Revelation 22 – KJV & NEN

King James Version

Revelation 22:1-21

1And he shewed me a pure river of water of life, clear as crystal, proceeding out of the throne of God and of the Lamb. 2In the midst of the street of it, and on either side of the river, was there the tree of life, which bare twelve manner of fruits, and yielded her fruit every month: and the leaves of the tree were for the healing of the nations. 3And there shall be no more curse: but the throne of God and of the Lamb shall be in it; and his servants shall serve him: 4And they shall see his face; and his name shall be in their foreheads. 5And there shall be no night there; and they need no candle, neither light of the sun; for the Lord God giveth them light: and they shall reign for ever and ever.

6And he said unto me, These sayings are faithful and true: and the Lord God of the holy prophets sent his angel to shew unto his servants the things which must shortly be done. 7Behold, I come quickly: blessed is he that keepeth the sayings of the prophecy of this book. 8And I John saw these things, and heard them. And when I had heard and seen, I fell down to worship before the feet of the angel which shewed me these things. 9Then saith he unto me, See thou do it not: for I am thy fellowservant, and of thy brethren the prophets, and of them which keep the sayings of this book: worship God. 10And he saith unto me, Seal not the sayings of the prophecy of this book: for the time is at hand. 11He that is unjust, let him be unjust still: and he which is filthy, let him be filthy still: and he that is righteous, let him be righteous still: and he that is holy, let him be holy still. 12And, behold, I come quickly; and my reward is with me, to give every man according as his work shall be. 13I am Alpha and Omega, the beginning and the end, the first and the last. 14Blessed are they that do his commandments, that they may have right to the tree of life, and may enter in through the gates into the city. 15For without are dogs, and sorcerers, and whoremongers, and murderers, and idolaters, and whosoever loveth and maketh a lie. 16I Jesus have sent mine angel to testify unto you these things in the churches. I am the root and the offspring of David, and the bright and morning star. 17And the Spirit and the bride say, Come. And let him that heareth say, Come. And let him that is athirst come. And whosoever will, let him take the water of life freely.

18For I testify unto every man that heareth the words of the prophecy of this book, If any man shall add unto these things, God shall add unto him the plagues that are written in this book: 19And if any man shall take away from the words of the book of this prophecy, God shall take away his part out of the book of life, and out of the holy city, and from the things which are written in this book. 20He which testifieth these things saith, Surely I come quickly. Amen. Even so, come, Lord Jesus. 21The grace of our Lord Jesus Christ be with you all. Amen.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ufunuo 22:1-21

Mto Wa Maji Ya Uzima

122:1 Ufu 4:6; Eze 47:1; Zek 14:8Kisha yule malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima, maangavu kama kioo yakitiririka kutoka kwenye kile kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo, 222:2 Ufu 2:7; Eze 47:12kupitia katikati ya barabara kuu ya huo mji. Kwenye kila upande wa huo mto kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, ukizaa matunda yake kila mwezi. Nayo majani ya mti huo ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa. 322:3 Zek 14:11; Ufu 7:15Katika mji huo hakutakuwa tena na laana, bali kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo humo na watumishi wake watamtumikia, 422:4 Mt 5:8; Ufu 14:1nao watamwona uso wake na Jina lake litakuwa kwenye vipaji vya nyuso zao. 522:5 Ufu 21:23, 25; 20:4; Dan 7:27Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, kwa maana Bwana Mungu atakuwa nuru yao, nao watatawala milele na milele.

622:6 Ufu 1:1; 19:9; 21:5; Ebr 12:9Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutukia upesi.”

Bwana Yesu Anakuja

722:7 Ufu 3:11; 1:3; Mt 16:27; Ufu 22:10, 18, 19“Tazama, naja upesi! Amebarikiwa yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.”

822:8 Ufu 1:1; 19:10Mimi, Yohana, ndiye niliyesikia na kuyaona mambo haya. Nami nilipokwisha kuyasikia na kuyaona, nilianguka chini nikasujudu miguuni pa yule malaika aliyekuwa akinionyesha mambo hayo. 922:9 Ufu 19:10; 22:10, 18, 19Lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi ni mtumishi pamoja nawe na ndugu zako manabii na wote wanaoyashika maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu!”

1022:10 Dan 8:26; Ufu 10:4; 1:3Kisha akaniambia, “Usiyafunge maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, kwa sababu wakati umekaribia. 1122:11 Eze 3:27; Dan 12:10Atendaye mabaya na aendelee kutenda mabaya, aliye mchafu na aendelee kuwa mchafu, yeye atendaye haki na aendelee kutenda haki, na yeye aliye mtakatifu na aendelee kuwa mtakatifu.”

1222:12 Isa 14:10; Mt 16:27; Isa 62:11“Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda. 1322:13 Ufu 1:8, 17; 21:6Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.

1422:14 Ufu 2:7; 21:12, 27“Wamebarikiwa wale wafuao mavazi yao, ili wapate haki ya kuuendea huo mti wa uzima na kuuingia huo mji kupitia kwenye malango yake. 1522:15 Kum 23:18; Kol 3:5, 6; Flp 3:2Huko nje wako mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu, na kila mtu apendaye udanganyifu na kuufanya.

1622:16 Ufu 1:1, 4; 5:5; 2Pet 1:19; Ufu 2:28“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kushuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndimi Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya Asubuhi ingʼaayo.”

1722:17 Ufu 14:13Roho na bibi arusi wanasema, “Njoo!” Naye asikiaye na aseme, “Njoo!” Yeyote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na anywe maji ya uzima bure.

1822:18 Kum 12:32; Mit 30:6; Ufu 5:6; 16:21Namwonya kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Mtu yeyote akiongeza humo chochote, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 1922:19 Kum 4:2Kama mtu yeyote akipunguza humo chochote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

2022:20 Ufu 1:2; 1Kor 16:22Yeye anayeshuhudia mambo haya asema, “Hakika, naja upesi!”

Amen. Njoo, Bwana Yesu.

2122:21 Rum 16:20Neema ya Bwana Yesu iwe na watakatifu wote. Amen.