Daniel 9 – NIV & NEN

New International Version

Daniel 9:1-27

Daniel’s Prayer

1In the first year of Darius son of Xerxes9:1 Hebrew Ahasuerus (a Mede by descent), who was made ruler over the Babylonian9:1 Or Chaldean kingdom— 2in the first year of his reign, I, Daniel, understood from the Scriptures, according to the word of the Lord given to Jeremiah the prophet, that the desolation of Jerusalem would last seventy years. 3So I turned to the Lord God and pleaded with him in prayer and petition, in fasting, and in sackcloth and ashes.

4I prayed to the Lord my God and confessed:

“Lord, the great and awesome God, who keeps his covenant of love with those who love him and keep his commandments, 5we have sinned and done wrong. We have been wicked and have rebelled; we have turned away from your commands and laws. 6We have not listened to your servants the prophets, who spoke in your name to our kings, our princes and our ancestors, and to all the people of the land.

7“Lord, you are righteous, but this day we are covered with shame—the people of Judah and the inhabitants of Jerusalem and all Israel, both near and far, in all the countries where you have scattered us because of our unfaithfulness to you. 8We and our kings, our princes and our ancestors are covered with shame, Lord, because we have sinned against you. 9The Lord our God is merciful and forgiving, even though we have rebelled against him; 10we have not obeyed the Lord our God or kept the laws he gave us through his servants the prophets. 11All Israel has transgressed your law and turned away, refusing to obey you.

“Therefore the curses and sworn judgments written in the Law of Moses, the servant of God, have been poured out on us, because we have sinned against you. 12You have fulfilled the words spoken against us and against our rulers by bringing on us great disaster. Under the whole heaven nothing has ever been done like what has been done to Jerusalem. 13Just as it is written in the Law of Moses, all this disaster has come on us, yet we have not sought the favor of the Lord our God by turning from our sins and giving attention to your truth. 14The Lord did not hesitate to bring the disaster on us, for the Lord our God is righteous in everything he does; yet we have not obeyed him.

15“Now, Lord our God, who brought your people out of Egypt with a mighty hand and who made for yourself a name that endures to this day, we have sinned, we have done wrong. 16Lord, in keeping with all your righteous acts, turn away your anger and your wrath from Jerusalem, your city, your holy hill. Our sins and the iniquities of our ancestors have made Jerusalem and your people an object of scorn to all those around us.

17“Now, our God, hear the prayers and petitions of your servant. For your sake, Lord, look with favor on your desolate sanctuary. 18Give ear, our God, and hear; open your eyes and see the desolation of the city that bears your Name. We do not make requests of you because we are righteous, but because of your great mercy. 19Lord, listen! Lord, forgive! Lord, hear and act! For your sake, my God, do not delay, because your city and your people bear your Name.”

The Seventy “Sevens”

20While I was speaking and praying, confessing my sin and the sin of my people Israel and making my request to the Lord my God for his holy hill— 21while I was still in prayer, Gabriel, the man I had seen in the earlier vision, came to me in swift flight about the time of the evening sacrifice. 22He instructed me and said to me, “Daniel, I have now come to give you insight and understanding. 23As soon as you began to pray, a word went out, which I have come to tell you, for you are highly esteemed. Therefore, consider the word and understand the vision:

24“Seventy ‘sevens’9:24 Or ‘weeks’; also in verses 25 and 26 are decreed for your people and your holy city to finish9:24 Or restrain transgression, to put an end to sin, to atone for wickedness, to bring in everlasting righteousness, to seal up vision and prophecy and to anoint the Most Holy Place.9:24 Or the most holy One

25“Know and understand this: From the time the word goes out to restore and rebuild Jerusalem until the Anointed One,9:25 Or an anointed one; also in verse 26 the ruler, comes, there will be seven ‘sevens,’ and sixty-two ‘sevens.’ It will be rebuilt with streets and a trench, but in times of trouble. 26After the sixty-two ‘sevens,’ the Anointed One will be put to death and will have nothing.9:26 Or death and will have no one; or death, but not for himself The people of the ruler who will come will destroy the city and the sanctuary. The end will come like a flood: War will continue until the end, and desolations have been decreed. 27He will confirm a covenant with many for one ‘seven.’9:27 Or ‘week’ In the middle of the ‘seven’9:27 Or ‘week’ he will put an end to sacrifice and offering. And at the temple9:27 Septuagint and Theodotion; Hebrew wing he will set up an abomination that causes desolation, until the end that is decreed is poured out on him.9:27 Or it9:27 Or And one who causes desolation will come upon the wing of the abominable temple, until the end that is decreed is poured out on the desolated city

