1 Nyakati 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 1:1-54

Kumbukumbu Za Historia Kuanzia Adamu Hadi Abrahamu

(Mwanzo 5:1-32; 10:1-32; 11:10-26)

Adamu Hadi Wana Wa Noa

11:1 Mwa 5:1-32; Lk 3:36-38Adamu, Sethi, Enoshi, 21:2 Mwa 5:9; 5:12; 5:15Kenani, Mahalaleli, Yaredi, 31:3 Mwa 5:18; Yud 14; Mwa 5:21; 5:25; 5:29Enoki, Methusela, Lameki, Noa.

41:4 Mwa 6:10; 10:1; 5:32Wana wa Noa walikuwa:

Shemu, Hamu na Yafethi.

Wana Wa Yafethi

5Wana wa Yafethi walikuwa:

Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

6Wana wa Gomeri walikuwa:

Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

7Wana wa Yavani walikuwa:

Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

Wana Wa Hamu

81:8 Mwa 16:10Wana wa Hamu walikuwa:

Kushi, Misraimu,1:8 Yaani Misri. Putu na Kanaani.

9Wana wa Kushi walikuwa:

Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.

Wana wa Raama walikuwa:

Sheba na Dedani.

101:10 Mwa 10:8, 13Kushi akamzaa

Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.

11Misraimu akawazaa:

Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 121:12 Mwa 10:14; Kum 2:23; Yer 47:4; Amo 9:7Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.

13Wana wa Kanaani walikuwa:

Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, 14Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 15Wahivi, Waariki, Wasini, 16Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Wana Wa Shemu

171:17 Mwa 9:23-26; 10:22; 11:10Wana wa Shemu walikuwa:

Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

Wana wa Aramu walikuwa:

Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

18Arfaksadi akamzaa Shela,

Shela akamzaa Eberi.

19Eberi alipata wana wawili:

Mmoja wao aliitwa Pelegi,1:19 Pelegi maana yake Mgawanyiko. kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

20Wana wa Yoktani walikuwa:

Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 21Hadoramu, Uzali, Dikla, 22Obali, Abimaeli, Sheba, 23Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.

241:24 Mwa 10:21-29; Lk 3:34-36Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,

251:25 Mwa 11:15; Hes 24:24; Lk 3:35Eberi, Pelegi, Reu,

26Serugi, Nahori, Tera,

271:27 Mwa 17:5; 2Nya 20:7; Isa 41:8; 51:2; Rum 4:16Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu).

Jamaa Ya Abrahamu

281:28 Mwa 21:2-3; 16:11, 15Abrahamu alikuwa na wana wawili:

Isaki na Ishmaeli.

Wazao Wa Hagari

(Mwanzo 25:12-16)

291:29 Mwa 25:13-26Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari:

Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 30Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, 31Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.

Wazao Wa Ketura

321:32 Mwa 22:24; 10:7Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa:

Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.

Wana wa Yokshani walikuwa:

Sheba na Dedani.

33Wana wa Midiani walikuwa:

Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.

Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.

Wazao Wa Sara

341:34 Lk 3:34; Mwa 21:2-3; Mdo 7:8; Mwa 18:5; 25:25-26Abrahamu alikuwa baba wa Isaki.

Wana wa Isaki walikuwa:

Esau na Israeli.

Wana Wa Esau

(Mwanzo 36:1-19)

351:35 Mwa 36:19; 36:4; Kum 2:22; Rum 9:13; Ebr 12:16; Mal 1:2-3Wana wa Esau walikuwa:

Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.

361:36 Kut 17:14; Mwa 36:11Wana wa Elifazi walikuwa:

Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;

Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.

371:37 Mwa 36:17Wana wa Reueli walikuwa:

Nahathi, Zera, Shama na Miza.

Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu

(Mwanzo 36:20-30)

381:38 Mwa 36:20Wana wa Seiri walikuwa:

Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.

391:39 Mwa 36:22Wana wa Lotani walikuwa wawili:

Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.

401:40 Mwa 36:2Wana wa Shobali walikuwa:

Alvani,1:40 Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian. Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.

Wana wa Sibeoni walikuwa:

Aiya na Ana.

411:41 Mwa 36:25-26Mwana wa Ana alikuwa:

Dishoni.

Nao wana wa Dishoni walikuwa:

Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

42Wana wa Eseri walikuwa:

Bilhani, Zaavani na Akani.

Wana wa Dishani walikuwa:

Usi na Arani.

Watawala Wa Edomu

(Mwanzo 36:31-43)

431:43 Mwa 36:31; 49:10Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:

Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.

44Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.

451:45 Mwa 36:11Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.

461:46 1Fal 11:14Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.

47Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.

481:48 Mwa 36:37Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.

49Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.

501:50 Mwa 36:39Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. 511:51 Mwa 36:40; Kut 15:15Naye Hadadi pia akafa.

Wakuu wa Edomu walikuwa:

Timna, Alva, Yethethi, 52Oholibama, Ela, Pinoni, 53Kenazi, Temani, Mibsari, 54Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.