الْمَزْمُورُ السَّبْعُونَ
لِقَائِدِ الْمُنْشِدِينَ مَزْمُورٌ لِدَاوُدَ. لِلتَّذْكِيرِ
1هَلُمَّ أَنْقِذْنِي يَا رَبُّ، وَأَسْرِعْ إِلَى مَعُونَتِي. 2لِيَخْزَ وَيَخْجَلِ السَّاعُونَ إِلَى قَتْلِي. لِيَرْتَدَّ وَيَخْجَلِ السَّاعُونَ لأَذِيَّتِي. 3لِيَرْجِعِ السَّاخِرُونَ مِنِّي مُكَلَّلِينَ بِالْعَارِ. 4لِيَفْرَحْ وَيَبْتَهِجْ بِكَ جَمِيعُ طَالِبِيكَ. وَلْيَقُلْ دَائِماً مُحِبُّو خَلاصِكَ: لِيَتَعَظَّمِ الرَّبُّ. 5إِنَّمَا أَنَا مُتَضَايِقٌ وَمُحْتَاجٌ، فَأَسْرِعِ الْلَهُمَّ إِلَيَّ. أَنْتَ عَوْنِي وَمُنْقِذِي. يَا رَبُّ لَا تَتَبَاطَأْ.
Zaburi 70
Kuomba Msaada
(Zaburi 40:13-17)
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.
170:1 Za 35:4; 6:10; 35:26; 71:12; 109:29; 129:5Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
270:2 Za 35:2Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
3Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
470:4 Za 31:6, 7; 35:27; 32:11; 118:24; 9:10Lakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
“Mungu na atukuzwe!”
570:5 Za 109:22; 141:1; 30:10; 86:1; 33:10; 18:2; 119:60Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
Ee Bwana, usikawie.