1 Nyakati 19 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 19:1-19

Vita Dhidi Ya Waamoni

(2 Samweli 10:1-19)

119:1 2Nya 20:1-2; Sef 2:8-11; 2Sam 10:1Baada ya muda, Nahashi mfalme wa Waamoni akafa, mwanawe akaingia mahali pake. 2Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alinitendea wema.”

Hivyo Daudi akatuma wajumbe ili kumfariji Hanuni kwa ajili ya kifo cha baba yake. Watu wa Daudi walipofika kwa Hanuni katika nchi ya Waamoni ili kumfariji, 319:3 Hes 21:32wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?” 4Kwa hiyo Hanuni akawakamata watu wa Daudi, akawanyoa ndevu akakata nguo zao katikati kwenye matako, akawaacha waende zao.

519:5 1Fal 16:34; Amu 16:22; Yos 6:24-26Mtu mmoja alipofika na kumpasha Daudi habari za watu hawa, akawatuma wajumbe wengine kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote, ndipo mje.”

619:6 Mwa 34:30; 1Nya 18:3; 1Sam 14:47; 2Sam 8:3; 10:6; 1Fal 11:23Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,00019:6 Talanta 1,000 za fedha ni sawa na tani 34. za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu,19:6 Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi. Aramu-Maaka na Soba. 719:7 Hes 21:30; Yos 13:9-16; Isa 15:2Wakakodisha magari ya vita 32,000 yakiwa na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake, wakaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita.

8Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji. 9Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati wale wafalme wengine waliokuja nao walijipanga kwa vita uwanjani.

10Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli akavipanga dhidi ya Waaramu. 1119:11 1Sam 26:6Akawaweka wale wanajeshi wengine waliobaki chini ya amri ya Abishai ndugu yake, nao wakapangwa ili wakabiliane na Waamoni. 12Yoabu akasema, “Kama Waaramu watanizidi nguvu, basi itakupasa wewe unisaidie; lakini kama Waamoni watakuzidi nguvu, basi mimi nitakusaidia. 1319:13 Isa 30:18; Yer 17:5-8; Za 20:7; 34:22; Mt 16:3, 20Uwe hodari na tupigane kwa ujasiri kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu. Bwana atafanya lile lililo jema machoni pake.”

1419:14 Law 26:7-8; Hes 14:9; Kum 28:7Basi Yoabu na vikosi vyake wakasonga mbele kupigana na Waaramu, nao Waaramu wakakimbia mbele yake. 15Waamoni walipoona Waaramu wanakimbia, nao pia wakakimbia mbele ya nduguye Abishai na kuingia ndani ya mji. Basi Yoabu akarudi Yerusalemu.

1619:16 2Sam 10:16Baada ya Waaramu kuona kwamba wameshindwa na Israeli, wakapeleka wajumbe na kuwataka Waaramu wengine kutoka ngʼambo ya Mto Frati, wakiongozwa na Shofaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri.

17Daudi alipoambiwa haya, akawakusanya Israeli wote na kuvuka Yordani. Akasonga mbele dhidi yao na akajipanga kuwakabili. Daudi akapanga vita ili kupigana na Waaramu, nao wakapigana dhidi yake. 1819:18 Za 33:16; Mit 21:31Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari 7,000 na askari wao wa miguu 40,000. Pia akamuua Shofaki, jemadari wa jeshi lao.

19Raiya wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, wakafanya mapatano ya amani na Daudi, wakawa watumishi wake.

Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志上 19:1-19

大衛擊敗亞捫人和亞蘭人

1後來,亞捫拿轄死了,他兒子繼位。 2大衛說:「我要恩待拿轄的兒子哈嫩,因為他父親曾經恩待我。」他便派臣僕去安慰喪父的哈嫩大衛的臣僕來到亞捫境內要安慰哈嫩3亞捫的官長卻對哈嫩說:「大衛派人來安慰你,你以為他是來弔唁你父親嗎?他的臣僕來見你不過是來探聽虛實,想征服這地方。」 4哈嫩便把大衛的臣僕抓起來,剃去他們一半鬍子,割去他們下身的衣服,然後放走他們。 5消息傳到大衛那裡,他就派人去迎接他們,告訴他們住在耶利哥,等鬍鬚長好了再回來,因為他們倍覺羞辱。

6哈嫩及其他亞捫人知道得罪了大衛,就派人用三十四噸銀子從美索不達米亞亞蘭瑪迦瑣巴招兵買馬, 7雇了三萬二千輛戰車和瑪迦王及其軍隊。他們在米底巴附近紮營,亞捫人也從各城出來準備作戰。 8大衛聽見消息後,就派約押率領全體勇士出戰。 9亞捫人在城門前列陣,來助戰的諸王在郊野列陣。

10約押見自己前後受敵,就從以色列軍中挑選一些精兵迎戰亞蘭人, 11把餘下的軍兵交給他的兄弟亞比篩領導,迎戰亞捫人。 12他對亞比篩說:「倘若我勝不過亞蘭人,你便過來支援我;倘若你勝不過亞捫人,我便過去支援你。 13我們要剛強,為我們的人民和我們上帝的城邑而奮勇作戰。願耶和華成全祂自己的旨意!」 14於是,約押率領軍兵進攻亞蘭人,亞蘭人敗逃。 15亞蘭人敗逃,亞捫人也逃離亞比篩,退回城中。約押便回師耶路撒冷

16亞蘭人見自己敗在以色列人手下,就派使者調來幼發拉底河那邊的亞蘭人,由哈大底謝的將軍朔法率領。 17大衛聽到消息後,就召集以色列全軍,渡過約旦河,列陣與亞蘭人交戰。 18他們擊潰了亞蘭人,殺了七千名戰車兵、四萬步兵,還殺了他們的將軍朔法19哈大底謝的屬下見自己敗於以色列人,便向大衛求和,臣服於他。從此,亞蘭人不敢再支援亞捫人了。