1 Nyakati 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 7:1-40

Wana Wa Isakari

17:1 Mwa 30:18; Hes 26:23; Mwa 46:13Wana wa Isakari walikuwa:

Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.

27:2 2Sam 24:1-2; 1Nya 21:1-5; 27:1Wana wa Tola walikuwa:

Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.

37:3 1Nya 5:24Mwana wa Uzi alikuwa:

Izrahia.

Wana wa Izrahia walikuwa:

Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao. 4Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.

5Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000.

Wana Wa Benyamini

67:6 Mwa 46:21; Hes 26:38Wana watatu wa Benyamini walikuwa:

Bela, Bekeri na Yediaeli.

7Wana wa Bela walikuwa:

Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034.

8Wana wa Bekeri walikuwa:

Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri. 97:9 Kum 10:8Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200.

10Mwana wa Yediaeli alikuwa:

Bilhani.

Wana wa Bilhani walikuwa:

Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. 11Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.

127:12 Hes 26:38-39Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.

Wana Wa Naftali

137:13 Mwa 30:8; 46:24Wana wa Naftali walikuwa:

Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha.

Wana Wa Manase

147:14 Mwa 41:51; Yos 17:1; Hes 26:30Wana wa Manase walikuwa:

Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi. 157:15 Hes 26:33; 36:1-12; 27:1-11Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu. 16Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.

177:17 Hes 26:30; 1Sam 12:11Mwana wa Ulamu alikuwa:

Bedani.

Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase. 187:18 Yos 17:2Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla.

19Wana wa Shemida walikuwa:

Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.

Wana Wa Efraimu

207:20 Mwa 41:52; Hes 26:35; Mwa 48:14-20; Kum 33:13, 17; Za 60:7; 108:8Wana wa Efraimu walikuwa:

Shuthela, ambaye alimzaa Beredi,

Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada,

Eleada akamzaa Tahathi, 21Tahathi akamzaa Zabadi,

na Zabadi akamzaa Shuthela.

Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. 227:22 Mwa 37:34-35; Yos 7:6; 2Sam 3:31; Ay 2:11; Za 69:11; Yoe 2:13; Yn 1:19Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. 237:23 Mwa 35:18; 1Sam 4:21; 1Nya 4:9Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. 247:24 Yos 10:10; 16:3, 5; 16:3; 1Sam 13:18; 2Nya 8:5Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.

25Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu,

Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,

26Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi,

Amihudi akamzaa Elishama, 277:27 Hes 13:8, 16Elishama akamzaa Nuni,

Nuni akamzaa Yoshua.

287:28 Yos 10:33; 16:7Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake. 297:29 Yos 17:11; 11:2; 1Fal 9:15; Amu 1:22-29Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.

Wana Wa Asheri

307:30 Mwa 40:17; Hes 26:44; Mwa 49:20; Kum 33:24Wana wa Asheri walikuwa:

Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.

31Wana wa Beria walikuwa:

Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.

32Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.

33Wana wa Yafleti walikuwa:

Pasaki, Bimhali na Ashvathi.

Hawa walikuwa wana wa Yafleti.

34Wana wa Shemeri walikuwa:

Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.

35Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa:

Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.

36Wana wa Sofa walikuwa:

Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, 37Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani7:37 Kwa jina lingine Yetheri. na Beera.

38Wana wa Yetheri walikuwa:

Yefune, Pispa na Ara.

39Wana wa Ula walikuwa:

Ara, Hanieli na Risia.

407:40 Kum 2:14Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.