1 Nyakati 14 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 14:1-17

Nyumba Ya Daudi Na Jamaa Yake

(2 Samweli 5:11-16)

114:1 1Fal 5:6; Hag 1:8; 2Sam 5:11Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, waashi na maseremala ili kumjengea jumba la kifalme. 214:2 Hes 24:7; Kum 26:19Naye Daudi akatambua kwamba Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na kwamba ufalme wake umetukuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake.

314:3 1Nya 3:1; Kum 17:14-17Huko Yerusalemu Daudi akaoa wake wengine zaidi na akawa baba wa wana na mabinti wengi. 414:4 2Sam 5:14; 1Nya 3:5Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, 5Ibihari, Elishua, Elpeleti, 6Noga, Nefegi, Yafia, 7Elishama, Beeliada na Elifeleti.

Daudi Awashinda Wafilisti

(2 Samweli 5:17-25)

814:8 1Nya 11:1; 2Sam 5:17; Za 2:1-5Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao. 914:9 Yos 15:8; 1Nya 11:15Basi Wafilisti walikuwa wameingia na kushambulia Bonde la Warefai, 10Hivyo Daudi akamuuliza Mungu: “Je, niende kuwashambulia hao Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”

Bwana akamjibu, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”

1114:11 Za 94:16; Isa 28:21Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu,14:11 Maana yake ni Bwana Afurikae. akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu. 1214:12 Kut 32:20; Yos 7:15Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto.

1314:13 2Sam 5:22Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde; 1414:14 Yos 8:6-7; 2Sam 5:23hivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi. 15Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.” 1614:16 Yos 9:3; 10:33; 2Sam 5:25Kwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri.

1714:17 Yos 6:27; 2Nya 26:8; Kum 2:25; Za 2:1-12Hivyo umaarufu wa Daudi ukaenea katika kila nchi, naye Bwana akayafanya mataifa yote kumwogopa Daudi.