Kiswahili Contemporary Version

Danieli 9:1-27

Maombi Ya Danieli

19:1 Dan 5:31; Ezr 4:6Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario mwana wa Ahasuero (mzaliwa wa Umedi), ambaye alifanywa mtawala juu ya ufalme wa Babeli, 29:2 Yer 29:10; Zek 7:5; Yer 25:11-12; 2Nya 36:21katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, mimi Danieli nilielewa kutokana na Maandiko, kulingana na neno la Bwana alilopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini. 39:3 2Sam 13:19; Neh 1:4; 2Nya 20:3; Yer 29:12; Dan 10:12; Yon 3:6Kwa hiyo nikamgeukia Bwana Mungu na kumsihi katika maombi na dua, katika kufunga, na kuvaa nguo ya gunia na kujipaka majivu.

49:4 Kum 7:9, 21; 1Fal 8:23, 30Nikamwomba Bwana Mungu wangu na kutubu:

“Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake, 59:5 Isa 53:6; Mao 1:20; Za 106:6; Mao 3:42; Ezr 9:6; Yer 8:14tumetenda dhambi na kufanya mabaya. Tumekuwa waovu na tumeasi; tumegeuka mbali na maagizo yako na sheria zako. 69:6 Yer 44:5; Yak 5:10; 2Fal 18:12; Ufu 10:7; 2Nya 36:16Hatukuwasikiliza watumishi wako manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, wakuu wetu, baba zetu, na watu wote wa nchi.

79:7 Ezr 9:7; Za 44:15; Kum 4:27; Amo 9:9; Eze 39:23-24; Yer 24:9; Isa 42:6“Bwana, wewe ni mwenye haki, lakini siku hii ya leo tumefunikwa na aibu: tukiwa wanaume wa Yuda, na watu wa Yerusalemu, na Israeli yote, wote walio karibu na walio mbali, katika nchi zote ulikotutawanya kwa sababu ya kukosa uaminifu kwako. 89:8 Neh 9:33; Yer 14; 20; Eze 16:63Ee Bwana, sisi na wafalme wetu, wakuu wetu na baba zetu tumefunikwa na aibu kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako. 99:9 Kut 34:7; Hes 14:18; Neh 9:17; Yer 14:7; Za 130:4; Yer 42:12; 2Sam 24:14Bwana Mungu wetu ni mwenye rehema na anayesamehe, hata ingawa tumefanya uasi dhidi yake. 109:10 2Fal 18:12; Ufu 10:7; 2Fal 17:13-15Hatukumtii Bwana Mungu wetu wala kuzishika sheria alizotupa kupitia kwa watumishi wake manabii. 119:11 Isa 1:4-7; Yer 8:5-10; Kum 27:15-26; Yer 2:29; 2Fal 22:16; Kum 11:26; 28:15; 2Fal 17:23Israeli yote imekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii.

“Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako. 129:12 Isa 44:26; Yoe 2:2; Zek 1:6; 7:12; Mao 2:17; Yer 30:7; 4:23; Dan 12:1Umetimiza maneno uliyosema dhidi yetu na dhidi ya watawala wetu, kwa kuleta maafa makubwa juu yetu. Chini ya mbingu yote kamwe hapajatendeka kitu kama kile kilichotendeka kwa Yerusalemu. 139:13 Isa 9:13; Yer 2:30; Isa 31:1; Kum 4:29Kama vile ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, misiba hii yote imekuja juu yetu, lakini hatujaomba fadhili kwa Bwana Mungu wetu kwa kugeuka kutoka dhambi zetu na kuwa wasikivu katika kweli yake. 149:14 Yer 18:8; 44:27; Neh 9:33; Yer 32:23; Mwa 18:25; 2Nya 12:6; Yer 40:3Bwana hakusita kuleta maafa juu yetu, kwa maana Bwana Mungu wetu ni mwenye haki katika kila afanyalo; lakini hata hivyo hatujamtii.

