Mwanzo 1 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 1:1-31

Siku Sita Za Uumbaji Na Sabato

11:1 Za 89:11; 90:2; 96:5; 102:25; Mit 8:23; Isa 40:21; 42:5; 51:13; 41:4, 26; Yn 1:1-2; Mwa 2:3; 14:19; Neh 9:6; Ay 9:8; 37:18; Yer 10:12; 32:17; 51:15; 2Fal 19:15; Mdo 14:15; 7:24; Efe 3:9; Kol 1:16; Ebr 1:10; 3:4; 11:3; Ufu 4:11; 10:6Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. 21:2 Isa 24:10; 27:10; 31:5; 32:14, 15; 34:11; 45:18; Yer 4:23; Mwa 8:2; Ay 7:12; 26:8; 33:4; 38:9; Za 36:6; 42:7; 104:6, 30; Mit 30:4Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

31:3 Za 33:6-9; 148:5; Ebr 11:3; 2Kor 4:6; 1Yn 5:7Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. 41:4 Za 18:28; 105:8; 104:31; 119:68; Yer 31:35; Kut 10:21-23; Ay 26:10; 8:19; Isa 42:16; 45:7Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. 51:5 Mwa 2:19, 23; Za 74:16Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

61:6 Isa 44:24; 2Pet 3:5; Za 24:2; 136:6Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.” 71:7 Mwa 7:11; Ay 26:10; 38:8-16; Za 68:33; 148:4; Mit 8:28Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo. 81:8 Ay 38:8-11; Za 33:7; 95:5; 104:6-9; Mit 8:29; Yer 5:22; 2Pet 3:5; Hag 2:6Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.

9Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo. 101:10 Za 33:7; 90:2; 95:5; Ay 38:8Mungu akaiita nchi kavu “ardhi,” nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.

111:11 Za 65:9-13; 104:14; Mwa 2:9; Law 11:14, 19; 1Kor 15:38Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo. 12Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema. 13Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu.

141:14 Za 74:16; 136:7; 104:19; Yer 10:2; Mwa 8:22; Yer 31:35-36; 33:20, 25Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka, 15nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia.” Ikawa hivyo. 161:16 Kum 17:3; Ay 38:33; 31:26; Yer 31:35; 43:13; Eze 8:16; Za 74:16; 104:19; 136:9; Yak 1:17; Kum 4:19Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota. 17Mungu akaiweka katika nafasi ya anga iangaze dunia, 181:18 Yer 33:20itawale usiku na mchana, na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema. 19Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya nne.

201:20 Za 146:6; Mwa 2:19Mungu akasema, “Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga.” 211:21 Ay 3:8; 7:12; Za 74:13; 148:7; 104:25-26; Isa 27:1; Eze 32:2Kwa hiyo Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema. 221:22 Mwa 8:17; 47:27; 9:17, 19; Law 26:9; Eze 36:11Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia.” 23Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tano.

241:24 Mwa 2:19Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo. 251:25 Mwa 7:21-22; Yer 27:5Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, wanyama wa kufugwa kulingana na aina zake, na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.

261:26 Mwa 5:3; 9:6; 9:2; Za 8:5-8; 8:8; 82:6; 89:6; Yak 3:9; 1Kor 11:7; 2Kor 4:4; Kol 1:15; 3:10; Mdo 17:28-29Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.”

271:27 Mwa 2:7; 5:1, 2; Za 103:14; 119:73; Mt 19:4; Mk 10:6; Gal 3:28; Kum 4:32Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe,

kwa mfano wa Mungu alimuumba;

mwanaume na mwanamke aliwaumba.

281:28 Mwa 6:1; 17:6; 33:5; Yos 24:3; Mdo 17:26; Za 8:6-8; 115:16; 113:9; 127:3, 5Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.”

291:29 Mwa 9:3; 1Tim 4:3; Kum 12:15; Za 104:14Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote, na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa chakula chenu. 301:30 Mwa 2:7; 7:22; Ay 38:41; Za 78:25; 104:14, 27; 111:5; 136:25; 145:15Nao wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.

311:31 Za 104:24; 136:5; Mhu 3:19; Yer 10:12; 1Tim 4:4Mungu akaona vyote alivyoumba, na tazama, ilikuwa vizuri sana. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya sita.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

創世記 1:1-31

上帝創造天地

1太初,上帝創造了天地。 2那時,大地空虛混沌,還沒有成形,黑暗籠罩著深淵,上帝的靈運行在水面上。 3上帝說:「要有光!」就有了光。 4上帝看光是好的,就把光和暗分開, 5稱光為晝,稱暗為夜。晚上過去,早晨到來,這是第一天1·5 這是第一天」或譯「這是一天」。6上帝說:「水與水之間要有穹蒼,把水分開。」 7果然如此。上帝開闢了穹蒼,用穹蒼將水上下分開。 8上帝稱穹蒼為天空。晚上過去,早晨到來,這是第二天。

9上帝說:「天空下面的水要聚在一處,使乾地露出來。」果然如此。 10上帝稱乾地為陸地,稱水匯聚的地方為海洋。上帝看了,感到滿意。 11上帝說:「陸地要長出植物——各類結種子的菜蔬和結果子的樹木,果子內都有籽。」果然如此, 12陸地長出了植物——各類結種子的菜蔬和結果子的樹木,果子內都有籽。上帝看了,感到滿意。 13晚上過去,早晨到來,這是第三天。

14上帝說:「天空要有光體,以區分晝夜,作記號,定節令,計算年日, 15發光普照大地。」果然如此。 16上帝造了兩個大光體,較大的管白晝,較小的管黑夜,又造了星辰。 17上帝把這些光體擺列在天空,讓它們發光普照大地, 18管理晝夜,分開明暗。上帝看了,感到滿意。 19晚上過去,早晨到來,這是第四天。

20上帝說:「水中要充滿各種動物,空中要有禽鳥飛翔。」 21上帝就造了海中的大魚等各類水族和各類禽鳥。上帝看了,感到滿意。 22上帝賜福給這一切生物,說:「水族要生養繁殖,充滿海洋,禽鳥也要在地上多多地繁殖。」 23晚上過去,早晨到來,這是第五天。 24上帝說:「大地要繁衍各類動物——各類的牲畜、爬蟲和野獸。」果然如此。 25上帝造了各類的野獸、牲畜和爬蟲。上帝看了,感到滿意。

上帝照自己的形像造人

26上帝說:「我們要照著我們的形像,按著我們的樣子造人,讓他們管理海裡的魚、空中的鳥和地上的牲畜及一切爬蟲。」 27上帝就照著自己的形像造了人,祂照著自己的形像造了男人和女人。 28上帝賜福給他們,對他們說:「你們要生養眾多,遍佈地面,治理大地,管理海裡的魚、空中的鳥以及地上的各種動物。」 29上帝對人說:「看啊,我把地上所有結種子的菜蔬和所有樹上有籽的果子都賜給你們作食物。 30我把植物賜給所有地上的走獸、空中的飛鳥及地上的爬蟲作食物。」果然如此。 31上帝看了,感到非常滿意。晚上過去,早晨到來,這是第六天。