1 Nyakati 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 13:1-14

Kurudishwa Kwa Sanduku La Mungu

(2 Samweli 6:1-11)

113:1 1Nya 12:14; Za 132:1; Mit 15:22Daudi alishauriana na kila afisa wake, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia. 213:2 1Nya 10:7; Isa 37:4Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote la Israeli, “Kama mkiona ni vyema, na kama ni mapenzi ya Bwana Mungu wetu, tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu wengine walio mbali na walio karibu katika nchi yote ya Israeli, pia kwa makuhani na Walawi walio pamoja nao katika miji yao na katika sehemu zao za malisho yao, waje waungane na sisi. 313:3 1Sam 7:1-2; 2Nya 1:5; 1Sam 23:2-4Sisi na tulirudishe Sanduku la Mungu wetu kwetu kwa maana hatukujali wakati wa utawala wa Sauli.” 4Kusanyiko lote likakubaliana kufanya hivyo, kwa sababu ilionekana vyema kwa watu wote.

513:5 1Nya 11:1; 15:3; Yos 13:3; Hes 13:21; 1Sam 6:21; 7:2Basi Daudi akawakusanya Waisraeli wote, kuanzia Mto Shihori ulioko Misri hadi Lebo-Hamathi, ili kulileta Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu. 613:6 Yos 15:9; 2Sam 6:2; Kut 25:22; 2Fal 19:15; 1Sam 4:4Daudi akiwa pamoja na Waisraeli wote wakaenda Baala ya Yuda (yaani Kiriath-Yearimu) kulipandisha Sanduku la Mungu Bwana, yeye anayeketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi: Sanduku linaloitwa kwa Jina lake, kutoka huko.

713:7 Hes 4:15; 1Sam 7:1Wakalisafirisha Sanduku la Mungu kwa gari jipya la kukokotwa na maksai kutoka nyumba ya Abinadabu, Uza na Ahio wakiliongoza gari hilo. 813:8 2Sam 6:5; Za 92:3Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.

913:9 2Sam 6:6Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Kidoni, Uza akaunyoosha mkono wake ili kulizuia Sanduku, kwa sababu maksai walijikwaa. 1013:10 1Nya 15:13, 15; Law 10:2; Hes 4:15Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Uza, akampiga kwa sababu aliuweka mkono wake kwenye Sanduku. Kwa hiyo akafa pale mbele za Mungu.

1113:11 1Nya 15:13; Za 7:11Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu ya Bwana ilifurika dhidi ya Uza, mahali pale pakaitwa Peres-Uza13:11 Maana yake ni Gadhabu dhidi ya Uza. hadi leo.

12Siku ile Daudi akamwogopa Mungu naye akauliza. “Nitawezaje kulichukua Sanduku la Mungu kwangu?” 1313:13 1Nya 15:18, 24; 16:38; 26:4-5, 15Hakulichukua hilo Sanduku akae nalo katika Mji wa Daudi. Badala yake, akalipeleka nyumbani kwa Obed-Edomu, Mgiti. 1413:14 2Sam 6:11; 1Nya 26:4-5; Mwa 30:27; 39:5; 1Nya 26:5; Za 37:22; Mit 3:9; 10:22; Mal 3:10Sanduku la Mungu likabaki pamoja na jamaa ya Obed-Edomu, nyumbani kwake kwa miezi mitatu, naye Bwana akaibariki nyumba yake pamoja na kila kitu alichokuwa nacho.