa, ninyi nyote ambao ni viongozi wa jeshi, na tutafute ni dhambi gani imefanywa leo. 3914:39 Hes 14:21; 2Sam 12:5; Ay 19:25; Za 18:46; 42:2; Yos 7:15Kwa hakika kama Bwana aiokoaye Israeli aishivyo, hata kama itakuwa juu ya mwana wangu Yonathani, ni lazima afe.” Lakini hakuna mtu yeyote aliyesema neno.

40Kisha Sauli akawaambia Waisraeli wote, “Ninyi simameni huko; mimi na mwanangu Yonathani tutasimama hapa.”

Watu wakajibu, “Fanya lile unaloona jema zaidi kwako.”

4114:41 Mdo 1:24; Mit 16:33; Yos 7:16; 1Sam 10:20-21Kisha Sauli akamwomba Bwana, Mungu wa Israeli, akisema, “Nipe jibu lililo sawa.” Yonathani na Sauli wakatolewa kwa kura, nao watu wakawa salama. 4214:42 Yon 1:7Sauli akasema, “Pigeni kura kati yangu na mwanangu Yonathani.” Kura ikamwangukia Yonathani.

4314:43 Yos 7:19Basi Sauli akamwambia Yonathani, “Niambie ni nini ulichokifanya.”

Hivyo Yonathani akamwambia, “Nilionja tu asali kidogo kwa ncha ya fimbo yangu. Je, sasa ni lazima nife?”

4414:44 Rut 1:17Sauli akasema, “Mungu na anishughulikie kwa ukali zaidi kama wewe Yonathani hutakufa.”

4514:45 1Fal 1:52; Mt 10:30; 2Sam 14:11; Lk 21:18; Isa 13:3; 2Kor 6:1Lakini watu wakamwambia Sauli, “Je, Yonathani atakufa, yeye ambaye ameleta wokovu huu mkubwa Israeli? Hasha! Hakika kama Bwana aishivyo, hakuna hata unywele wa kichwa chake utakaoanguka juu ya ardhi, kwa kuwa alifanya jambo hili leo kwa msaada wa Mungu.” Basi watu wakamwokoa Yonathani, wala hakuuawa.

46Kisha Sauli akaacha kuwafuata Wafilisti, nao wakajiondoa na kurudi katika nchi yao.

4714:47 Mwa 19:37-38; 2Sam 12:31; 8:3; 10:6; 23:36Baada ya Sauli kujitwalia utawala katika Israeli, alipigana dhidi ya adui zake kila upande: Moabu, Waamoni, Edomu, wafalme wa Soba, na Wafilisti. Popote alipogeukia, aliwashinda. 4814:48 Mwa 36:12; Hes 13:29; Amu 3:13; 1Sam 15:2, 7; 27:8; 28:18; 30:13; 2Sam 1:13; 1Nya 4:43Akapigana kishujaa na kuwashinda Waamaleki, akiikomboa Israeli kutoka mikono ya wale waliokuwa wamewateka nyara.

Jamaa Ya Sauli

4914:49 1Sam 31:2; 1Nya 8:33; Mwa 29:26; 1Sam 18:17-20Wana wa Sauli walikuwa Yonathani, Ishvi na Malki-Shua. Jina la binti yake mkubwa lilikuwa Merabu, naye mdogo aliitwa Mikali. 5014:50 2Sam 2:8; 3:6; 1Fal 2:5; 1Sam 10:14Jina la mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu binti wa Ahimaasi. Jina la jemadari wa jeshi la Sauli aliitwa Abneri mwana wa Neri, naye Neri alikuwa babaye mdogo Sauli. 5114:51 1Sam 9:1Babaye Sauli yaani, Kishi na Neri baba yake Abneri walikuwa wana wa Abieli.

5214:52 1Sam 8:11Siku zote za utawala wa Sauli zilikuwa za vita vikali dhidi ya Wafilisti, na wakati wowote Sauli alimwona mtu mwenye nguvu au shujaa, alimchukua kwa utumishi wake.