159:15 Kut 3:20; Yer 32:21; Neh 9:10“Sasa, Ee Bwana Mungu wetu, ambaye uliwatoa watu wako Misri kwa mkono wenye nguvu, na ambaye umejifanyia Jina linalodumu mpaka leo, tumetenda dhambi, tumefanya mabaya. 169:16 Amu 5:11; Kut 15:17; Zek 8:2; Za 39:8; Eze 5:14; Isa 5:25Ee Bwana, wewe kwa kadiri ya matendo yako ya haki, ondoa hasira yako na ghadhabu yako juu ya Yerusalemu, mji wako, mlima wako mtakatifu. Dhambi zetu na maovu ya baba zetu yameifanya Yerusalemu na watu wako kitu cha kudharauliwa kwa wale wote wanaotuzunguka.

179:17 Hes 6:24-26; Za 80:19“Basi Mungu wetu, sasa sikia maombi na dua ya mtumishi wako. Ee Bwana, kwa ajili yako angalia kwa huruma ukiwa wa mahali pako patakatifu. 189:18 Za 80:14; Kum 28:10; Isa 37:17; Yer 7:10-12; 25:29; Lk 18:13Ee Mungu, tega sikio na ukasikie; fumbua macho yako ukaone ukiwa wa mji ule wenye Jina lako. Hatukutolei maombi yetu kwa sababu sisi tuna haki, bali kwa sababu ya rehema zako nyingi. 199:19 Za 44:23; 1Sam 12:22Ee Bwana, sikiliza! Ee Bwana, samehe! Ee Bwana, sikia na ukatende! Kwa ajili yako, Ee Mungu wangu, usikawie, kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa Jina lako.”

Majuma Sabini

209:20 Za 145:18; Isa 58:9; Ezr 10:1Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na nikifanya maombi yangu kwa Bwana Mungu wangu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu, 219:21 Dan 8:16; Lk 1:19; Kut 29:39wakati nilipokuwa bado katika maombi, Gabrieli, yule mtu niliyekuwa nimemwona katika maono hapo awali, alinijia kwa kasi karibu wakati wa kutoa dhabihu ya jioni. 229:22 Dan 7:16; 10:14; Amu 3:7Akanielimisha na kuniambia, “Danieli, sasa nimekuja kukupa akili na ufahamu. 239:23 Dan 10:19; Lk 1:24; Dan 10:11-12; Mt 24:15; Isa 65:24Mara ulipoanza kuomba, jibu lilitolewa, ambalo nimekuja kukupasha habari, kwa maana wewe unapendwa sana. Kwa hiyo, tafakari ujumbe huu na uelewe maono haya:

249:24 Isa 53:10; 56:1; Ebr 9:12; Isa 1:26“Majuma sabini yameamriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu, ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii, na pia kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu sana.

259:25 Ezr 4:24; 6:15; Yn 4:25; 1Sam 13:14; Ezr 3:3“Ujue na kuelewa hili: Tangu kutolewa kwa amri ya kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu mpaka kuja kwa Mpakwa mafuta, aliye mtawala, kutakuwako majuma saba na majuma sitini na mawili. Barabara zitajengwa tena pamoja na mahandaki, lakini katika wakati wa taabu. 269:26 Isa 53:8; Mt 16:21; Isa 28:2; Nah 1:8; Dan 1:8; 11:10; Za 46:8; Zek 4:14; Hag 2:23Baada ya majuma sitini na mawili, Mpakwa Mafuta atakatiliwa mbali, wala hatabaki na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea mpaka mwisho, nao ukiwa umeamriwa. 279:27 Isa 10:22Mtawala huyo atathibitisha agano na watu wengi kwa juma moja. Katikati ya juma hilo atakomesha dhabihu na sadaka. Mahali pa dhabihu katika Hekalu atasimamisha chukizo la uharibifu, hadi mwisho ulioamriwa utakapomiminwa juu yake yeye aletaye uharibifu.”