1 Nyakati 16 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 16:1-43

Sanduku Lawekwa Ndani Ya Hema

116:1 2Sam 6:17-19Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 216:2 Kut 39:43; Hes 6:23-27Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la Bwana. 3Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu.

416:4 1Nya 15:1-2Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli: 5Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi, 6nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.

Zaburi Ya Daudi Ya Shukrani

(Zaburi 105:1-15; 96:1-13; 106:1, 47-48)

716:7 2Sam 23:1; Za 47:7Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana:

816:8 Za 107:1; 118:1; 2Fal 19:19Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;

wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.

916:9 Za 100:1; Kut 15:1; Za 7:17; 95:1-2Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa;

waambieni matendo yake yote ya ajabu.

1016:10 Za 34:3; Isa 45:25Lishangilieni jina lake takatifu;

mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.

1116:11 Za 27:8; Mit 8:17; Amo 5:6-14Mtafuteni Bwana na nguvu zake;

utafuteni uso wake siku zote.

1216:12 Za 78:43; 103:2Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,

miujiza yake na hukumu alizozitamka,

13enyi wazao wa Israeli mtumishi wake,

enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

1416:14 Isa 29:9; 4:4Yeye ndiye Bwana Mungu wetu;

hukumu zake zimo duniani pote.

15Hulikumbuka agano lake milele,

neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,

1616:16 Mwa 17:2; Neh 9:8; Ebr 6:13-18; Za 105:8-10; Mwa 15:18; 26:3agano alilolifanya na Abrahamu,

kiapo alichomwapia Isaki.

1716:17 Mwa 35:9-12Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,

kwa Israeli liwe agano la milele:

1816:18 Mwa 13:14-17“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani

kuwa sehemu utakayoirithi.”

1916:19 Mwa 34:30; Ebr 11:13; Kum 7:7Walipokuwa wachache kwa idadi,

wachache sana na wageni ndani yake,

20walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,

kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.

2116:21 Mwa 20:3; Kut 7:15-18; Za 9:5; Mwa 12:17Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;

kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:

2216:22 Mwa 20:7; Za 105; 15; 1Yn 2:27“Msiwaguse niliowatia mafuta;

msiwadhuru manabii wangu.”

2316:23 Za 47:1; 96:1Mwimbieni Bwana dunia yote;

tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

2416:24 Isa 12:4Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,

matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

2516:25 Za 18:3; 76:7; 89:7; Kut 18:11; Isa 40:25-26; Za 24:8Kwa kuwa Bwana ni mkuu,

mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;

yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

2616:26 Law 19:4; Isa 45:20; 1Kor 8:4; Za 115:4-8; Yer 10:3Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,

lakini Bwana aliziumba mbingu.

27Fahari na enzi viko mbele yake;

nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

2816:28 Za 29:1-2; 8:1Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa,

mpeni Bwana utukufu na nguvu,

29mpeni Bwana utukufu

unaostahili jina lake.

Leteni sadaka na mje katika nyua zake;

mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.

3016:30 Za 2:11; 33:8Dunia yote na itetemeke mbele zake!

Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa.

3116:31 Isa 44:23; 35:10; 49:13; Mao 5:19; Isa 52:7; Lk 2:13; Ufu 14:2Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;

semeni katikati ya mataifa, “Bwana anatawala!”

3216:32 Kut 20:11; Za 98:7; 96:10Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;

mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake.

3316:33 Isa 14:8; 55:12; Za 110:6Kisha miti ya msituni itaimba,

itaimba kwa furaha mbele za Bwana,

kwa maana anakuja kuihukumu dunia.

3416:34 Isa 12:4; Za 25:7; Ezr 3:11; Yer 33:1Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

3516:35 Kum 32:15; Mik 7:7; Ezr 3:11; Yer 33:11; Za 106:47Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe.

Tukusanye tena na utukomboe kutoka kwa mataifa,

ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu,

na kushangilia katika sifa zako.”

3616:36 Kum 27:15; 1Fal 8:15; Neh 8:6; 10:27; 2Nya 8:14; Za 72:18-19Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli,

tangu milele na hata milele.

Nao watu wote wakasema, “Amen,” na “Msifuni Bwana.”

37Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano la Bwana ili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku. 3816:38 1Nya 13:13; 26:4-10Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango.

3916:39 1Sam 2:35; 1Nya 21:29; 2Sam 8:17; Yos 9:3; 1Fal 3:4Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada ya Bwana katika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni 4016:40 Kut 29:38; Hes 28:1-8ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Bwana kwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria ya Bwana ambayo alikuwa amempa Israeli. 4116:41 1Nya 15:19; 2Nya 5:13; Yak 5:11; Ezr 3:11; Neh 9:17; Za 25:10; 33:5; Yer 33:11; Yoe 2:13; Lk 3:36Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa Bwana shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.” 4216:42 2Nya 7:6Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni.

4316:43 2Sam 6:19-20; Mwa 18:19; Yos 24:15Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake.