Acts 10 – NIV & NEN

New International Version

Acts 10:1-48

Cornelius Calls for Peter

1At Caesarea there was a man named Cornelius, a centurion in what was known as the Italian Regiment. 2He and all his family were devout and God-fearing; he gave generously to those in need and prayed to God regularly. 3One day at about three in the afternoon he had a vision. He distinctly saw an angel of God, who came to him and said, “Cornelius!”

4Cornelius stared at him in fear. “What is it, Lord?” he asked.

The angel answered, “Your prayers and gifts to the poor have come up as a memorial offering before God. 5Now send men to Joppa to bring back a man named Simon who is called Peter. 6He is staying with Simon the tanner, whose house is by the sea.”

7When the angel who spoke to him had gone, Cornelius called two of his servants and a devout soldier who was one of his attendants. 8He told them everything that had happened and sent them to Joppa.

Peter’s Vision

9About noon the following day as they were on their journey and approaching the city, Peter went up on the roof to pray. 10He became hungry and wanted something to eat, and while the meal was being prepared, he fell into a trance. 11He saw heaven opened and something like a large sheet being let down to earth by its four corners. 12It contained all kinds of four-footed animals, as well as reptiles and birds. 13Then a voice told him, “Get up, Peter. Kill and eat.”

14“Surely not, Lord!” Peter replied. “I have never eaten anything impure or unclean.”

15The voice spoke to him a second time, “Do not call anything impure that God has made clean.”

16This happened three times, and immediately the sheet was taken back to heaven.

17While Peter was wondering about the meaning of the vision, the men sent by Cornelius found out where Simon’s house was and stopped at the gate. 18They called out, asking if Simon who was known as Peter was staying there.

19While Peter was still thinking about the vision, the Spirit said to him, “Simon, three10:19 One early manuscript two; other manuscripts do not have the number. men are looking for you. 20So get up and go downstairs. Do not hesitate to go with them, for I have sent them.”

21Peter went down and said to the men, “I’m the one you’re looking for. Why have you come?”

22The men replied, “We have come from Cornelius the centurion. He is a righteous and God-fearing man, who is respected by all the Jewish people. A holy angel told him to ask you to come to his house so that he could hear what you have to say.” 23Then Peter invited the men into the house to be his guests.

Peter at Cornelius’s House

The next day Peter started out with them, and some of the believers from Joppa went along. 24The following day he arrived in Caesarea. Cornelius was expecting them and had called together his relatives and close friends. 25As Peter entered the house, Cornelius met him and fell at his feet in reverence. 26But Peter made him get up. “Stand up,” he said, “I am only a man myself.”

27While talking with him, Peter went inside and found a large gathering of people. 28He said to them: “You are well aware that it is against our law for a Jew to associate with or visit a Gentile. But God has shown me that I should not call anyone impure or unclean. 29So when I was sent for, I came without raising any objection. May I ask why you sent for me?”

30Cornelius answered: “Three days ago I was in my house praying at this hour, at three in the afternoon. Suddenly a man in shining clothes stood before me 31and said, ‘Cornelius, God has heard your prayer and remembered your gifts to the poor. 32Send to Joppa for Simon who is called Peter. He is a guest in the home of Simon the tanner, who lives by the sea.’ 33So I sent for you immediately, and it was good of you to come. Now we are all here in the presence of God to listen to everything the Lord has commanded you to tell us.”

34Then Peter began to speak: “I now realize how true it is that God does not show favoritism 35but accepts from every nation the one who fears him and does what is right. 36You know the message God sent to the people of Israel, announcing the good news of peace through Jesus Christ, who is Lord of all. 37You know what has happened throughout the province of Judea, beginning in Galilee after the baptism that John preached— 38how God anointed Jesus of Nazareth with the Holy Spirit and power, and how he went around doing good and healing all who were under the power of the devil, because God was with him.

39“We are witnesses of everything he did in the country of the Jews and in Jerusalem. They killed him by hanging him on a cross, 40but God raised him from the dead on the third day and caused him to be seen. 41He was not seen by all the people, but by witnesses whom God had already chosen—by us who ate and drank with him after he rose from the dead. 42He commanded us to preach to the people and to testify that he is the one whom God appointed as judge of the living and the dead. 43All the prophets testify about him that everyone who believes in him receives forgiveness of sins through his name.”

