1 Samweli 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 10:1-27

110:1 1Sam 16:1; 9:16; 2Fal 9:1; Kut 29:7; 34:9; 1Sam 9:16; 1Fal 1:39; 2Sam 20:19; Za 78:62-71; Kum 32:9; Yer 10:16Ndipo Samweli akachukua chupa ndogo ya mafuta na kuyamimina juu ya kichwa cha Sauli, akambusu, akisema, “Je, Bwana hakukutia mafuta uwe kiongozi juu ya watu wake Israeli? 210:2 Mwa 35:20; 1Sam 9:4-5; Yos 18:28Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na watu wawili karibu na kaburi la Raheli, huko Selsa kwenye mpaka wa Benyamini. Watakuambia, ‘Punda wale uliotoka kwenda kuwatafuta, wamekwisha kupatikana. Sasa baba yako ameacha kufikiri kuhusu punda na sasa ana hofu kukuhusu wewe. Anauliza, “Nitafanyaje kuhusu mwanangu?” ’

310:3 Mwa 35:8; 28:22; Yos 19:22; Amu 4:6, 12; 8:18; Za 89:12“Kisha utakwenda mbele kutoka hapa mpaka uufikie mwaloni wa Tabori. Watu watatu wanaopanda kwa Mungu huko Betheli watakutana nawe hapo. Mmoja atakuwa amechukua wana-mbuzi watatu, mwingine mikate mitatu, na mwingine kiriba cha divai. 410:4 1Sam 16:20; Mit 18:20; Amu 18:15Watakusalimu na kukupa mikate miwili, ambayo utaipokea kutoka kwao.

510:5 1Sam 11:4; 15:34; 13:3; Hes 11:29; 1Fal 20:35; 2Fal 2:3; 4:1; 6:1; 9:1; 3:15; Amo 7:14; Law 26:30; Mwa 31:27; Yer 31:4; 1Fal 1:40; Isa 30:29; 1Sam 16:16; 18:10; 19:9; 19:20; Za 92:3; 1Nya 25:1; 1Kor 14:1“Baada ya hayo utakwenda Gibea ya Mungu, ambapo hapo kuna kambi ya Wafilisti. Unapokaribia mji utakutana na kundi la manabii wakiteremka kutoka mahali pa juu wakiwa na vinubi, matari, filimbi na zeze vikipigwa mbele yao, nao watakuwa wakitoa unabii. 610:6 Hes 11:25; 1Sam 19:23-24; Mt 7:22Roho wa Bwana atakuja juu yako kwa nguvu, nawe utatoa unabii pamoja nao; nawe utageuzwa kuwa mtu wa tofauti. 710:7 2Sam 7:3; 1Fal 8:17; 1Nya 22:7; 28:2; 2Nya 6:7; Mhu 9:10; Amu 9:33; Yos 1:3; Lk 1:28; Ebr 13:5Mara ishara hizi zitakapotimizwa, fanya lolote mkono wako upasao kufanya, kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.

810:8 Yos 4:20; 10:43; 1Sam 7:16; 11:14; 13:4“Tangulia kushuka mbele yangu mpaka Gilgali. Hakika nami nitateremka nikujie ili kutoa dhabihu za sadaka za kuteketezwa na dhabihu za amani, lakini lazima ungoje kwa siku saba hata nitakapokujia na kukuambia likupasalo kufanya.”

Sauli Afanywa Mfalme

910:9 Kum 13:2Ikawa Sauli alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu aliubadilisha moyo wa Sauli, na ishara hizi zote zikatimizwa siku ile. 1010:10 Hes 11:25; 1Sam 11:6; 19:20; Mt 7:21-23Walipofika Gibea, akakutana na kundi la manabii. Roho wa Mungu akaja juu yake kwa nguvu, naye akajiunga nao katika kutoa unabii kwao. 1110:11 Mt 13:54; Yn 7:15; 1Sam 19:24; 2Fal 9:11; Yer 29:26; Hos 9:7Ikawa wale wote waliomfahamu hapo mwanzo walipomwona akitoa unabii pamoja na manabii, wakaulizana, “Ni nini hiki kilichomtokea mwana wa Kishi? Je, Sauli naye pia yumo miongoni mwa manabii?”

