New American Standard Bible

1 Thessalonians 3

Encouragement of Timothy’s Visit

1Therefore when we could endure it no longer, we thought it best to be left behind at Athens alone, and we sent Timothy, our brother and God’s fellow worker in the gospel of Christ, to strengthen and encourage you as to your faith, so that no one would be [a]disturbed by these afflictions; for you yourselves know that we have been destined for this. For indeed when we were with you, we kept telling you in advance that we were going to suffer affliction; [b]and so it came to pass, [c]as you know. For this reason, when I could endure it no longer, I also sent to [d]find out about your faith, for fear that the tempter might have tempted you, and our labor would be in vain.

But now that Timothy has come to us from you, and has brought us good news of your faith and love, and that you always think kindly of us, longing to see us just as we also long to see you, for this reason, brethren, in all our distress and affliction we were comforted about you through your faith; for now we really live, if you stand firm in the Lord. For what thanks can we render to God for you in return for all the joy with which we rejoice before our God on your account, 10 as we night and day keep praying most earnestly that we may see your face, and may complete what is lacking in your faith?

11 Now may our God and Father Himself and Jesus our Lord direct our way to you; 12 and may the Lord cause you to increase and abound in love for one another, and for all people, just as we also do for you; 13 so that He may establish your hearts without blame in holiness before our God and Father at the [e]coming of our Lord Jesus with all His [f]saints.

Footnotes

  1. 1 Thessalonians 3:3 Or deceived
  2. 1 Thessalonians 3:4 Lit just as
  3. 1 Thessalonians 3:4 Lit and
  4. 1 Thessalonians 3:5 Or to know, to ascertain
  5. 1 Thessalonians 3:13 Or presence
  6. 1 Thessalonians 3:13 Or holy ones

Neno: Bibilia Takatifu

1 Wathesalonike 3

Timotheo Atumwa Kwenda Thesalonike

1Hatimaye tuliposhindwa kuvumilia zaidi, tuliona afadhali tubaki Athene peke yetu. Tukamtuma Timotheo ambaye ni ndugu yetu na mtumishi wa Mungu katika kuieneza Habari Njema ya Kristo, aje kuwaimarisha na kuwatia moyo ili asije mtu akababaishwa na mateso haya. Kama mjuavyo, tumepangiwa mateso. Hata tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaambia mara kwa mara kwamba tutateswa, na kama mjuavyo ndivyo ilivyokuwa. Ndio maana niliposhindwa kuvumilia nilituma mtu ili nifahamu msimamo wenu katika imani. Niliogopa kuwa pengine yule mjaribu shetani alikuwa amewajaribu na kwamba pengine juhudi yetu kwenu ingekuwa ni bure.

Taarifa Ya Timotheo

Lakini sasa Timotheo amekwisha rejea kutoka kwenu na ameleta taarifa nzuri kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuam bia kwamba mnatukumbuka kwa wema na kwamba mna hamu siku zote kutuona kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaona. Kwa sababu hiyo ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa ajili yenu, kutokana na imani yenu. Maana sasa hakika tunaishi kwa kuwa ninyi mmesimama imara katika Bwana. Tutawezaje kumshu kuru Mungu kiasi cha kutosha kwa ajili yenu, kutokana na furaha tuliyo nayo mbele za Mungu wetu kwa sababu yenu? 10 Usiku na mchana tunaomba kwa bidii ili tuwezeshwe kuwaona tena na kuwapa tieni kile ambacho bado kinapungua katika imani yenu.

11 Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe na Bwana wetu Yesu atutayarishie njia ya kuja kwenu. 12 Bwana na awawezeshe ninyi kupendana zaidi na zaidi na kuwapenda watu wote kama sisi tunav yowapenda ninyi. 13 Tunamwomba awaimarisheni mioyo ili msiwe na lawama bali muwe watakatifu mbele za Mungu Baba yetu, wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na watakatifu wake wote.