44While Peter was still speaking these words, the Holy Spirit came on all who heard the message. 45The circumcised believers who had come with Peter were astonished that the gift of the Holy Spirit had been poured out even on Gentiles. 46For they heard them speaking in tongues10:46 Or other languages and praising God.

Then Peter said, 47“Surely no one can stand in the way of their being baptized with water. They have received the Holy Spirit just as we have.” 48So he ordered that they be baptized in the name of Jesus Christ. Then they asked Peter to stay with them for a few days.

Kiswahili Contemporary Version

Matendo 10:1-48

Kornelio Amwita Petro

110:1 Mdo 8:40Katika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu jina lake Kornelio, ambaye alikuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia. 210:2 Mdo 13:16-26Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na wote wa nyumbani mwake. Aliwapa watu sadaka nyingi na kumwomba Mungu daima. 310:3 Mdo 3:1; 9:10; 5:19Siku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, “Kornelio!”

410:4 Za 20:3; Mt 10:42; Ufu 8:4Kornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?”

Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. 510:5 Mdo 9:36Sasa tuma watu waende Yafa wakamwite mtu mmoja jina lake Simoni aitwaye Petro. 610:6 Mdo 9:43Yeye anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.”

7Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye alipoondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili pamoja na askari mmoja mcha Mungu aliyekuwa miongoni mwa wale waliomtumikia. 810:8 Mdo 9:36Akawaambia mambo yote yaliyotukia, kisha akawatuma waende Yafa.

Maono Ya Petro

910:9 Mt 24:17; Mdo 11:5Siku ya pili yake, walipokuwa wameukaribia mji, wakati wa adhuhuri, Petro alipanda juu ya nyumba kuomba. 1010:10 Mdo 22:17Alipokuwa akiomba akahisi njaa, akatamani kupata chakula. Lakini wakati walikuwa wakiandaa chakula, akalala usingizi mzito sana. 1110:11 Mdo 11:5-17; Mt 3:16; Ufu 19:11Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama nguo kubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne. 12Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani. 13Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.”

1410:14 Mdo 9:5; Kum 14:3-20; Eze 4:14Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”

1510:15 Mwa 9:3; Tit 1:15Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.”

16Jambo hili lilitokea mara tatu na ghafula ile nguo ikarudishwa mbinguni.

1710:17 Mdo 9:10; 10:7, 8Wakati Petro akiwa bado anajiuliza kuhusu maana ya maono haya, wale watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakaipata nyumba ya Simoni mtengenezaji wa ngozi wakawa wamesimama mbele ya lango. 18Wakabisha hodi na kuuliza kama Simoni aliyeitwa Petro alikuwa anaishi hapo.

1910:19 Mdo 8:29; 13:2; 15:28Wakati Petro akiwa anafikiria juu ya yale maono, Roho Mtakatifu akamwambia, “Simoni, wako watu watatu wanaokutafuta. 2010:20 Mdo 15:7-9Inuka na ushuke, usisite kwenda nao kwa kuwa mimi nimewatuma.”

21Petro akashuka na kuwaambia wale watu waliokuwa wametumwa kutoka kwa Kornelio, “Mimi ndiye mnayenitafuta. Mmekuja kwa sababu gani?”

2210:22 Mdo 11:14Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani kwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.” 2310:23 Mdo 1:16Basi Petro akawakaribisha wakafuatana naye ndani, akawapa pa kulala. Kesho yake akaondoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu kutoka Yafa wakafuatana naye.

Petro Nyumbani Mwa Kornelio

2410:24 Mdo 8:40Siku iliyofuata wakawasili Kaisaria. Kornelio alikuwa akiwangoja pamoja na jamaa yake na marafiki zake wa karibu. 25Petro alipokuwa akiingia ndani, Kornelio alikuja kumlaki, akaanguka miguuni pake kwa heshima. 2610:26 Ufu 19:10; 22:8-9Lakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama, mimi ni mwanadamu tu.”

