Ezekiel 9 – NIV & NEN

New International Version

Ezekiel 9:1-11

Judgment on the Idolaters

1Then I heard him call out in a loud voice, “Bring near those who are appointed to execute judgment on the city, each with a weapon in his hand.” 2And I saw six men coming from the direction of the upper gate, which faces north, each with a deadly weapon in his hand. With them was a man clothed in linen who had a writing kit at his side. They came in and stood beside the bronze altar.

3Now the glory of the God of Israel went up from above the cherubim, where it had been, and moved to the threshold of the temple. Then the Lord called to the man clothed in linen who had the writing kit at his side 4and said to him, “Go throughout the city of Jerusalem and put a mark on the foreheads of those who grieve and lament over all the detestable things that are done in it.”

5As I listened, he said to the others, “Follow him through the city and kill, without showing pity or compassion. 6Slaughter the old men, the young men and women, the mothers and children, but do not touch anyone who has the mark. Begin at my sanctuary.” So they began with the old men who were in front of the temple.

7Then he said to them, “Defile the temple and fill the courts with the slain. Go!” So they went out and began killing throughout the city. 8While they were killing and I was left alone, I fell facedown, crying out, “Alas, Sovereign Lord! Are you going to destroy the entire remnant of Israel in this outpouring of your wrath on Jerusalem?”

9He answered me, “The sin of the people of Israel and Judah is exceedingly great; the land is full of bloodshed and the city is full of injustice. They say, ‘The Lord has forsaken the land; the Lord does not see.’ 10So I will not look on them with pity or spare them, but I will bring down on their own heads what they have done.”

11Then the man in linen with the writing kit at his side brought back word, saying, “I have done as you commanded.”

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 9:1-11

Waabudu Sanamu Wauawa

1Kisha nikamsikia akiita kwa sauti kubwa akisema, “Walete wasimamizi wa mji hapa, kila mmoja akiwa na silaha mkononi mwake.” 29:2 Dan 10:5; 12:6; Ufu 15:6; Eze 10:2; Law 16:4Nami nikaona watu sita wakija toka upande wa lango la juu, linalotazama kaskazini kila mmoja na silaha za kuangamiza mkononi mwake. Pamoja nao alikuwepo mtu aliyekuwa amevaa mavazi ya kitani safi, naye alikuwa na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande mmoja. Wakaingia ndani ya Hekalu wakasimama pembeni mwa madhabahu ya shaba.

39:3 1Sam 4:21; Eze 10:4; 11:22Basi utukufu wa Mungu wa Israeli ukaondoka hapo juu ya makerubi, ulikokuwa umekaa, ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Ndipo Bwana akamwita yule mtu aliyevaa kitani safi aliyekuwa na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande wake mmoja, 49:4 Mwa 4:15; 2Kor 1:22; Yer 7:29; Amo 6:6; Za 119:53; Kut 12:7; Yer 25:29akamwambia, “Pita katika mji wote wa Yerusalemu ukaweke alama juu ya vipaji vya nyuso za wale watu wanaohuzunika na kuomboleza kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.”

59:5 Yer 13:14; Eze 5:11; Kut 32:27; Isa 13:18Nikiwa ninasikia, akawaambia wale wengine, “Mfuateni anapopita katika mji wote mkiua, pasipo huruma wala masikitiko. 69:6 Eze 8:11-16; Yer 25:29; 1Pet 4:17; Yer 7:32; Mwa 4:15; Kut 12:7Waueni wazee, vijana wa kiume na wa kike, wanawake na watoto, lakini msimguse mtu yeyote mwenye alama. Anzieni katika mahali pangu patakatifu.” Kwa hiyo wakaanza na wale wazee waliokuwa mbele ya Hekalu.

79:7 Eze 6:7Ndipo akawaambia, “Linajisini Hekalu na mkazijaze kumbi zake maiti za wale waliouawa. Nendeni!” Kwa hiyo wakaenda wakaanza kuua watu mjini kote. 89:8 Yos 7:6; Hes 14:5; Amo 7:1-6; Eze 11:3; 7:8Wakati walikuwa wakiwaua watu, nami nilikuwa nimeachwa peke yangu, nikaanguka kifudifudi, nikapiga kelele nikisema, “Ee Bwana Mwenyezi! Je, utaangamiza mabaki yote ya Israeli, katika kumwagwa huku kwa ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?”

99:9 Za 58:2; Hab 1:4; Ay 22:13; Eze 14:23; Isa 29:15; Eze 22:13Bwana akanijibu, “Dhambi ya nyumba ya Israeli na Yuda imekuwa kubwa mno kupita kiasi, nchi imejaa umwagaji damu na mjini kumejaa udhalimu. Kwani wamesema, ‘Bwana ameiacha nchi, Bwana hauoni.’ 109:10 Yer 13:14; Eze 22:29; Isa 22:5; Eze 23:49; 8:18; Isa 22:5Kwa hiyo sitawahurumia wala kuwaachilia lakini nitaleta juu ya vichwa vyao, yale waliyoyatenda.”

11Ndipo mtu yule aliyekuwa amevaa nguo ya kitani safi na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande wake mmoja, akarudi na kutoa taarifa akisema, “Nimefanya kama ulivyoniagiza.”