1 Petro 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Petro 1:1-25

Salamu

11:1 2Pet 1:1; Mt 24:22; Mdo 16:7Petro, mtume wa Yesu Kristo:

Kwa wateule wa Mungu, wageni katika ulimwengu, waliotawanyika kote katika Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia. 21:2 Rum 8:29; 2The 2:13; Ebr 10:22; 12:24Ni ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba kulingana na alivyotangulia kuwajua, kupitia kwa kazi ya utakaso wa Roho, katika utiifu kwa Yesu Kristo na kunyunyiziwa damu yake:

Neema na amani ziwe kwenu kwa wingi.

Tumaini Lenye Uzima

31:3 1Kor 1:3; Efe 1:3; Tit 3:5; Yak 1:18; 1Pet 3:21Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema zake kuu ametuzaa sisi mara ya pili katika tumaini lenye uzima kupitia kwa kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu, 41:4 1Tim 4:8; Mdo 20:32; Rum 8:17; 1Pet 5:4; Kol 1:5ili tuupate urithi usioharibika, usio na uchafu, ule usionyauka: uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu, 51:5 1Sam 2:9; Yn 10:28; Rum 11:14; 8:18ninyi ambao mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani, hadi uje ule wokovu ulio tayari kufunuliwa nyakati za mwisho. 61:6 Rum 5:2; 1Pet 5:10; 4:12Katika hili mnafurahi sana, ingawa sasa kwa kitambo kidogo mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna nyingi. 71:7 Mit 17:3; Isa 48:10; 1The 2:19Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atadhihirishwa. 81:8 Yn 20:29; 1Yn 4:10; 2Kor 5:7; Ebr 11:1, 27Ingawa hamjamwona, mnampenda; tena ingawa sasa hammwoni, mnamwamini na kujawa na furaha isiyoneneka yenye utukufu usioelezeka. 91:9 Rum 6:22Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.

101:10 Mt 22:24; 3:17Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewajia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa, 111:11 Mdo 16:7; Za 22:1; Isa 52:13; 53:12; Lk 24:26wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao alionyesha, alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata. 121:12 Efe 3:10; Lk 2:13Walidhihirishiwa kwamba walikuwa hawajihudumii wao wenyewe, bali waliwahudumia ninyi, waliponena kuhusu mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiria ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Hata malaika wanatamani kuyafahamu mambo haya.

Mwito Wa Kuishi Maisha Matakatifu

131:13 Mdo 24:25; 1Pet 1:3, 21; Ebr 3:6; 1Pet 1:7, 10; 1Kor 1:7; Efe 5:19; Kol 3:16Kwa hiyo, tayarisheni nia zenu kwa kazi; mwe na kiasi, mkitumainia kikamilifu ile neema mtakayopewa Yesu Kristo atakapodhihirishwa. 141:14 Rum 12:2; Efe 4:18Kama watoto watiifu, msifuate tamaa zenu mbaya wakati mlipoishi kwa ujinga. 151:15 Isa 35:8; 1The 4:7; 1Yn 3:3Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi kuweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. 161:16 Law 19:2; 20:7Kwa maana imeandikwa: “Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”

171:17 Mdo 10:34; Ebr 12:28Kwa sababu mnamwita Baba ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni. 181:18 Mt 20:28; 1Kor 6:20Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu, 191:19 Yn 1:29; Kut 12:5bali kwa damu ya thamani ya Kristo, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa. 201:20 Mt 25:34; Ebr 9:26Yeye alichaguliwa kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, lakini akadhihirishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili yenu. 211:21 Rum 10:9Kupitia kwake mmemwamini Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na akampa utukufu, ili imani yenu na tumaini lenu ziwe kwa Mungu.

221:22 Yak 4:8; Rum 12:10; Ebr 13:1Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni. 231:23 Yn 1:13; Ebr 4:12Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele. 241:24 Za 103:15; Isa 40:6Maana,

“Wanadamu wote ni kama majani,

nao utukufu wao ni kama maua ya kondeni;

majani hunyauka na maua huanguka,

251:25 Isa 40:6-8; Yak 1:10-11lakini neno la Bwana ladumu milele.”

Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.