Wana Wa Israeli
12:1 Mwa 32:28; 35:10; Kut 32:13; Hes 1:5-15; 13:4-15; Mwa 29:32; 1Fal 18:31Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli:
Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni, 2Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.
Yuda
Hadi Wana Wa Hesroni
32:3 Mwa 29:35; 38:2; Hes 26:19Wana wa Yuda walikuwa:
Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua. 42:4 Mwa 38:11-30; 11:31; 38:29Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.
52:5 Mwa 46:12; Hes 26:21; Rut 4:18Wana wa Peresi walikuwa:
Hesroni na Hamuli.
62:6 1Fal 4:31Wana wa Zera walikuwa:
Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.
72:7 Yos 7:1; 6:18; 1Nya 4:1Mwana wa Karmi alikuwa:
Akari,2:7 Akari maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani (Yos 6:1-26; 22:20). ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu.
8Mwana wa Ethani alikuwa:
Azariya.
92:9 Hes 26:21Wana wa Hesroni walikuwa:
Yerameeli, Ramu na Kalebu.
Kuanzia Ramu Mwana Wa Hesroni
102:10 Lk 3:32-33; Kut 6:23; Hes 1:7; Rut 4:19Ramu alimzaa
Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda. 11Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi, 122:12 Rut 2:1; 4:17Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.
132:13 Rut 4:17; Isa 16:6Yese akawazaa
Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,2:13 Au: Shima, maana yake Sifa njema (pia 1Sam 16:9; 17:13). 14wa nne Nethaneli, wa tano Radai, 15wa sita Osemu, na wa saba Daudi. 162:16 1Sam 26:6; 2Sam 2:18; 2:13Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli. 172:17 2Sam 17:25Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.
Kalebu Mwana Wa Hesroni
18Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni. 192:19 1Nya 2:42, 50Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri. 202:20 Kut 32:2; 35:30; 2Nya 1:5Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.
212:21 Hes 21:1Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu. 22Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi. 232:23 Hes 32:41; 32:42; Yos 13:30; Kum 3:14(Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.
242:24 1Nya 4:5; 2Nya 11:6; 20:20; 2Sam 14:2; Neh 3:5; Yer 6:1Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.
Yerameeli Mwana Wa Hesroni
25Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa:
Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya. 26Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.
27Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa:
Maasi, Yamini na Ekeri.
28Wana wa Onamu walikuwa:
Shamai na Yada.
Wana wa Shamai walikuwa:
Nadabu na Abishuri.
29Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi.
30Wana wa Nadabu walikuwa
Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.
31Apaimu akamzaa:
Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani.
Sheshani akamzaa Alai.
32Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa:
Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.
33Wana wa Yonathani walikuwa:
Pelethi na Zaza.
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli.
34Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu.
Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha. 35Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.
362:36 1Nya 11:41Atai akamzaa Nathani,
Nathani akamzaa Zabadi,
37Zabadi akamzaa Eflali,
Eflali akamzaa Obedi,
38Obedi akamzaa Yehu,
Yehu akamzaa Azaria,
39Azaria akamzaa Helesi,
Helesi akamzaa Eleasa,
40Eleasa akamzaa Sismai,
Sismai akamzaa Shalumu,
41Shalumu akamzaa Yekamia,
naye Yekamia akamzaa Elishama.
Koo Za Kalebu
42Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa:
Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.
43Hebroni alikuwa na wana wanne:
Kora, Tapua, Rekemu na Shema. 44Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai. 452:45 Yos 15:55; 15:58Shamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri.
46Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi.
47Wana wa Yadai walikuwa:
Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.
48Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana. 492:49 Yos 15:31; 15:16Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa. 502:50 1Nya 4:4; 2:19Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu.
Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa:
Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu, 51Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.
52Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa:
Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi, 532:53 2Sam 23:38pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.
542:54 Ezr 2:22; Neh 12:28Wazao wa Salma walikuwa:
Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wasori, 552:55 Mwa 15:19; Amu 1:16; Yos 19:35; 2Fal 10:15, 23; Yer 35:2-19; Amu 4:11; Hes 24:21-22pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.
