1 Nyakati 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 17:1-27

Ahadi Ya Mungu Kwa Daudi

(2 Samweli 7:1-17)

117:1 Mdo 7:46; 1Nya 15:1Baada ya Daudi kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, akamwambia nabii Nathani, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mierezi, wakati Sanduku la Agano la Bwana liko ndani ya hema.”

217:2 1Nya 22:7; 2Nya 6:7Nathani akamjibu Daudi, “Lolote ulilo nalo moyoni mwako litende, kwa maana Mungu yu pamoja nawe.” 3Usiku ule neno la Mungu likamjia Nathani, kusema:

417:4 1Nya 28:3“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Wewe hutanijengea mimi nyumba ili nikae humo. 517:5 2Sam 6:21; Kut 40:2; 1Fal 8:4, 16Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku ile niliyowatoa Israeli kutoka Misri mpaka leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine na kutoka mahali pamoja hadi pengine. 6Je, popote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wowote nilimwambia kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’ 

717:7 2Sam 6:21“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli. 8Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani. 917:9 2Nya 15:2; Isa 49:17; Yer 31:12; Eze 34:14Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali na nitawapa ili wawe na mahali pao wenyewe pa kuishi na wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni, 1017:10 Amu 2:16na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote.

“ ‘Pamoja na hayo ninakuambia kwamba Bwana atakujengea nyumba: 11Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake. 1217:12 1Fal 5:5; 2Nya 7:18; 13:5Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili yangu, nami nitakifanya imara kiti cha ufalme wake milele. 1317:13 2Kor 6:18; 2Sam 7:14-15; Ebr 1:5; Lk 1:32; 1Nya 28:6; 22:10Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia. 1417:14 1Fal 2:12; 2Nya 9:8; Za 132:11; Yer 33:17; Za 2:6; 89:36; Isa 9:7; Eze 37:25; Dan 2:44; 7:14-27; Mt 21:1-11; Lk 1:33; Ebr 1:8Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’ ”

15Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.

Maombi Ya Daudi

(2 Samweli 7:18-29)

1617:16 2Sam 7:18; 2Fal 19:14; Ay 7:14-17; Mwa 32:10; Za 144:3Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema:

“Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? 17Kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Mungu, umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Umeniangalia kama mtu aliyetukuka kuliko watu wote, Ee Bwana Mungu.

1817:18 Za 139:1; Yn 21:17“Daudi aweza kukuambia nini zaidi kuhusu kumheshimu mtumishi wako? Kwa maana wewe unamjua mtumishi wako, 1917:19 2Sam 7:16-17, 25; 2Fal 20:6; Mt 11:26; Efe 1:11Ee Bwana Mungu. Kwa ajili ya mtumishi wako, tena sawasawa na mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa sana na kujulisha ahadi hizi zote zilizo kubwa sana.

2017:20 Kut 8:10; Kum 3:24; Isa 44:6; Kut 15:11; Kum 33:26; 1Sam 2:2; 2Sam 7:22; Za 86:8“Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana Mungu, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe. 2117:21 Kut 6:6Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli: taifa pekee duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri? 2217:22 Kut 19:5-6Uliwafanya watu wako Israeli kuwa watu wako wewe mwenyewe milele, nawe, Ee Bwana Mungu, umekuwa Mungu wao.

2317:23 1Fal 8:25“Sasa basi, Bwana ahadi uliyoweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake na uithibitishe milele. Fanya kama ulivyoahidi, 2417:24 2Nya 6:33; Yn 12:28; Za 21:13; 72:19; Mt 6:9, 13ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako.

25“Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya. 2617:26 Kut 34:6; Ebr 6:18Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu! Umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri. 2717:27 Za 16:11; 21:6; Rum 11:29; Mwa 27:33; Za 72:17Basi imekupendeza kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu milele machoni pako; kwa ajili yako, Ee Bwana, umeibariki, nayo itabarikiwa milele.”