27Petro alipokuwa akizungumza naye akaingia ndani na kukuta watu wengi wamekusanyika. 2810:28 Yn 4:9; 18:28; Mdo 15:8-9Akawaambia, “Mnajua kabisa kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu wa Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwite mtu yeyote kuwa najisi au asiye safi. 29Ndiyo sababu ulipotuma niitwe nilikuja bila kupinga lolote. Basi sasa naomba unieleze kwa nini umeniita?”

3010:30 Mt 28:3; Mk 16:5; Lk 24:4; Yn 20:12Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa alasiri. Ghafula mtu aliyevaa nguo zilizongʼaa akasimama mbele yangu, 3110:31 Mdo 10:4; Dan 10:12; Ebr 6:10akasema, ‘Kornelio, maombi yako yamesikiwa na sadaka zako kwa maskini zimekumbukwa mbele za Mungu. 32Basi tuma watu waende Yafa wakaulize mtu mmoja Simoni aitwaye Petro, yeye ni mgeni katika nyumba ya Simoni mtengenezaji ngozi, ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.’ 33Nilituma watu kwako mara moja, nawe umefanya vyema kuja. Basi sasa sisi sote tuko hapa mbele za Mungu kuyasikiliza yote ambayo Bwana amekuamuru kutuambia.”

Hotuba Ya Petro

3410:34 Ay 34:19; Mk 12:14Ndipo Petro akafungua kinywa chake akasema, “Mungu hana upendeleo, 3510:35 Mdo 15:9Lakini katika kila taifa, kila mtu amchaye na kutenda yaliyo haki hukubaliwa naye. 3610:36 Mdo 13:32; Lk 2:14; Mt 28:18Ninyi mnajua ule ujumbe uliotumwa kwa Israeli, ukitangaza habari njema za amani kwa Yesu Kristo. Yeye ni Bwana wa wote. 3710:37 Lk 4:14; Mt 4:12-17Mnajua yale yaliyotukia katika Uyahudi wote kuanzia Galilaya baada ya mahubiri ya Yohana Mbatizaji: 3810:38 Mdo 4:26; Mt 4:23; Yn 3:2Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi alivyokwenda huku na huko akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za ibilisi, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.

3910:39 Lk 24:48; Mdo 5:30“Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika Uyahudi na Yerusalemu. Wakamuua kwa kumtundika msalabani. 4010:40 Mdo 2:24Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu siku ya tatu na akamwezesha kuonekana na watu. 4110:41 Yn 14:17-22; Lk 24:43; Yn 21:13Hakuonekana kwa watu wote, lakini kwetu sisi tuliochaguliwa na Mungu kuwa mashahidi, ambao tulikula na kunywa naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. 4210:42 Mt 28:19-20; 2Tim 4:11; 1Pet 4:5Naye alituamuru kuhubiri kwa watu wote na kushuhudia kwamba ndiye alitiwa mafuta na Mungu kuwa hakimu wa walio hai na wafu. 4310:43 Isa 53:11; Mdo 26:22; 15:9Manabii wote walishuhudia juu yake kwamba kila mtu amwaminiye hupokea msamaha wa dhambi katika Jina lake.”

Watu Wa Mataifa Wapokea Roho Mtakatifu

4410:44 Lk 1:15; Mdo 19:6Wakati Petro alikuwa akisema maneno haya, Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wakisikiliza ule ujumbe. 4510:45 Mdo 2:33-38; 11:18; 15:8Wale wa tohara walioamini waliokuja na Petro walishangaa kwa kuona kuwa kipawa cha Roho Mtakatifu kimemwagwa juu ya watu wa Mataifa. 4610:46 Mk 16:17Kwa kuwa waliwasikia wakinena kwa lugha mpya na kumwadhimisha Mungu.

Ndipo Petro akasema, 4710:47 Mdo 8:36; 11:17; Yn 20:22“Je, kuna mtu yeyote anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.” 4810:48 Mdo 2:38; 8:16Kwa hiyo akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Wakamsihi Petro akae nao kwa siku chache.