1 Nyakati 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 11:1-47

Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Israeli

(2 Samweli 5:1-10)

111:1 1Nya 9:1; Mwa 13:18; 23:19; 2Sam 5:1; 1Nya 12:23Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako. 211:2 1Sam 18:5, 16; Za 78:71; Mt 2:6; 1Nya 5:2Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye Bwana Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”

311:3 1Sam 16:1-13; 2Sam 5:3; Rum 8:31Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na Bwana alivyoahidi kupitia kwa Samweli.

Daudi Ateka Yerusalemu

411:4 Yos 3:10; Amu 1:21; 2Sam 5:6; Mwa 10:16; 15:21; Kut 3:17; Amu 19:10Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi walioishi humo 5wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.

611:6 2Sam 2:13; 8:16Daudi alikuwa amesema, “Yeyote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu.

711:7 2Sam 5:7Daudi akafanya makao yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi. 811:8 2Sam 5:9; 2Nya 32:5Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu. 911:9 2Sam 3:1; Es 9:4Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Bwana Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye.

Mashujaa Wa Daudi

(2 Samweli 23:8-39)

1011:10 1Nya 11:1; 12:23; 2Sam 23:8; 1Sam 16:1, 12Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama Bwana alivyoahidi. 1111:11 2Sam 17:10Hii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi:

Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja.

12Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu. 1311:13 1Sam 17:1Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti. 1411:14 Kut 14:30; 1Sam 17:10; Mit 21:31Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.

1511:15 1Nya 14:9Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai. 1611:16 2Sam 5:17Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu. 17Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!” 1811:18 Kum 12:16Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana. 19Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa.

Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.

2011:20 1Sam 26:6Abishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu. 2111:21 2Sam 23:24; 1Nya 27:7Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

2211:22 Yos 15:21; 1Sam 17:36; 2Sam 1:23; 23:20; 1Nya 12:8Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba. 2311:23 1Sam 26:6Alimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano.11:23 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao. 24Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu. 25Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

2611:26 1Nya 2:18; 2Sam 23:24; 1Nya 27:7Wale watu mashujaa walikuwa:

Asaheli nduguye Yoabu,

Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,

2711:27 1Nya 27:8Shamothi Mharori,

Helesi Mpeloni,

2811:28 1Nya 27:12Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa,

Abiezeri kutoka Anathothi,

2911:29 2Sam 21:18Sibekai Mhushathi,

Ilai Mwahohi,

30Maharai Mnetofathi,

Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi,

3111:31 1Nya 27:14; Amu 12:13Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini,

Benaya Mpirathoni,

32Hurai kutoka mabonde ya Gaashi,

Abieli Mwaribathi,

33Azmawethi Mbaharumi,

Eliaba Mshaalboni,

34wana wa Hashemu Mgiloni,

Yonathani mwana wa Shagee Mharari,

35Ahiamu mwana wa Sakari Mharari,

Elifale mwana wa Uru,

36Heferi Mmekerathi,

Ahiya Mpeloni,

37Hezro Mkarmeli,

Naarai mwana wa Ezbai,

38Yoeli nduguye Nathani,

Mibhari mwana wa Hagri,

39Seleki Mwamoni,

Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,

4011:40 Yos 15:48; 1Nya 2:50-53Ira Mwithiri,

Garebu Mwithiri,

4111:41 2Sam 11:6; 1Nya 2:36Uria Mhiti,

Zabadi mwana wa Alai,

42Adina mwana wa Shiza Mreubeni, ambaye alikuwa mkuu wa Wareubeni, akiwa pamoja na watu thelathini,

43Hanani mwana wa Maaka,

Yoshafati Mmithni,

4411:44 Kum 1:4Uzia Mwashterathi,

Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri,

45Yediaeli mwana wa Shimri,

nduguye Yoha Mtizi,

46Elieli Mmahawi,

Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu,

Ithma Mmoabu,

47Elieli, na Obedi na Yaasieli Mmesobai.