1 Samweli 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 11:1-15

Sauli Aukomboa Mji Wa Yabeshi

111:1 Mwa 19:38; 1Sam 12:12; 31:11; 2Sam 10:2; 17:27; 2:4-5; 21:12; Kut 23:32; Yer 37:1; Eze 17:13; 1Nya 19:1; Amu 21:8Nahashi yule Mwamoni, akakwea kuuzunguka kwa jeshi mji wa Yabeshi-Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia, “Fanya mkataba na sisi, na tutakuwa chini yako.”

211:2 Mwa 34:15; Hes 16:14; 1Sam 17:26; 2Sam 17:26Lakini Nahashi yule Mwamoni akajibu, “Nitafanya mkataba na ninyi tu kwa sharti kwamba nitangʼoa jicho la kulia la kila mmoja wenu, na hivyo kuleta aibu juu ya Israeli yote.”

311:3 1Sam 8:4; Amu 2:16Viongozi wa Yabeshi wakamwambia, “Tupe siku saba ili tuweze kutuma wajumbe katika Israeli yote, kama hakuna hata mmoja anayekuja kutuokoa, tutajisalimisha kwako.”

411:4 1Sam 10:5; 15:34; Mwa 27:38; Hes 25:6; Amu 2:4; 21:2; 2Sam 21:6; Rum 12:15Wajumbe walipofika Gibea ya Sauli na kutoa taarifa juu ya masharti haya kwa watu, wote walilia kwa sauti kubwa. 5Wakati huo huo Sauli alikuwa anarudi kutoka mashambani, akiwa nyuma ya maksai wake, naye akauliza, “Watu wana nini? Mbona wanalia?” Ndipo wakamweleza jinsi watu wa Yabeshi walivyokuwa wamesema.

611:6 Amu 3:10; 6:34; 13:25; 1Sam 10:10; 16:13Sauli aliposikia maneno yao, Roho wa Mungu akaja juu yake kwa nguvu, naye akawaka hasira. 711:7 1Sam 6:14; Amu 19:29; 21:5; 20:1; Mwa 35:5; 1Nya 14:14; 17:10; Mit 14:26Akachukua jozi ya maksai na kuwakata vipande vipande, naye kuvituma hivyo vipande kupitia wajumbe katika Israeli yote, wakitangaza, “Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa maksai wa kila mmoja ambaye hatamfuata Sauli na Samweli.” Kisha hofu ya Bwana ikawaangukia watu, nao wakatoka kama mtu mmoja. 811:8 Amu 20:2; 1:4; 2Sam 24:9Sauli alipowakusanya huko Bezeki, watu wa Israeli walikuwa 300,000 na watu wa Yuda 30,000.

9Wakawaambia wale wajumbe waliokuwa wamekuja, “Waambieni watu wa Yabeshi-Gileadi, ‘Kesho kabla jua halijawa kali, mtaokolewa.’ ” Wajumbe walipokwenda na kutoa taarifa hii kwa watu wa Yabeshi, wakafurahi. 10Wakawaambia Waamoni, “Kesho tutajisalimisha kwenu, nanyi mtaweza kututendea chochote mnachoona chema kwenu.”

1111:11 Amu 7:16; Mwa 19:38Kesho yake Sauli alitenganisha watu wake katika vikosi vitatu; wakati wa zamu ya mwisho ya usiku wakaingia katika kambi ya Waamoni na kuwachinja mpaka mchana. Wale walionusurika wakasambaa, kiasi kwamba hawakusalia watu wawili pamoja.

Sauli Athibitishwa Kuwa Mfalme

1211:12 Kum 13:13; Lk 19:27Kisha watu wakamwambia Samweli, “Ni nani yule aliyeuliza, ‘Je, Sauli atatawala juu yetu?’ Tuletee hawa watu, nasi tutawaua.”

1311:13 2Sam 19:22; 1Sam 19:5; 1Nya 11:14; Kut 14:13; Za 44:4-8; Ebr 2:3Lakini Sauli akasema, “Hakuna hata mmoja atakayeuawa leo, kwa kuwa siku hii Bwana ameokoa Israeli.”

1411:14 Yos 10:43; 1Sam 10:8; 10:25Ndipo Samweli akawaambia watu, “Njooni, twendeni Gilgali na huko tuthibitishe ufalme.” 1511:15 Yos 5:9; 2Sam 19:15; 1Sam 12:1Kwa hiyo watu wote wakaenda Gilgali na kumthibitisha Sauli kuwa mfalme mbele za Bwana. Huko wakatoa dhabihu za sadaka za amani mbele za Bwana, naye Sauli na Waisraeli wote wakafanya karamu kubwa.