1 Nyakati 20 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 20:1-8

Kutekwa Kwa Raba

(2 Samweli 12:26-31)

120:1 Kum 3:11; 2Sam 12:26; Amo 1:13-15; 2Nya 36:10; Mhu 3:8; Yer 49:2; 1Sam 11:1; 1Fal 20:22; Eze 21:20Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni, na akaenda Raba na kuuzingira, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akashambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu. 220:2 2Sam 12:30-31Daudi akachukua taji kutoka kwa kichwa cha mfalme wao, lililokuwa na uzito wa talanta moja ya dhahabu,20:2 Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34. nayo ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua nyara nyingi kutoka mjini huo. 320:3 Kum 29:11Akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.

Vita Na Wafilisti

(2 Samweli 21:15-22)

420:4 Yos 10:33; Mwa 14:5Baada ya muda, kulitokea vita dhidi ya Wafilisti, huko Gezeri. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Sipai, aliyekuwa mmoja wa wazao wa Warefai,20:4 Yaani majitu. nao Wafilisti wakashindwa.

520:5 1Sam 17:7Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.

6Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu: jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai. 7Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua.

8Hawa walikuwa ndio wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake.