Philippians 4 – NIV & NEN

New International Version

Philippians 4:1-23

Closing Appeal for Steadfastness and Unity

1Therefore, my brothers and sisters, you whom I love and long for, my joy and crown, stand firm in the Lord in this way, dear friends!

2I plead with Euodia and I plead with Syntyche to be of the same mind in the Lord. 3Yes, and I ask you, my true companion, help these women since they have contended at my side in the cause of the gospel, along with Clement and the rest of my co-workers, whose names are in the book of life.

Final Exhortations

4Rejoice in the Lord always. I will say it again: Rejoice! 5Let your gentleness be evident to all. The Lord is near. 6Do not be anxious about anything, but in every situation, by prayer and petition, with thanksgiving, present your requests to God. 7And the peace of God, which transcends all understanding, will guard your hearts and your minds in Christ Jesus.

8Finally, brothers and sisters, whatever is true, whatever is noble, whatever is right, whatever is pure, whatever is lovely, whatever is admirable—if anything is excellent or praiseworthy—think about such things. 9Whatever you have learned or received or heard from me, or seen in me—put it into practice. And the God of peace will be with you.

Thanks for Their Gifts

10I rejoiced greatly in the Lord that at last you renewed your concern for me. Indeed, you were concerned, but you had no opportunity to show it. 11I am not saying this because I am in need, for I have learned to be content whatever the circumstances. 12I know what it is to be in need, and I know what it is to have plenty. I have learned the secret of being content in any and every situation, whether well fed or hungry, whether living in plenty or in want. 13I can do all this through him who gives me strength.

14Yet it was good of you to share in my troubles. 15Moreover, as you Philippians know, in the early days of your acquaintance with the gospel, when I set out from Macedonia, not one church shared with me in the matter of giving and receiving, except you only; 16for even when I was in Thessalonica, you sent me aid more than once when I was in need. 17Not that I desire your gifts; what I desire is that more be credited to your account. 18I have received full payment and have more than enough. I am amply supplied, now that I have received from Epaphroditus the gifts you sent. They are a fragrant offering, an acceptable sacrifice, pleasing to God. 19And my God will meet all your needs according to the riches of his glory in Christ Jesus.

20To our God and Father be glory for ever and ever. Amen.

Final Greetings

21Greet all God’s people in Christ Jesus. The brothers and sisters who are with me send greetings. 22All God’s people here send you greetings, especially those who belong to Caesar’s household.

23The grace of the Lord Jesus Christ be with your spirit. Amen.4:23 Some manuscripts do not have Amen.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wafilipi 4:1-23

14:1 Flp 1:8; 1Kor 16:13Kwa hiyo, ndugu zangu, ninaowapenda na ambao ninawaonea shauku, ninyi mlio furaha yangu na taji yangu, hivi ndivyo iwapasavyo kusimama imara katika Bwana, ninyi wapenzi wangu.

Mausia

24:2 Flp 2:2; 3:16Nawasihi Euodia na Sintike wawe na nia moja katika Bwana. 34:3 Flp 2:25; Ufu 20:12Naam, nakusihi wewe pia, mwenzangu mwaminifu, uwasaidie hawa wanawake, kwa sababu walijitaabisha katika kazi ya Injili pamoja nami bega kwa bega, wakiwa pamoja na Klementi na watendakazi wenzangu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.

44:4 Za 85:6; 97:12; Hab 3:18; Mt 5:12; Rum 12:12; Flp 3:1Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! 54:5 Za 119:151; 145:18; Ebr 10:37; Yak 5:8, 9Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. 64:6 Mt 6:25-34; Kol 4:2; 1Pet 5:7; Za 145:18; Efe 6:18; 1Tim 2:1Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 74:7 Isa 26:3; Yn 14:27; Efe 3:19Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

84:8 1The 5:22; Rum 12:17Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. 94:9 1Kor 4:16; Rum 12:17Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

Shukrani Kwa Matoleo Yenu

104:10 2Kor 11:9Nina furaha kubwa katika Bwana kwamba hatimaye mmeanza upya kushughulika tena na maisha yangu. Kweli mmekuwa mkinifikiria lakini mlikuwa hamjapata nafasi ya kufanya hivyo. 114:11 1Tim 6:6, 8; Ebr 13:5Sisemi hivyo kwa vile nina mahitaji, la! Kwa maana nimejifunza kuridhika katika hali yoyote. 124:12 1Kor 4:11; 2Kor 11:9Ninajua kupungukiwa, pia ninajua kuwa na vingi. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa kushiba na wakati wa kuona njaa, wakati wa kuwa na vingi na wakati wa kupungukiwa. 134:13 2Kor 12:9; Efe 3:16; Kol 1:11; 1Tim 1:12; 2Tim 4:17Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

144:14 Flp 1:7Lakini, mlifanya vyema kushiriki nami katika taabu zangu. 154:15 Flp 1:5; Mdo 16:9; 2Kor 11:8, 9Zaidi ya hayo, ninyi Wafilipi mnajua kwamba siku za kwanza nilipoanza kuhubiri Injili, nilipoondoka Makedonia, hakuna kanisa jingine lililoshiriki nami katika masuala ya kutoa na kupokea isipokuwa ninyi. 164:16 Mdo 17:1; 1The 2:9Kwa maana hata nilipokuwa huko Thesalonike, mliniletea msaada kwa ajili ya mahitaji yangu zaidi ya mara moja. 174:17 1Kor 9:11, 12Si kwamba natafuta sana yale matoleo, bali natafuta sana ile faida itakayozidi sana kwa upande wenu. 184:18 Flp 2:25; 2Kor 2:14Nimelipwa kikamilifu hata na zaidi; nimetoshelezwa kabisa sasa, kwa kuwa nimepokea kutoka kwa Epafrodito vile vitu mlivyonitumia, sadaka yenye harufu nzuri, dhabihu inayokubalika na ya kumpendeza Mungu. 194:19 Za 23:1; 2Kor 9:8; Rum 2:4Naye Mungu wangu atawajaza ninyi na kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu.

204:20 Gal 1:4; 1The 1:3; 3:11, 13; Rum 11:36Mungu wetu aliye Baba yetu apewe utukufu milele na milele. Amen.

Salamu Za Mwisho

214:21 Gal 1:2Msalimuni kila mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walioko pamoja nami wanawasalimu. 224:22 Mdo 9:13Watakatifu wote wanawasalimu, hasa wale watu wa nyumbani mwa Kaisari.

234:23 Rum 16:20; Gal 6:18Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.