以色列的後裔
1以色列的兒子是呂便、西緬、利未、猶大、以薩迦、西布倫、 2但、約瑟、便雅憫、拿弗他利、迦得、亞設。
猶大的後裔
3猶大的兒子是珥、俄南和示拉。這三人是迦南人書亞的女兒生的。猶大的長子珥在耶和華眼中是個邪惡的人,因而被耶和華擊殺了。 4猶大的兒媳她瑪給猶大生了法勒斯和謝拉。猶大共有五個兒子。 5法勒斯的兒子是希斯崙和哈姆勒。 6謝拉的五個兒子是心利、以探、希幔、甲各、大拉。 7迦米的兒子是亞干,這亞干私藏本該毀滅的東西,連累了以色列人。 8以探的兒子是亞撒利雅。
9希斯崙的兒子是耶拉篾、蘭和迦勒2·9 「迦勒」希伯來文是「基路拜」,「迦勒」的另一種拼法。。 10蘭生亞米拿達,亞米拿達生拿順,拿順是猶大人的首領。 11拿順生撒門,撒門生波阿斯, 12波阿斯生俄備得,俄備得生耶西。 13耶西生長子以利押、次子亞比拿達、三子示米亞、 14四子拿坦業、五子拉代、 15六子阿鮮、七子大衛。 16他們的姊妹是洗魯雅和亞比該。洗魯雅的三個兒子是亞比篩、約押和亞撒黑。 17亞比該生亞瑪撒,亞瑪撒的父親是以實瑪利人益帖。
希斯崙的後裔
18希斯崙的兒子迦勒和妻子阿蘇巴生了兒子,他也和耶略生了兒子。阿蘇巴的兒子是耶設、朔罷和押墩。 19阿蘇巴死後,迦勒又娶了以法她,生了戶珥。 20戶珥生烏利,烏利生比撒列。 21希斯崙六十歲娶瑪吉的女兒,與她生了西割。瑪吉是基列的父親。 22西割生雅珥,雅珥在基列有二十三座城邑。 23後來基述人和亞蘭人奪取了雅珥的城邑,包括基納及其附近的六十個村落。這些人都是基列的父親瑪吉的後代。 24希斯崙死在迦勒·以法他後,他的妻子亞比雅給他生了亞施戶。亞施戶是提哥亞的父親。
耶拉篾的後裔
25希斯崙的長子耶拉篾生了長子蘭,又生了布拿、阿連、阿鮮、亞希雅。 26耶拉篾的另一個妻子名叫亞他拉,是阿南的母親。 27耶拉篾的長子蘭的兒子是瑪斯、雅憫和以結。 28阿南的兒子是沙邁和雅大。沙邁的兒子是拿答和亞比述。 29亞比述的妻子名叫亞比孩,他們生了亞班和摩利。 30拿答的兒子是西列和亞遍。西列死後沒有留下兒子。 31亞遍的兒子是以示,以示的兒子是示珊,示珊的兒子是亞來。 32沙邁的兄弟雅大的兒子是益帖和約拿單。益帖死後沒有留下兒子。 33約拿單的兒子是比勒和撒薩。這些人都是耶拉篾的子孫。 34示珊沒有兒子,只有女兒,還有一個名叫耶哈的埃及僕人。 35示珊把女兒嫁給僕人耶哈,他們生了亞太。 36亞太生拿單,拿單生撒拔, 37撒拔生以弗拉,以弗拉生俄備得, 38俄備得生耶戶,耶戶生亞撒利雅, 39亞撒利雅生希利斯,希利斯生以利亞薩, 40以利亞薩生西斯邁,西斯邁生沙龍, 41沙龍生耶加米雅,耶加米雅生以利沙瑪。
迦勒的後裔
42耶拉篾的兄弟迦勒的長子是西弗的父親米沙,希伯崙的父親瑪利沙也是迦勒的兒子。 43希伯崙的兒子是可拉、他普亞、利肯、示瑪。 44示瑪生拉含,拉含是約幹的父親。利肯生沙邁, 45沙邁的兒子是瑪雲,瑪雲是伯·夙的父親。 46迦勒的妾以法生哈蘭、摩撒和迦謝。哈蘭生迦諧。 47雅代的兒子是利健、約坦、基珊、毗力、以法、沙亞弗。 48迦勒的妾瑪迦生示別、特哈拿、 49麥瑪拿的父親沙亞弗、抹比拿和基比亞的父親示法。迦勒的女兒是押撒。 50這些人都是迦勒的子孫。 以法她的長子戶珥生基列·耶琳的父親朔巴、 51伯利恆的父親薩瑪、伯迦得的父親哈勒。 52基列·耶琳的父親朔巴的子孫是哈羅以和半數米努·哈人。 53基列·耶琳的各宗族是以帖人、布特人、舒瑪人、密來人,從這些宗族中又衍生出瑣拉人和以實陶人。 54薩瑪的後代是伯利恆人、尼陀法人、亞他綠·伯·約押人、半數瑪拿哈人、瑣利人, 55以及住在雅比斯的文書世家特拉人、示米押人和蘇甲人。這些都是基尼人,是利甲家族的祖先哈末的後代。