1210:12 Isa 54:13; Yn 3:8Mtu mmoja ambaye aliishi huko akajibu, “Je, naye baba yao ni nani?” Basi ikawa mithali, kusema, “Je, Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?” 1310:13 1Sam 19:23Baada ya Sauli kumaliza kutoa unabii, alikwenda mahali pa juu.

1410:14 1Sam 14:50; 9:3Basi babaye mdogo akamuuliza Sauli na mtumishi wake, “Je, mlikuwa wapi?”

Akajibu, “Tulikuwa tukiwatafuta punda. Lakini tulipoona hawapatikani, tulikwenda kwa Samweli.”

15Babaye mdogo Sauli akasema, “Niambie Samweli amekuambia nini.”

1610:16 1Sam 9:3, 20Sauli akajibu, “Alituhakikishia kwamba punda wamepatikana.” Lakini hakumwambia babaye mdogo kila kitu Samweli alichomwambia kuhusu ufalme.

1710:17 1Sam 7:5; Amu 20:1; 1Sam 11:15Samweli akawaita watu wa Israeli kuja kwa Bwana huko Mispa, 1810:18 Kut 1:14; Hes 10:9; Amu 6:8-9; Kum 4:34; Neh 9:9-12naye akawaambia, “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Niliwatoa Israeli kutoka Misri, nami niliwaokoa toka nguvu za Misri na falme zote zilizowaonea.’ 1910:19 Hes 11:20; Kum 33:5; Za 7:10; 18:48; 68:20; 145:19; 1Sam 8:5; Kum 17:14; Yos 7:14Lakini sasa mmemkataa Mungu wenu, ambaye anawaokoa toka katika maafa yenu yote na taabu zenu zote. Nanyi mmesema, ‘Hapana, tuteulie mfalme atutawale.’ Sasa basi, jihudhurisheni wenyewe mbele za Bwana kwa kabila zenu na kwa koo zenu.”

2010:20 Yos 7:14; Mdo 1:24Samweli alipoyasogeza makabila yote ya Israeli, kabila la Benyamini likachaguliwa. 2110:21 Es 3:7; Mit 16:33Kisha akalisogeza mbele kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo, nao ukoo wa Matri ukachaguliwa. Mwishoni Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipomtafuta, hakuonekana. 2210:22 Mwa 25:22; Amu 18:5Wakazidi kuuliza kwa Bwana, “Je, huyo mtu amekwisha kufika hapa?”

Naye Bwana akasema, “Ndiyo, amejificha katikati ya mizigo.”

2310:23 1Sam 9:2Wakakimbia na kumleta kutoka huko, naye aliposimama katikati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu wengine wote. 2410:24 Kum 17:15; 2Sam 21:6; 1Sam 9:2; 1Fal 1:25, 34, 39; 2Fal 11:12Samweli akawaambia watu wote, “Je, mnamwona mtu ambaye Bwana amemchagua? Hayupo aliye kama yeye miongoni mwa watu wote.”

Ndipo watu wakapiga kelele, wakasema, “Mfalme na aishi maisha marefu.”

2510:25 1Sam 8:9; Kum 17:14-20; 1Sam 8:11-18; 2Fal 11:12; 1Sam 11:14Samweli akawaeleza watu madaraka ya ufalme. Akayaandika kwenye kitabu na kuweka mbele za Bwana. Kisha Samweli akawaruhusu watu, kila mmoja aende nyumbani kwake.

2610:26 Amu 19:14; 20:44Sauli pia akaenda nyumbani kwake huko Gibea, akisindikizwa na watu hodari ambao Mungu alikuwa amegusa mioyo yao. 2710:27 Kum 13:13; 1Sam 20:7; 1Fal 10:25; 2Nya 32:23; 17:5; Za 68:29; Mdo 7:35, 51, 52; 2Sam 8:2; 1Fal 4:21; 10:25; Za 72:10; Mt 2:11Lakini baadhi ya watu wakorofi walisema, “Huyu mtu atawezaje kutuokoa?” Wakamdharau na wala hawakumletea zawadi. Lakini Sauli akanyamaza kimya.